To His Excellency Hakainde Hichilema, President-elect of the Republic of Zambia: on behalf of the Government and the people of the United Republic of Tanzania, I extend my heartfelt congratulations on your re-election as the President of the Republic of Zambia.
I am looking forward to continuing working with you in strengthening the deep, historical and fraternal bonds between Tanzania and Zambia for the benefits of our people and our two nations.
Mr President-elect, you have my best wishes.
God bless you. God bless Zambia. God bless Africa.
Ikulu Ndogo, Zanzibar.
Mapema leo nimefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Mheshimiwa Fรฉlix Antoine Tshisekedi Tshilombo, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi. Mazungumzo yetu yamejikita katika kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na DRC, hususan katika kuunganisha nchi zetu kupitia ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara kwa kuondoa vikwazo visivyo vya lazima, kuboresha huduma za mipakani na kuwezesha ushiriki zaidi wa sekta binafsi katika shughuli za maendeleo.
Tanzania ina fursa kubwa katika uzalishaji wa bidhaa za kilimo, uvuvi na mifugo, hivyo nimeikaribisha DRC kutumia fursa hizo katika kuongeza biashara na Tanzania. Aidha, tumekubaliana kuendeleza ushirikiano katika sekta ya madini, kuanzia uchimbaji, uongezaji thamani na masoko hadi tafiti na kubadilishana uzoefu na ujuzi, ikiwemo kupitia Kituo chetu cha Madini.
Tumesisitiza pia umuhimu wa kuendelea kushirikiana katika masuala ya amani na usalama, kwa lengo la kuimarisha utulivu na ustawi wa wananchi wa Tanzania, DRC na ukanda wetu kwa ujumla.
Leo ni siku kubwa na ya kihistoria kwa nchi yetu ambapo nimezindua Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), hatua inayotimiza maono ya zaidi ya miaka 50 ya Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Nyerere, ya kuzalisha umeme katika Mto Rufiji ili kuchochea maendeleo yetu. Ninawashukuru watangulizi wangu, viongozi na watendaji wa Wizara na taasisi mbalimbali, pamoja na wananchi, kwa mchango wao mkubwa katika kukamilisha safari hii.
JNHPP ni kielelezo cha uwezo wetu wa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, pia ni ushahidi kuwa nchi za Afrika zikishirikiana zinaweza kufanikisha mambo makubwa yenye maslahi kwa watu wetu. Pamoja na manufaa mengine, mradi huu umeongeza uwezo wetu wa kuzalisha umeme hadi megawati 4,646, hivyo kutuhakikishia umeme wa uhakika nchini na ziada ambayo tutaiuza kwa nchi jirani, pia umetoa ajira kwa maelfu ya vijana wetu na kuwapa ujuzi na uzoefu.
Ninawasihi Watanzania kuchangamkia fursa zinazotokana na mradi huu, kutunza mazingira, hasa vyanzo vya maji, pamoja na kulinda miundombinu yake ili udumu na kuhudumia vizazi vijavyo. Aidha, nimeielekeza Wizara ya Nishati kuongeza kasi katika ujenzi wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme, ili wananchi waone tija ya uwekezaji huu kwenye maisha yao na maendeleo ya Taifa letu.
Mungu Ibariki Tanzania.
Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), Rufiji, Pwani
Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kutuwezesha kushuhudia tukio hili la kihistoria kwa Taifa letu. Hii ni hatua ya kujivunia katika safari yetu ya kuendelea kufanya kazi ya kujikomboa kiuchumi, ili kuiishi maana halisi ya Uhuru wetu, pamoja na malengo na ndoto za waasisi wetu.
Hongera kwa kila Mtanzania.
๐Dar es Salaam
โช๏ธWAZIRI KOMBO ATETA NA BALOZI MKINGULE, AMHIMIZA KUIMARISHA MAHUSIANO YA TANZANIA NA CUBA
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.), amekutana kwa mazungumzo na Balozi mteule wa Tanzania nchini Cuba, Luteni Jenerali Mathew Mkingule, anayetarajiwa kuanza rasmi majukumu yake ya kidiplomasia.
Akizungumza Aprili 27, 2026 katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam, Waziri Kombo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha uhusiano wa kihistoria uliopo kati ya Tanzania na Cuba.
Amemtaka Balozi Mkingule kutumia vyema uzoefu alioupata alipokuwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia ili kuongeza tija katika ushirikiano wa kisiasa, kiuchumi na kijamii kati ya mataifa hayo mawili.
Kwa upande wake, Balozi Mkingule amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kuiwakilisha Tanzania nchini Cuba.
Aidha, amemhakikishia Waziri Kombo kuwa atafanya kazi kwa bidii kuimarisha na kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya Tanzania na Cuba kwa manufaa ya pande zote mbili.
Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha mwigizaji mkongwe wa filamu nchini, Hashim Kambi kilichotokea leo, Dar es Salaam. Taifa limepoteza kipaji adhimu kilichochangia kwa kiasi kikubwa kukuza na kuitangaza tasnia ya filamu nchini.
Ninatoa pole kwa Shirikisho la Filamu Tanzania, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), wasanii wa filamu nchini, familia ya marehemu, wadau wa filamu, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
โZipo pia hasara kwa upande wa Sekta ya Fedha, kwa mfano, jumla ya sh. milioni 621.7 ziliiporwa kutoka kwenye viotomotela (ATM) vya Mabenki makubwa matatu, CRDB, NMB na NBC.โ
Sekta nyingine zilizoathirika kiuchumi ni kushuka kwa Masoko ya Fedha, mabadiliko ya mzunguko wa fedha, usafiri na usafirishaji, na utalii.
โWajasiriamali wadogo na wa kati waliporwa au kuibwa mali zenye thamani ya sh. bilioni 1.6. Shahidi kutoka Tegeta, Dar es Salaam aliyeeleza kuwa: โMimi ni mfanya biasara wa simu, siku ya Uchaguzi Mkuu duka langu lilivamiwa na wafanya vurugu wakaiba simu zote ndani ya duka, simu zenyewe ni za mkopo, nina hali mbaya sana hata sijui nitafanyaje, uwezo wangu haupo tena, hapa nilipo nimejaa msongo wa mawazo.โ
Hata hivyo, wawakilishi wa taasisi za kimataifa, ikiwemo Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Madola, tayari wamefika nchini na kuahidi kushirikiana na Tanzania katika hatua hii ya kitaifa. Hivyo basi, hoja ya kutaka kupuuzwa kwa mchakato uliopo haina msingi.
Kwa kuwa nia ya baadhi ya wanasiasa hawa inaonekana kuendelea kuwatumia Watanzania kwa maslahi ya kisiasa, ni muhimu kwa wananchi kuendelea kuwa macho na kuwakataa. Changamoto tuliyoipitia isijirudie tena.
Siku moja baada ya kutolewa kwa ripoti ya Tume ya Uchunguzi wa matukio yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2025 hali ni shwari nchini. Watanzania wanaendelea na shughuli zao. Mamilioni kwa mamilioni waliofuatilia uwasilishwaji wa ripoti na mapendekezo yake wanayo matumaini ya kusonga mbele kuonesha kuumizwa na ghasia zilizotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu 2025.
Hata hivyo, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT Wazalendo vimejitokeza kuipinga kazi iliyofanywa na Tume hiyo. Hata hivyo, hoja wanazozitoa zinaonekana kuwa dhaifu, hasa tukizingatia mustakabali wa nchi yetu na madhara tuliyoyapitia.
Ni muhimu kujiuliza: kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025, hali ya nchi ilikuwa shwari. Mambo yalianza kubadilika pale chokochoko za kupandikiza chuki na kuandaa ghasia zilipoanza kushika kasi. Kwa mujibu wa taarifa ya uchunguzi iliyotolewa jana, uratibu wa ghasia hizo ulianza takribani miezi sita kabla ya uchaguzi kufanyika. Baada ya kupita kwa kipindi hicho cha ghasia - ambacho ripoti imeeleza bayana kuwa ghasia hizo zilipangwa, zilifadhiliwa na kutekelezwa na watu waliopata mafunzo - Watanzania walio wengi walitamani kurejea katika amani yao waliyoizoea. Hawakutaka tena kutumika kama nyenzo ya wanasiasa kwa maslahi yao binafsi.
Baada ya kutolewa kwa ripoti, amani na utulivu vikiendelea kutamalaki, CHADEMA na ACT Wazalendo wametoa matamko yao kwa umma wakieleza sababu mbalimbali za kupinga ripoti hiyo. Katika taarifa yake, CHADEMA imedai kuwa kwa mujibu wa Sheria ya Uchunguzi (Commissions of Inquiry Act, 2002; Sura ya 32 kama ilivyorekebishwa mwaka 2023), Tume ni chombo cha Rais kinachofanya kazi kwa matakwa na maelekezo yake. Kwa mantiki hiyo, wamejaribu kuuaminisha umma kuwa Tume si chombo huru na hakiwezi kutoa ukweli wala haki, hasa katika mazingira ambayo serikali ndiyo wanayoituhumu.
Hoja wanayoieneza inahitaji ufafanuzi wa kisheria. Ni kweli kwamba Rais, kama Mkuu wa Nchi na Amiri Jeshi Mkuu, ana mamlaka ya kuunda Tume kwa mujibu wa Ibara ya 36(2) ya Katiba na Kifungu cha 3 cha Sheria ya Uchunguzi. Lakini kwa kutambua kuwa Tume ni chombo cha nchi, kifungu cha 6 cha Sheria ya Uchunguzi kinaweka bayana kuwa Tume haitakoma wala kuathiriwa kwa namna yoyote kutokana na kifo, kutokuwepo au kuondolewa madarakani kwa Rais aliyeiunda. Hii ni kinga muhimu ya kisheria inayolinda uhuru wa Tume katika kutekeleza majukumu yake.
Zaidi ya hapo, vifungu vya 9, 11 na 12 vya Sheria hiyo vinaipa Tume mamlaka ya kufanya kazi kwa uhuru, kujiwekea kanuni za uendeshaji wa kazi zake, na hata kutumia mamlaka ya Mahakama Kuu katika kuita mashahidi na kuhitaji taarifa zozote muhimu kwa uchunguzi wake. Hivyo basi, madai ya CHADEMA kuhusu ukosefu wa uhuru wa Tume ni upotoshaji mkubwa.
Ni muhimu pia kukumbuka kuwa CHADEMA walisusia uchaguzi, na pia hawakujitokeza mbele ya Tume. Leo hii wanajaribu kuibua hoja nyingine mpya, jambo linalopaswa kueleweka mapema na Watanzania wapenda amani ili wasipotoshwe.
Kwa upande mwingine, ACT Wazalendo nao wameikataa ripoti hiyo kwa hoja zinazofanana - wakidai kuwa Tume haina uhuru na iliundwa kulinda wahusika badala ya kutoa haki. Hoja hii inakosa mashiko pia, ukizingatia taarifa imegusia mambo mbalimbali, yakiwemo masuala yanayohitaji uwajibikaji.
Ni wazi kuwa CHADEMA na ACT Wazalendo ni wadau muhimu katika siasa za Tanzania. Hata hivyo, katika hatua hii, wanaonekana kuyumba baada ya kuona kuwa mkakati wa chuki waliouanzisha haukuzaa matokeo waliyotarajia. Aidha, kwa kususia mchakato wa Tume, wamejinyima wenyewe fursa ya kusikilizwa.
Ikumbukwe kuwa Mwenyekiti wa Tume, Jaji Mohamed Chande Othman, alieleza wazi kuwa Tume iliwafikia zaidi ya watu 63,000 na ilitoa fursa kwa kila mtu au taasisi iliyotaka kushiriki kufanya hivyo bila kikwazo. Wapo waliochagua kutoshiriki, wakiwa na matarajio kwamba wangeendelea kushinikiza ili vyombo vingine wanavyovitaka wao vije kufanya uchunguzi huo nchini.
Unamjua lakini? Ni kijana aliyezaliwa mwaka 1981. Haiba yake na sura yake haviendani na umri mdogo alio nao. Kwa nini? Amejaa ganzi na gesi zinazomfanya ajisikie kuripuka kila wakati. Fikiria, ni kijana anayetoka eneo lililobarikiwa na Mungu madini ya kutosha ya dhahabu. Akili yake isivyoweza kuona mbali, amejiweka kwenye harakati za kuichafua nchi yake badala ya kukamata fursa. Ni mwanasiasa aliyefilisika katika mambo yafuatayo:
1. Alitaka kuwa Chacha Wangwe mpya. Watanzania walimshtukia mapema na kumweka sehemu anayostahili.
2. Alishiriki kampeni ya kumpaka matope Freeman Mbowe kwa kumsaidia Tundu Lissu kuendesha kampeni ya kumdhalilisha mwenyekiti wake. Juhudi zake hizo, zimekigawa chama chake na baadhi ya viongozi kukimbilia kwingineko.
3. Anatamani Tundu Lissu aendelee kukaa ndani ili atumie nafasi hiyo kuongoza chama chake kwa kipindi kirefu.
4. Anatamani kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Kila akimtazama Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba anazidi kuumia roho, akihisi yeye ndiye angefaa kuchukua nafasi hiyo. Uwaziri Mkuu ni nafasi yenye heshima yake; siyo ya wavuta bangi wa milimani.
5. Alianzisha kampeni haramu ya kuwakimbiza wawekezaji wa uchimbaji wa madini wa Kampuni ya North Mara huko kwao Nyamango, akiwahamasisha vijana kuvamia mgodi kila mara. Kiu yake ya kutafuta umaarufu kwa gharama ya damu za watu iliendelea kumwanika vibaya kama mwanasiasa aliyefilika.
6. Ni mwanasiasa anayehamasisha siasa za chuki na kutumia damu za watanzania ili kufikia maslahi yake ya kisiasa.
7. Ni mwanasiasa anayeamini kuwa Tanzania inatakiwa kuongozwa na umoja wa mataifa โ msimamo unaoanika akili kisoda alizo nazo. Anajitoa akili kuwa alitaka kuzuia uchaguzi ambao chama chake hakikushiriki na akashindwa. Kumbe yeye na chama chao walikuwa wanaamini kuwa nchi yetu inapaswa kukabidhiwa umoja wa mataifa. Imagine!
Na Mwandishi maalum
Kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuhusu kuundwa kwa Tume ya Uchunguzi itakayochunguza kwa kina yale yaliyobainishwa kwenye ripoti ya Tume ya Rais ya iliyoundwa kuchunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea Oktoba 29, 2025 imeungwa mkono na Watanzania walio wengi, hongera Mhe Rais kwa uamuzi huu.
Ni wazi kuwa, Kiongozi wetu ana maono makubwa yanayolenga kuendelea kuliunganisha Taifa la Tanzania ambalo limeendelea kuwa moja na lenye misingi imara iliyojengwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, Watanzania tunaungana na Kiongozi wetu katika kuhakikisha kuwa Tume itakayoundwa inatekeleza majukumu yake ya uchunguzi kwa ufanisi ili nchi yetu iendelee mbele zaidi katika Nyanja zote katika kujenga umoja wa kitaifa ulio imara zaidi.
Akizungumza na moja ya Chombo cha habari Prof. Palamagamba Kabudi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge ambaye pia ni nguli wa Sheria ameonesha kuwa jambo hili limekuja wakati muafa na litasaidia Taifa kupiga hatua katika kuleta maridhiano na kuimarisha zaidi umoja wa kitaifa.
โTume imesema kuna watu wamepanga, kutekeleza na kufadhili matukio ya Oktoba 29, 2026,โ anaeleza Prof. Kabudi, hivyo ni muhimu Tume itakayoundwa kufanya uchunguzi wa masuala yote ya jinai yaliyobainishwa ikapewa nafasi na ikaaminiwa katika kutekeleza jukumu hili la kiuchunguzi kuhusu masuala yote yaliyoainishwa na ripoti ya Jaji Chande.
Serikali ya Awamu ya Sita ina utashi wa kisiasa katika kujenga umoja wa kitaifa na imekuwa nyakati zote ikifanya kazi kwa kuweka maslahi ya Watanzania mbele nyakati zote. Jukumu letu kama watanzania ni kuangalia tulipotoka, tulipo na tunapotaka kwenda kwa maslahi ya Taifa letu, heko watanzania kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa.
โAmani, Umoja na Mshikamano ndio msingi wa maendeleo yetuโ Mwl Nyerere alisisitiza kuwa bila amani hakuna maendeleo yoyote yanayoweza kupatikana. Dhamira ya kufanyika kwa uchunguzi wa kina inatuelekeza kwenye kuendelea kutibu tatizo na kuepuka masuala kama haya kujirudia.
Hivi Karibuni, Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Dkt Fredrick Shoo ameonesha wazi kuwa Ripoti ya Tume ya Rais ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani ya Oktoba 29, 2025 imekuja kuliponya Taifa. Jukumu la Kila Mtanzania ni kulinda amani na kuungana na viongozi wetu katika kuwezesha Tume ya uchunguzi itakayoundwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.