Je, unataka kuwa wa kwanza kupata updates za MACA Gulio bila kelele za magroup ya WhatsApp? 🤫
Tumezindua Channel yetu! Uzuri wa hii Channel:
✅ Namba yako ya simu inabaki kuwa siri (Privacy).
✅ Hupati usumbufu wa meseji nyingi. https://t.co/GgHHJwEuJH
Kimsingi Mahakama Kuu imezima jaribio la Serikali la kutaka kuingiza mambo ya Oktoba 29 kwa mlango wa nyuma. TAL amewalazimisha Jamhuri kurejea katika mstari wa kesi (mambo ya April wakati anakamatwa) siyo (mambo ya Oktoba akiwa gerezani). Baada ya Mahakama Kuu kusema Notice of Additional Witnesses (ushahidi wa nyongeza) chini ya kifungu cha 308 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (Criminal Procedure Act - CPA) iliyoletwa na upande wa Jamhuri ni incompetent (haina sifa wala uwezo wa kusimama mbele ya sheria) na kwamba kifungu cha 308 CPA hakiruhusu upande wa mashitaka “kuboresha” ushahidi wao katikati ya kesi kwa kutumia shahidi yuleyule. Baada ya notisi yao kufutwa (struck out), upande wa Jamhuri ukatakiwa kuleta shahidi kesi iendelee, wakasema shahidi wao hawajamuandaa. Hapa ndipo Tundu Lissu alipowaka kama mbogo na kupinga hairisho na kutaka Jamhuri walete shahidi kesi iendelee. Upande wa Jamhuri wamechanganyikiwa na wameomba muda wa “kutafakari.”. Mahakama ikawapa muda wa dakika 40, watafakari. Tunasubiri. TAL anajua kuwa Serikali haina mashahidi wengine waliojipanga vizuri kwa sasa nje ya ule ushahidi wao wa “matukio ya Oktoba 29” ambao umekataliwa Mahakamani. TAL anasisitiza kesi iendelee. TAL anawaweka upande wa Jamhuri katika shinikizo (pressure) la kuleta ushahidi uleule wa mwanzo uliodhoofika. Hawana ushahidi na shahidi wa msingi.