Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda amemteua Diwani wa Kata ya Kariakoo, Haji Manara kuwa msemaji wa timu zote za Taifa za Tanzania.
Makonda ametangaza uteuzi huo akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 28, 2026 katika Viwanja vya Bunge Dodoma, ambapo amesema Manara atafanya kazi chini ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT).
Pia Amesema Manara atakuwa na jukumu la kuzisemea timu zote za Taifa za mpira wa miguu na kuimarisha mawasiliano kati ya mashabiki na uongozi wa michezo nchini.
#mwananchiupdates
#tunaliwezeshataifa