Issue kubwa ni namba tatu. Uegeshaji usiosahihi. Hii inaanzia kwenye magari yanayoharibika, daladala na sasa hivi gonjwa kuu ni Bajaj. Yani unakuta Bajaj imewasha hazard imesimama. Inaweka foleni kubwa tu.
Jambo lingine ulilosahau ni vivuko vya waenda kwa miguu. Hili ni janga kubwa la foleni. Mfano mkubwa Morogoro road yote. Mfano mwingine mkubwa ni pale riverside.
@EduTalkTz Hapo umepigia hesabu faida ya passenger train tu. Passenger train huwa ni ya huduma na sio profit. Reli yoyote duniani faida ni goods train.
Nikuelekeze tena kaka. Tandem au multiple units inatokea pale mzigo unapokua mzito na hakuna locomotive yenye uwezo wa kuvuta peke yake. Kwa hiyo zinafungwa engine mbili za class sawa au hata tatu ili kuongeza nguvu ya kuweza kuvuta mzigo. Na kuna muda treni inaweza kufunga loco moja lakini kwenye mlima inaongezwa engine yenye nguvu (Banker loco) ili ku assist main loco. Swali ambalo ulipaswa kujiuliza hiyo engine ina uwezo gani? Then fananisha na engine zetu.
Kaka mkubwa. Nikuelimishe jambo la msingi kwenye reli. Issue sio container issue ni uzito wa mzigo na aina ya reli. Hizo aina za reli zinasaidia/kutofautiana aina ya mzigo zinazobe. Kuna meter gauge, standard gauge narrow gauge na nyinginezo. Kuvuta makontena mengi reli yoyote inavuta isipokua tu je hiyo reli sehemu za kupishana au marshalling yard ina track ndefu za accommodate hiyo treni?
Kwa hiyo tumeona hapo issue ni urefu wa njia za kupishana na stesheni pia. Iila kuhusu wingi wa mabehewa hata reli yetu mpya ya SGR inaweza vuta hata behewa mia mbili sema tu kuwe na njia ya kupishana inayoruhusu hali hiyo
@pius_thoma95606 Sababu ni madaraja. Kuna daraja la hale, na pale Ruvu (Juu reli) kwa hiyo kwa urefu huo haliwezi kupita. Ndio maana wakachagua njia ya Mtwara-Ruvuma-Njombe-Iringa Dodoma Via Mtera. Hakuna madara yenye height restrictions.
@Ramatech255 Kama Battery saver ipo on kwenye Android au Low power mode ipo on kwenye Iphone haiwezi kwenda kwenye 5G instead itaishia kwenye Longe Term Evolution mode. Ili ku save battery. Kama ujuavyo 5G inanyonya sana battery.
@Wizdomtz Kukiwa na double line zilizo straight ndio hauruhusiwa ku overtake. Lakini kwa sheria zetu za Tz hata line moja uki overtake jamaa wanakuchapa 30k ya offense.
Umeandika vizuri sana. Hata mwenye F zote anaelewa.
Kwa kuongezea tu. Wazazi wetu asilimia kubwa wameolewa below 18 enzi hizo. Wakimaliza la saba tu hao ndoa! Manake wengi walikua wameshabalehe. Na ukifuatilia zaidi hutosikia wanawake wa zamani wame cheat sababu waliolewa wakiwa wapya na wanamjua mwanaume mmoja tu (ambae kamuoa).
Sasa miaka hii mdada/mkaka mpaka amalize chuo ana 25 years huko. Ashakutana na experience ya kutosha. Ndio maana ndoa na mahusiano yanakua magumu.
Bwana Satoshi. Inabidi uelewe kwanza kwa nini zinaitwa Hazard lights! Je unavyowasha kwenye intersection unaonyesha kuna Hazard gani? Jibu ni moja tu. Hauruhusiwi kuwasha Hazard lights.
Ndio maana kwenye intersection kuna barabara inayopewa kipaumbele. Nyingine inabidi usimame kwanza kabla ya kupita
@MiriamMkanaka Akienda Six na akapata Zero inakuaje? Akienda chuo (Diploma/Certificate) kama akiwa serious anatoka na ujuzi na anaweza akapata ajira then akaja kujiendeleza. Lakini form six anatoka na cheti tu.
Hakuna maswali mapya kwenye mitihani yetu. Maswali yote ni ya miakaya nyuma.
Kama ukiweza kumpa mwanao/mwanafunzi maswali kufanya mara kwa mara akiingia kwenye mtihani lazima abutue.
Swali la msingi je mitihani yetu inawaandaa wanafunzi kwenye soko la ajira? Na maisha kwa ujumla? Ukitaka kujua hilo kaa na mwanafunzi aliepata division one ndani ya miaka kumi hii uone uelewa wake na uwezo wa kujenga hoja. Wengi wao hawana uwezo huo.
In a nutshell wanafaulu mitihani lakini sio elimu/ujuzi/uelewa.
@GodemaE Maana ya XT. Ni hiyo Scania imekua designed kwa kazi ngumu, kama vile minings au kwenye tough roads.
Inakua na bumper ngumu, side mirrors zinakua na material magumu, ground clearance inakua kubwa ili kuhimili barabara mbaya na cabin yake inakua designed na latest tech