“Waheshimiwa Majaji, kwa bahati mbaya sana, mmefanya kile ambacho Mahakama Kuu ya Kenya ilifanya mwaka 1954 katika kesi ya Mzee Jomo Kenyatta. Walimuadhibu kwa sababu ya kuwa mpinzani wa wakoloni. Historia haijawahi kuwaacha salama wale Majaji walioamua kutumika kisiasa. Kwa sababu nyinyi wenyewe mnajua kwamba sina hatia, mnamuadhibu mtu asiye na hatia. Hivyo, nataka niseme jambo moja: Watu wasio na hatia hawaombi msamaha. Wanaoomba msamaha ni wale waliokosa. Huombi msamaha unapokuwa huna hatia. Waheshimiwa Majaji, kwa hiyo, naomba iwekwe wazi katika kumbukumbu rasmi za Mahakama kwamba SIJAOMBA MSAMAHA. Mimi nipo hapa, na Mahakama imekubali kunitia hatiani licha ya kutokuwa na hatia, kutokana na shinikizo na maelekezo ya kisiasa. Mahakama inatumika kisiasa. Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, nataka niwe wazi kabisa kwamba maneno nitakayoyasema yasichukuliwe, kwa namna yoyote ile, kuwa ni ombi la msamaha. Siombi msamaha. Siombi msamaha kwa sababu sina hatia kabisa (I am completely innocent).”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Kwa kuwa Wakili wa Serikali amezungumza hayo, naomba nijibu hoja zake sasa. Wakili wa Serikali amezungumzia Kifungu cha 35, ambapo ameomba Mahakama itoe adhabu kali. Amesema kuwa adhabu ya juu ni kifungo cha miaka mitano, faini au vyote viwili kwa pamoja. Sasa, Waheshimiwa Majaji, sheria inapoweka adhabu ya aina hiyo, yaani kifungo au faini au vyote viwili kwa pamoja, Mahakama inatakiwa kufanya nini? Wakili wa Serikali amesema hana uhakika kama nimewahi kukutwa na hatia. Sasa, nawaambieni wazi kwamba sijawahi kutiwa hatiani katika maisha yangu yote. Kwa hiyo, mnapofikiria adhabu ya kutoa kwa lile mnaloliita kosa, msisahau kwamba mtakuwa mnatoa adhabu kwa mtu ambaye hajawahi kupatikana na hatia katika maisha yake yote. Waheshimiwa Majaji, nina tumaini kwamba mnafahamu kuwa nina msiba mkubwa sana. Nimempoteza mtu ambaye amenifanya kuwa nilivyo leo; mtu aliyenifanya kuwa Mwanasheria na ambaye amenilea. Kwa sababu sikuweza kumuuguza, nilikuwa na matumaini kwamba, kwa kuwa Mahakama ingeona ukweli kwamba sijafanya kosa, ningepata nafasi ya kwenda kumzika Mzee Alute. Lakini, inaonekana, Waheshimiwa Majaji, kwamba jambo hilo halipo katika fikra zenu. Mtu huyu amefariki, na habari za msiba wake zimeandikwa katika magazeti kila mahali. Nilikuwa na matumaini ya kupata nafasi ya kutimiza wajibu wangu wa kifamilia, yaani kwenda kumzika mtu huyu aliyenilea. Katika shauri hilo, Waheshimiwa Majaji, Bunge lilisema kwamba pale ambapo sheria inaweka adhabu mbadala tatu, yaani kifungo, faini au vyote viwili, Mahakama lazima ianze kwa kutoa adhabu ya faini. Kwa hiyo, mnapotafakari ombi la Wakili wa Serikali la kutoa adhabu kali, msisahau kwamba sheria inawaelekeza kuanza na adhabu ya faini.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Sasa, Waheshimiwa Majaji, kuna maneno ambayo yamesemwa hapa na Wakili Mkuu wa Serikali, ambapo amejigeuza kuwa shahidi badala ya kubaki kuwa Wakili wa Serikali. Amesema kwamba matukio ya vurugu za Oktoba yalitokana na kauli zangu, kama nimemwelewa vizuri. Waheshimiwa Majaji, sina uhakika kama katika kesi hii mmeletewa ushahidi wa hotuba ya Jaji Mkuu, Othman Chande. Hotuba hiyo haipo katika ushahidi wa kesi hii. Jaji Mkuu Othman Chande hajaja hapa kutoa ushahidi kuthibitisha kwamba kauli hizo zilitolewa na wanasiasa gani. Mnaombwa kutoa adhabu kwa kosa, kama kweli lipo, ambalo inadaiwa lilitokea miezi sita baada ya mimi kuwa tayari nimewekwa mahabusu. Mkikubaliana na mwaliko huo, Waheshimiwa Majaji, itakuwa ni uthibitisho kwamba huu ni uamuzi wa maelekezo. Kesi nyingi kuhusu matukio mbalimbali ya uchochezi yamezungumziwa hapa. Lakini matukio hayo ni mangapi? Yametokea wapi? Na nani ameyafanya? Wakili Mkuu wa Serikali anataka muamini porojo za mitandaoni. Mkizikubali, Waheshimiwa Majaji, itakuwa ni uthibitisho mwingine kwamba huu ni uamuzi wa maagizo.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Waheshimiwa Majaji, naomba nimalizie. Uamuzi wa kunitia hatiani kwa kosa ambalo sikushitakiwa nalo, na ambalo sikupata fursa ya kujitetea dhidi yake, kwa lengo la kubalansisha tu, una athari kubwa. Athari yake ni kwamba mmewapa kinga wale waliohusika na mauaji, kwa sababu watasema kwamba wale waliochochea wamekutwa na hatia. You are covering mass murderers. Serikali hii imeua watu wengi kuliko serikali zote zilizowahi kutawala nchi hii. Mara ya mwisho mauaji ya halaiki kutokea kwa kiwango hiki ilikuwa wakati wa Vita vya Majimaji. Mmewapa sababu ya kusema kwamba mkosaji aliyesababisha mauaji hayo amekutwa na hatia. Kama mnafikiria kwamba uamuzi huu utawasaidia, hautawasaidia. Watawajibishwa mahali pengine. Serikali ya Nyerere iliua watu 37. Wakati huo, Mwinyi alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na alijiuzulu. Shahidi alikuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na alijiuzulu. Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Peter, naye alijiuzulu. Leo hii, serikali imeua watu ambao idadi yao, kwa makadirio ya chini kabisa, ni 500, lakini hakuna aliyejiuzulu. Uamuzi wenu hautaficha ukweli huo. Nimewakumbusha, Waheshimiwa Majaji, kwamba katika Sentencing Guidelines, kipengele cha kwanza kinaelekeza kwamba adhabu ya faini itolewe isipokuwa pale ambapo kosa ni kubwa. Uchochezi, ambao sikushitakiwa nao, hauna adhabu maalumu. Ndiyo maana Wakili Mkuu wa Serikali anakwenda kwenye General Provisions. Waheshimiwa Majaji, namalizia kwa kusema: TOENI HUKUMU AMBAYO MNAYO, AMBAYO MMEAGIZWA KUITOA.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, 6 Novemba 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania, katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
“Tumezingatia hoja za pande zote mbili; upande wa Mashitaka, ulioomba adhabu kali, na upande wa Mshtakiwa. Tuanze na suala la dhamana. Ombi la dhamana utalifanya wakati wake utakapofika. Mahakama imezingatia kwamba wewe ni mkosaji wa mara ya kwanza. Tumezingatia pia hoja zilizotolewa kuhusu adhabu ya faini, kifungo au vyote viwili. Nakubaliana na pande zote mbili kwamba Kifungu cha 390 hakijaainisha adhabu. Kifungu cha 35 kinatumika pale ambapo sheria haijaelekeza adhabu mahsusi. Kifungu hicho kinaelekeza kifungo kisichozidi miaka mitano, faini au adhabu zote mbili. Kifungu hicho hakijaainisha kiwango cha faini kinachopaswa kutolewa. Hata hivyo, tunafahamu kwamba pale ambapo adhabu ya kifungo na faini zinapoweza kutolewa, faini ndiyo chaguo la kwanza, lakini Mahakama inaweza kuzingatia sababu nyingine katika kuamua aina ya adhabu. Kuhusu hoja nyingine tulizozieleza, ikiwemo suala la kuzuia uchaguzi, kufanya hivyo ni kukiuka Katiba ya nchi. Ukiisoma Ibara ya 30(1), inaeleza kwamba unapotekeleza haki zako, unapaswa kuhakikisha kuwa huingilii haki za watu wengine. Kwa mazingira hayo, Mahakama inaona kwamba kuhamasisha vurugu za uchaguzi ni kuzuia haki za watu wengine. Kwa hiyo, Mahakama inaona kwamba adhabu ya kifungo inafaa zaidi kuliko faini. Mahakama inakuhukumu kifungo cha miaka minne badala ya miaka mitano.”
Jaji Dunstan Ndunguru, Mahakama Kuu ya Tanzania, 06 November 2026 akisoma hukumu ya kesi ya uhaini ya Tundu Lissu ambayo imegeuzwa kuwa uchochezi.
Leo ni BLACK FRIDAY.
Mahakama Kuu inapotoa uamuzi kuhusu tafsiri ya sheria, uamuzi huo unaweza kuwa na athari kwa kesi zijazo, hasa katika Mahakama za chini.
Uamuzi wa leo uliotolewa na Mahakama Kuu una hatari ya kuwa judicial precedent itakayotumiwa na Mahakama za chini katika kuamua kesi zijazo,
Uamuzi huo utaathiri kwa upana zaidi haki ya washtakiwa wanaoshindwa kutiwa hatiani kwa makosa makubwa waliyoshtakiwa nayo.
Kwamba sasa imewezekana mtuhumiwa kufikishwa mahakamani kwa kosa kubwa, akanyimwa dhamana na kukaa mahabusu kwa takribani siku 577
Wakati mtuhumiwa akisubiri haki yake atakuwa akitokea gerezani kwenda mahakamani. Kwamba, mtuhumiwa atapoteza uhuru wake wakati wote.
Upande wa Jamhuri ukishindwa kuthibitisha kosa aliloshtakiwa nalo, Mahakama inachukua ushahidi huo huo na kutengeneza kosa jingine dogo,
Halafu Mahakama inatoa hukumu ya kifungo gerezani bila fursa ya kulipa faini. Hakimu atafanya rejea ya kesi ya Jamhuri Vs. Tundu A.M Lissu.
Unafungwa gerezani kwa kosa ambalo hujashtakiwa na hujawahi kusikilizwa popote. Unabadilishiwa kosa lako ukiwa kizimbani na unahukumiwa kifungo.
Hii ni siku mbaya sana kwa utawala wa sheria, haki ya kusikilizwa na misingi ya utoaji haki. Kama unaona haikuhusu, itawagusu ndugu, jamaa na rafiki zako
“Waheshimiwa Majaji nashukuru kwa fursa ya kuzungumza. Naomba mnisikilize kwa makini kama ambavyo mmenisikiliza kwa makini mwaka mzima. Naomba pia m’rekodi proceedings kama mlivyo’rekodi vizuri mwaka mzima na nusu. Leo Waheshimiwa majaji ni siku ya 577 nikiwa gerezani kwa kosa la uhaini. Ndiyo kosa kubwa Kuliko yote katika Jamhuri ya Muungano. Ndiyo kosa pekee lililotamkwa katika katiba, kosa la uhaini. Kwa siku 577 nimeitwa mhaini. Kosa ambalo kwa mujibu wa kifungu cha 39(2)(d) ambapo adhabu yake inaeeza kuwa ni KIFO. Baada ya siku 577 baaada ya wingu jeusi la adhabu ya kifo kuning’inia juu ya kichwa changu. Leo Waheshimiwa Majaji mmeniita MCHOCHEZI. Kosa ambalo wala halijapangiwa adhabu. Unaona hapa, wakili mkuu wa serikali anahangaika kutafuta hii adhabu yake ni nini., anasema nipewe adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine, nihukumiwe kifungo cha miaka mitano gerezani. Hii maana yake ni nini Waheshimiwa Majaji? Waheshimiwa majaji mmesema wenyewe hakukuwa kosa. Kwa hiyo nimekaa gerezani siku 577 bila kosa lolote. Kuna kitu kimoja hamjakisema nitakisema kwa ajili ya kumbukumbu za Mahakama. Ushahidi wangu umethibitisha kwamba hii ilikuwa kesi ya kisiasa. Kugeuza Mahakama kuwa uwanja wa mapambano ya kisiasa, it’s an obvious political persecution. Kwa sababu ni political persecution inabidi vi’sababu vitangenezwe vya kumfunga huyu mgomvi wetu. Vi’sababu vya kumfunga huyu mpinzani wetu. Hili kosa la UCHOCHEZI ni kisa ambalo ninyi Waheshimiwa Majaji mmelitengeneza. Mimi nilishitakiwa kwa UHAINI na kusambaza taarifa za uongo. Mmetafuta kosa ambalo halikuwepo, mmenipa. With all due respect mmefanya hivyo kwa sababu za kisiasa na kwa maelekezo ya kisiasa tu. Ni kama mmeambiwa, huyu mtu hana kosa lakini tafuteni kosa lingine dogo, isije ikaonekana serikali imepata aibu. Mimi ninajua mtani’hukumu. Na mnaonekana tayari mnayo hukumu, l feel it in my heart.”
Tundu Antiphas Mughwai Lissu, O6 November 2026, Mahakama Kuu ya Tanzania katika hukumu ya kesi yake ya uhaini.
Mnaua watu kwa maelfu, Mnateka watu na kuwapoteza. Mnaiba uchaguzi kwa nguvu..
Alafu mnasema kuna watu wanawaonea wivu kwasababu ya rasimali!!!!
Hivi mnawaona Watanzania ni wajinga?
Kwamba Mataifa ya nje ndio yaliwatuma kuiba uchaguzi ambao hamjashinda!!!!
Watu sio sisimizi mmeua lazima muwajibike.
Mwenyekiti Tundu Lissu.
Wewe ni mtu mwema sana, Mzalendo unaeipenda Nchi yetu na watu wake kuliko hata unavyojipenda mwenyewe.
Umetoa maisha yako na umepitia matatizo na maumivu makubwa sana kwaajili ya watu wa Nchi hii.
Umedai maisha bora, ajira, maji, umeme maendeleo na matibabu bora kwa Watanzania wote.
Umedai rasilimali nyingi za Nchi hii zitumike kwaajili ya manufaa ya Watanzania wote ambao wanateswa na umasikini mkubwa wa makusudi, unaosababishwa na ccm.
Kwasababu hiyo serikali hiii ya CCM chini ya utawala huu huu walijaribu kukuua wakakupiga risasi 36 Mungu mkuu akakuokoa.
Leo watu hao hao waliojaribu kukuua wakashindwa wanataka kukufunga kwa uongo na kesi ya kubumba.
Wanaweza kufanya hivyo kwasababu mahakama ni zao na wanaweza kuzielekeza nini cha kufanya.
Kitu ambacho hawatafanikiwa ni kushinda kwa kutumia uovu na mauaji yao, kwa hakika hilo watalipia wao na familia zao.
Naomba Watanzania wote tumuombee Mwenyekiti
Tuombee Chama chetu
Tuombee Nchi yetu na demokrasia tunayoipigania.
Tutashinda.
. @godbless_lema msikilize Lissu kwa makini.
‘ikiwa hali itakuwa mbaya, mapambano yataendelea”
Huu ndio msimamo wa Tundu Lissu, mwanaume mwenye balls.
Sasa hizo “strategic engagements” zako zikome mara moja. Lissu hataki kutoka kwa njia haram unazofanya wewe na watesi wetu. Anataka kutoka kwa kutumia utawala wa sheria ili aweze kuwa mpinzani wa kweli.
Lissu hataki kurudia kosa la Mbowe, kutoka jela kwa “huruma” za watesi wake.
Kila Mtanzania anaelewa kuwa mtu unapokubali uhuru wako uwe chini ya mwenyekiti wa CCM, kwamba yeye ndo anaweza kukufunga na kukuachia huru, huwezi kuwa mpinzani wake bali utakuwa puppet wake huku unajifanya mpinzani. Mfano huu tuliona kwa Mbowe, alikaza siku zote mpaka siku alipokubali kutoka jela kwa maelewano na Samia Suluhu na sio kutoka kwa utawala wa sheria. HILI KOSA HALITAKIWI KURUDIWA EVER AGAIN!!!!!!
Lissu kaamua kukaza mpaka haki itakapopatikana, sasa nyie wanasiasa wa hovyo mnaojifanya mnampenda Lissu kuliko wananchi ambao Lissu anawapigania tulizeni makalio yenu yaliofika bei za kina Abdul. Lissu hataki short cut na Watanzania hatutaki short cut.
TUNATAKA UTAWALA WA SHERIA NA HAKI na sio mambo ya kupigia simu na kuwapiga magoti watesi wetu……
Huu ndio msimamo wa CHADEMA tunaoufahamu na kuuunga mkono kwa nguvu zote.
Ni msimamo kama ule wa NO REFORMS NO ELECTION ambao baadae wale “wanasiasa malaya malaya” walianza kuuyumbisha na kutuambia “mkuu hakumaanisha hivyo.”
Kama kuna chochote kimebadilika mtuambie. Vinginevyo tutaendelea kuutumia kama benchmark.
Viva💪💪💪💪!
Kama hoja ya kujipendekeza kwa watawala msingi wake ni “hofu ya kuendelea kufungwa, kutekwa, na hata kuuawa,” kwa nini mshishauriane kunyamazia matendo dhalimu ya serikali??
Kwa sababu serikali inapambana na wanaoikosoa, kuanzia watu wake wenyewe kama wakina Nchimbi, Ndugai, na Polepole, mpaka wa nje kama wakina Lissu, Soka, Mdude, na wengineo.
Sasa kama hoja ya msingi ni hii hofu, njia ya mkato ni kunyamaza kimya.
Unless unaenda kuihakikishia serikali kuwa “tutafunga mdomo mkimwachia Tundu Lissu,” kilichoongelewa hapa hakimake sense hata kidogo.
In fact, ni kinyume kabisa na ajenda ya NO REFORM NO ELECTION, matakwa ya katiba mpya, na mengine yote.
Haingii akilini hata kidogo kwamba unayasema yote haya halafu bado unabaki na msimamo wa NO REFORMS NO ELECTION.
“It's better to keep your mouth shut and appear stupid than open it and remove all doubt.” — Mark Twain
Mwanzo watu walikuwa na doubt nae ila leo ka prove yote yaliyokuwa yanasemwa ni kweli…….
Dah yani kajimaliza mwenyewe………..
Ndio naamka……
Kati ya moja ya vitu alivyoongea Lema leo ambavyo vimemuanika ni hii sentensi pia.
Imagine anasema “ watu wanakufa” na sio wanauawa.
Pili ananilaumu mimi kwa October 29 na hamlaumu alietoa order wananchi wauliwe na waliotelekeza order. Hamlaumu kimama na polisi. Instead anasema wananchi wanapende polisi…..
Rest in Peace baba, ulitubu kabla ya kifo chako. Ulihakikisha unaawacha Watanzania na ukweli kabla hujaenda.
Imagine ungekufa kabla ya ile interview kina Mange milele tungeishi watu waki tu doubt ila you cleared it kwa ushujaaa na ujasiri.
Uligoma kukutana na Mungu wako kabla hujaongea ukweli juu ya serikali hii inayofosi “mhaini” aombe msamaha. Kumbe kesi ni ya kuomba msamaha tu. Sasa hiyo mahakama si inafanya uhuni tuu maana wamiliki wa mahakama wanataka kupigiwa magoti tu.