Kitabu kipya HAKI YA DHALIMU kimeingia rasmi sokoni. Ni riwaya ya kijasusi, mapenzi, usaliti na wivu.
Bei ni TZS 10,000
Dar es Salaam kinapatikana;
Duka la Kona ya Riwaya, Kinondoni Block 41 - 0655 428 085.
Kwa Hellen - Kariakoo - 0653 254 110.
UZIπ
MAGOGONI HAS FALLEN
Mtihani wangu wa kwanza baada ya kuwa nimerejea masomoni kutoka nchini Israel, ilikuwa ni wimbi la matukio ya uporaji magari, uvamizi wa vituo vya polisi na kuporwa silaha
Lakini yote tisa, kumi ilikuwa ni mauaji yaliyokuwa yanatingisha katika mae- neo ya Mkuranga, Kibiti na Rufiji.
Nasema ulikuwa ni mtihani mkubwa kwa sababu ndani ya muda mfupi niliofanya kazi, nilitokea kuaminiwa na viongozi wangu wa ngazi za juu kabisa na kila tatizo lililokuwa linatokea, mimi ndiye niliyekuwa nafikiriwa haraka kwamba naweza kuwa na mbinu za kujua nini cha kufanya.
Sina haja ya kujitambulisha sana, wengi tayari mnanijua.
Wengi walikuwa wanapenda kuniita Chief.
Hatua ya kwanza ilikuwa ni kujaribu kuyatazama matatizo yote matatu na kujua ni kwa namna gani yalikuwa na uhusiano.
Namaanisha ujambazi wa kupora magari, matukio ya kuvamia vituo vya polisi na mauaji ya watu yaliyojawa na utata mkubwa yaliyokuwa yakiendelea Kibiti, Mkuranga na Rufiji.
Waliokuwa wananiamini hawakuwa wanakosea.
Mafunzo niliyoyapata awali kitengo na yale niliyoenda kuyapata nchini Israel, yalinifanya kuwa na uwezo mkubwa sana wa kugundua jambo ambalo kwa akili ya kawaida, ingewachukua wengine muda mrefu sana kupata picha.
Matukio haya matatu yaliyokuwa yakitokea kwa kasi, kwangu yalikuwa ni ishara kwamba kuna jambo linaloenda kutokea lakini ilikuwa kazi ngumu sana kuwaaminisha wenzangu kwamba matukio haya yalikuwa na uhusiano.
Ilikuwa ni lazima kwanza nipate ushahidi wa kutosha, niwe na taarifa za kutosha kisha ndipo niwasilishe kwa viongozi wangu wa juu ili kwa pamoja, tujue nini cha kufanya kumaliza kabisa matukio yote.
Kwa hiyo, nilichokifanya kwanza ilikuwa ni kuwa macho kuyatazama matukio yote, kujua nani na nani wanahusika na uhusika wao umekaaje.
Ni hapa ndipo nilipoamua kwanza kuanza kulifuatilia tatizo la uporaji wa magari lililokuwa limeshamiri.
Niliamua kuanzia huku kwanza kwa sababu kuna jambo nilikuwa nimelihisi.
Ndani ya muda mfupi tu, tayari nilikuwa nimeshapata picha kamili kuhusu nini hasa kilichokuwa kinaendelea kwenye ujambazi wa magari.
Nilibaini kwamba kulikuwa na makundi mawili, kundi la kwanza lilikuwa ni wahalifu wa kawaida lakini kundi
la pili lilikuwa ni watu ambao huwezi kusema ni wahalifu wa kawaida.
Nitafafanua ni kwa nini nasema hivi na mbinu iliyofanya niujue ukweli huo ambao wengine hawakuwa wakiujua.
Ilikuwa ni kuwatumia wahusika wenyewe kuwa βmachoβ yangu.
Kama ambavyo mimi niliweza kugeuzwa kutoka upande mmoja
hadi kwenda upande mwingine, mimi pia nilikuwa naamini zaidi katika falsafa hii kwamba unapowakamata kwa mfano majambazi, badala ya kuwapiga risasi au kuwapeleka jela wakaenda kuozea huko, unaweza kuwachukua wachache kati yao ambao wanaweza kuwa msaada mkubwa kwako kwa kukuonyesha ni kwa namna gani huwa wanafanya uhalifu huo na huwa wanashirikiana na nani.
Nilijifunza kwa undani kuhusu mbinu hii nilipokuwa nchini Israel na hata niliporudi nchini, niliamua kuwa nitakuwa naitumia hiyo zaidi kuliko ile iliyokuwa imezoeleka ya βkuwanyangβanyaβ silaha majambazi kwa kutumia nguvu.
Ninaposema kuwanyangβanya bila shaka utakuwa unanielewa vizuri kwamba mtu akiwa na bunduki, ni kwa namna gani unavyoweza kumnyangβanya kabla hajakudhuru.
Sikuwa naikubali kabisa falsafa hii na niliamua kuja kuonesha tofauti ili hata siku nikisimama mahali na kuwaelekeza wenzangu, kuwe na ushahidi wa kutosha wa namna nilivyofanikiwa katika njia tofauti.
Basi katika oparesheni ya kupambana na wezi wa magari, kama nilivyosema nilibaini kwamba kulikuwa na makundi mawili, wezi wa magari wa kawaida lakini na kundi jingine lisilo la kawaida.
Nilitumia mbinu shirikishi kwa kuwatumia baadhi ya wahusika ambao walikamatwa katika oparesheni hiyo ambao walikuja kugeuka na kuwa msaada mkubwa sana kwangu.
Hili pia nitakuja kulieleza.
Sasa hili kundi la pili, lenyewe lilikuwa na namna ya tofauti kabisa ya kufanya uhalifu wao.
Kwanza, matukio ya uporaji wao wa magari, yalikuwa yakihusisha mauaji.
Orodha ya usajili mpya 2023/24 imefika katika kitengo cha habari na mawasiliano.
Pakua Simba App, lipia alafu subiri sajili za moto kuja kuimarisha kikosi cha Mnyama π¦ #NguvuMoja