#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 35
Anaendelea Mhe. Lissu
Hizo nyaraka baada kusomewa kule chini vyote kwa pamoja vinaletwa huku.
Sasa ukileta kimojawapo bila kingine ujue hapo hakuna kesi yani ulete information bila witness statement. Kwamba taarifa inaweza kusimama peke yake.
Naomba hili Waheshimiwa majaji mumuachie Katuga abaki nalo yeye na kikundi cha wenzake hapo maana hakuna information without witness statement. They go together.
Sasa mmeambiwa hivi walijiandikia au waliandika hayo ni maswala ya ushahidi.
Sasa hilo sio suala la ushahidi maana it is on the face of records, nyaraka mnazo hapo na mnaona mkiangalia.
Sasa anasema wakija watasema wameandika kwa mamlaka gani?
Hatuhitaji kuwasubiri waje waseme walishaandika tayari na mamlaka hayo wameshayasema sasa S. 10(3) ya CPA inaruhusu wajiandikie wenyewe maelezo?
Hilo ndio swali sasa.
Sheria imesema nani anayepaswa kuandika maelezo ya mashahidi ni police officer anayechunguza yeye ndio anawakanya, anawaonya, anasign na kumuandika mashahidi.
Hili limefanywa na mapolisi wengine kwenye kesi hii hii hawajaandika wenyewe. Wameandikiwa na mapolisi wengine kama sheria inavyotaka.
Kwanini kuwe na mapolisi waliojiandika na wawepo walio andikiwa? Unaelewa nini hapo.
Kwanini vyote viwe sahihi? Wasituchezee akili hapa wajifunze sheria.
Hakuna mtu anayeweza kujionya mwenyewe na kujiapisha mwenyewe.
Haya yote yapo on face of records. Tusipeleke kesi mbele wakati haipo wako polisi wanne wamepatia utaratibu.
Shida ya mapolisi huwa hawasomi sheria eti wameandika kwa mujibu wa kifungu cha 10(3) ambacho kinasema wanapaswa kuandikiwa maelezo na sio kujiandika wenyewe.
Lipo lile lingine la hawa Mawakili wa serikali waliomba mashahidi wao wasijulikane wafichwe na jaji akawapa alichowaomba. Kusiwepo na anuani, majina, kazi zao, makazi yao, majina ya ndugu zao na hakikisheni mnawapa majina bandia na mfute hayo ambayo hayatakiwi.
Wakaondoka na hiyo amri wakafuta futa majina mengine wakaacha,
Amesimama Katuga anasema Mheshimiwa ameanza tena kwenda mbali huko hatukufika. Naombeni mwongozo sisi tulielewa hivyo. Mtoe guidance.
Jaji: Lissu unasemaje?
Lissu: hicho anachopinga sio sahihi na amesema haya mambo hata yeye leo hapa.
Majaji wanateta kidogo hapa.
Wanasema tuendelee hebu achanana na Katuga.😂
Sasa kwenye ile kesi ya Felius Mulokozi kesi ya armed robbery aliyenyooshewa silaha hakutajwa. Mahakama ya rufani ikasema hilo shitaka na hati yake ni batili.
Isdory Patrice kesi ya attempted rape waendesha mashitaka kwenye hati ya mashitaka hawakuweka neno attempted mahakama ya rufani ikasema hilo sio shitaka ikafuta.
Waheshimiwa Majaji kwenye kesi ya Uhaini usipotaja kulikuwa na nia ya kutenda kosa la uhaini na ukasema kulikuwa na nia ya watu kuzuia uchaguzi mkuu.
Hiyo hati ya mashitaka inasalimika vipi?
Kama kutokutaja nani aliyenyooshewa silaha imefuta kesi ya armed robbery na kutotaja neno attempted kesi ilifutwa. Huku kutokutaja kabisa kosa la uhaini kunabakije?
Kwa maoni yangu kosa hili ni kubwa zaidi kuliko kutokuandika attempted au kutokusema nani alinyooshewa silaha.
Hili la uhaini mambo yanabaki vipi yalivyo kwa maoni yangu hati ya mashitaka haibaki kabisa na kama nilivyosema.
Haiwezi kubaki hii hati ya mashitaka.
Naomba waheshimiwa majaji wala msiicheleweshe kabisa, ifutilieni mbali huko.
Wakili wa Serikali Mkuu amesema pia kuhusiana na Grey Likungu Mataka na Khatibu Gandi kwamba yale yote niliyosema kuhusu namna ya kuandika charge sheet au information hayakuamuliwa kwenye objection yaliamuliwa kwenye hukumu ya kesi kwahiyo na hii twende tutaamua mbele kwa mbele.
Waheshimiwa Majaji ni kweli hayo yaliamuliwa kwenye Judgement yaani yalisemwa kwenye trial kwasababu mawakili wa mashitaka hawakukosea waliandika hati zao sawasawa.
Hivyo ndio maana yaliibuka huko mbele. Kwenye hii kesi yangu wao wamekosea kuandika hii information yao.
Part 36 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 33
Anaendelea Mh. Lissu.
Watu wanafurahi kumsikiliza.
Mawakili wa serikali wamesema hati ya mashitaka kuhusu publication na kifungu cha 39(2) cha Penal Code.
Publication maana yake maneno yaliyochapishwa kwenye karatasi yaani writing au printing.
Nilimsikia anasema nilichapisha na nikaweka kwenye mitandao ya kijamii.
Angalieni kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha kwenye mitandao ya Kijamii.
Sasa angalieni hayo maneno kama yapo kwenye hati ya mashitaka kuwa nilichapisha hayo maneno kwenye mitandao ya kijamii.
Kama yapo niambieni ili nikae chini kama maneno hayo hayapo hawawezi kuja kusema wakati wa ushahidi.
Hivyo basi publication by writing or printing haipo kokote sasa Waheshimiwa Majaji kuna kitu nimesikia kwa mara ya kwanza katika maisha yangu.
Kwamba maneno ni matendo. The deed of uttering words. Waheshimiwa majaji maneno sio matendo ieleweke vizuri.
Huyu Katuga ni mtu mwema sana alituletea maana ya deed kutoka Black's law dictionary anaisoma hapa.
Deed sio maneno, something that is done or carried out na sio kusema, kuongea. Hiyo ndio Deed.
😂😂😂😂Katuga alisoma maana ya Deed kwenye blacks law dictionary hakuelewa.
Anaendelea Lissu.
Kwa mara ya kwanza nimesikia kwa Katuga kuwa maneno ni matendo hiyo tafsiri tumuachie Katuga akae nayo mwenyewe ni yake.
Amegundua hili yeye.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisemaje juu ya maneno na uhaini, nafikiri hata hili Katuga hajalielewa na halifahamu kabisa.
Tutaelekezana pia katika hili.
Mahakama ya rufani ya Tanzania ilisema hivi ...... Kwenye uhaini maneno ni nini?
Ukurasa wa 55 mere words do not amount to overt act on a treason charge na ikasema maneno matupu haitengenezi kosa la uhaini isipokuwa hayo maneno yanaelezea kitendo cha uhaini.
Maana yake ni kwamba wanaopanga uhaini wanakaa vikao na kupeana maelekezo hapo utasema maneno hayo ni vitendo vya uhaini eti kuhamasisha wananchi kuzuia uchaguzi. Hii ni kesi ya Khatibu Gandi.
Sasa kama Mahakama ya Rufani imesema Maneno hayatengenezi matendo ya uhaini nani anayeweza kubisha?
Ni huyu Katuga?
Pia ukurasa wa 67 inasema hivi Francis Nyalali Jaji mkuu anasema kanuni kuu maneno hayatengenezi matendo ya uhaini lakini wakiwa wengi inaweza kuwa vinginevyo na isipokuwa mshitakiwa akiwa mmoja huwezi kusema maneno yake yanatengeneza uhaini.
Kwa kifupi akisema mtu mmoja kama nilivyosema mimi na nikashitakiwa mtu mmoja kama nilivyoshitakiwa mimi basi hakuwezi kuwa na uhaini ndio msimamo wa sheria ya uhaini as we speak today.
Hajalijibia hili amekimbia kimbia tu sasa kwahiyo nimesema hakuna nia ya kufanya kosa na hakuna publication na maneno matupu hayavunji mfupa kwenye uhaini.
Kuna kitu hapa amekisema sana katuga, umma, umma, umma.
Hivi UMMA ni nini? Anaongea ongea tu umma. Umma ni watanzania milioni 63+ hayo majina yanapaswa kuwepo kwenye hati yaje kuwa pleaded nimezungumza na watu fulani usipowataja ni kosa, umekosea kuandaa hati ya mashitaka.
Haya hayahitaji ushahidi, hati ikiwa mbovu inafutwa kabla mshitakiwa hajajibu shitaka, inafutwa kabla ya ushahidi ieleweke hivyo.
Anaendelea Lissu.
Waheshimiwa Majaji kabla sijaondoka kwenye habari ya publishing kwasababu sheria inasema publishing by writing or printing sasa hiyo writing or printing ni lazima iwe pleaded.
Mtakaposoma Grey Likungu mtaona hao waliopanga kupindua serikali walikuwa wanaandikiana baru na kulikuwa na chapisho linaloitwa Ukweli na hayo yote yalikuwa set out kwenye hati ya mashitaka.
Waheshimiwa majaji mkiangalia kwenye kesi hiyo hiyo kwenye ukurasa wa mwisho kabisa, ameainisha hizo overt act zaidi ya 34 because the were pleaded ziliwekwa kwenye hati ya mashitaka.
Huwezi ukasema alichapisha halafu ukaishia hapo, unapaswa kusema alichapisha nini, wapi, akapeleka wapi? Hata walete mashahidi hayapo kwenye information.
Part 34 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 32
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa Waheshimiwa Majaji wakili wa serikali akaenda kwenye kifungu cha 39(d) cha Penal Code yaani Kanuni ya Adhabu juu ya Uhaini na akarudi kesi za Grey Likungu Mataka.
Na akasema kwa Mujibu wa Grey Likungu Mataka kwamba mambo yanayofanya kosa la uhaini ni matatu makuu ndio alivyosema Katuga.
1. Utiifu kwa jamhuri ya muungano
2. Kutengeneza nia yaani nia ya kutenda kosa la uhaini.
3. Uthibitisho wa kutenda hiyo nia ya kosa la uhaini. Manifestation.
Wakili wa serikali amesema hayo masharti matatu sio pekeee.
Sasa mimi namuuliza so what?
Hayo masharti mengine mimi sijalalamikia.
Utiifu kwa jamhuri mimi sina shida na sharti hilo na hoja yangu haipo hapo.
Hoja yangu ni kwamba kulikuwa na nia ya kuunda kosa la uhaini.
Na pili hiyo nia ilithibitishwa kama inavyotakiwa?
Sharti la pili la hicho kifungu cha 39(2) cha Penal Code. Hati ya mashitaka inapaswa kuonyesha ulitengeneza nia ya kutenda kosa la uhaini.
Taarifa iliyoko mbele yenu waheshimiwa majaji inasema nilitengeneza nia ya kuhamasisha watu kuzuia uchaguzi mkuu.
Anaisoma hapo hiyo taarifa yaani Charge sheet ile hati ya mashitaka.
Wakili wa serikali hajagusa hilo hata kidogo kwamba nilihamasisha watu kuzuia uchaguzi sio kosa la uhaini wala kosa lolote la jinai.
Amekimbia kwenye hili
Hajagusa hata kidogo. Hakuna nia na sijatengeneza nia ya kutenda uhaini.
Ila nimetengeneza nia ya kufanya watu kuzuia uchaguzi wa Tanzania na hiyo sio kosa la uhaini.
Huwezi kuelewa mambo haya kama hujui sheria.
Nilisema mambo yako zaidi ya 10 yanayotengeneza kosa la uhaini wakili wa serikali akasema yako 13 sasa naomba kumuuliza kwenye hayo 13 je ni kitendo gani kinasema kuzuia uchaguzi ndio uhaini? Hakipo na hajasema hapa.
Wakili wa serikali Mkuu alivyokimbia kwenye hoja hiyo akasema kwamba.
Hii taarifa iko sawa sawa kwasababu imetaja jina langu, tarehe, kwamba mimi ni mtiifu wa jamhuri hayo yote wapi nilisema yana shida?
Anasema alitengeneza nia ya kuzuia uchaguzi mkuu wa 2025. Kama nilivyosema Waheshimiwa Majaji hilo sio kosa wala sio inshu kabisa.
Infact kwa kusema hayo anathibitisha niliyosema nia ni kuzuia uchaguzi. YES. That is not an offence under the laws of the National Republic of Tanzania.
Anasema kwa lengo la kuitisha serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Watu wazuie itishike Serikali. Waheshimiwa majaji naomba angalieni hiyo information kuna mahali nimetaja serikali? Huwezi kusema ana lengo la kuitaja serikali wakati hajaitaja serikali sikutaja hata MWENYEKITI WA KIJIJI sio serikali tu.
Sasa hayo anayosema yalipaswa kuwepo kwenye taarifa yanapaswa kuwepo kwenye hati ya mashitaka.
Iseme ulitisha serikali yenyewe inasema nilikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi, hakuna kosa la kumshitakia mtu hapa labda uwe hujitambui.
Akasema haya mambo ni ya ushahidi. Sasa watambue kuwa tukienda kwenye ushahidi hawatakuja kusema ilitishwa serikali wakati humu wamesema walikuwa na nia ya kuzuia uchaguzi.
Wasifikiri tukienda kwenye ushahidi wasifikiri wataenda kwenye UVUVI WA USHAHIDI kwamba waseme lolote.
Na facts zako kwenye Charge sheet hazioneshi chochote kuhusu kutisha serikali na kosa la uhaini.
Hawatatengeneza kosa la uhaini kwenye ushahidi kosa linatengenezwa kwenye hati ya mashitaka.
Part 33 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 31
Tumerudi sasa.
Sauti ya High Court imepigwaa na askari kwa sauti fulani hivi ya kinyonge sana.
Majaji wanaingia tayari.
Mhe. Lissu ameingia pia.
Mawakili wa serikali tunawaona.
Anaandika kidogo Jaji Nduguru na anamuuliza Mhe. Lissu kama yuko tayari.
Mhe. Lissu anasema yuko tayari na anaweza kuendelea.
Katuga: Mh. Coram iko vile vile kama ya asubuhi.
Lissu anaanza sasa.
Waheshimiwa Majaji nawashukuru sana kwa nafasi na naomba nianze kusema kosa hili ni kosa kubwa kuliko yote na lipo kwenye Katiba na adhabu yake ni kifo.
Sheria zinazotumika kwenye makosa ya jinai kama uhaini? Ni sheria za jinai. Hizo ndio hutumika. Sheria za Jinai zina utaratibu wake wa namna ya kutafsiri.
Kanuni ya Msingi ni strictly interpretation hakuna utaratibu wa kutanua au kubana kwa kadri unavyotaka.
Sheria za jinai they are interrelated strictly.
Kwa msingi huo vifungu ambavyo nimevitaja katika hoja yangu ya msingi na vifungu ambavyo amevitaja wakili wa serikali Katuga vinapaswa kuwa interpreted strictly hakuna latitude ya kutafsiri hizo sheria.
Wakili wa Serikali amekubaliana na mimi kwamba masharti ya kifungu cha 135 cha CPA basi hati hiyo inafutwa.
Pia amekubaliana na mimi kuwa Mahakama yetu ya Rufaa inasema usipozingatia kifungu cha 135 cha CPA hati ya mashitaka inafutwa.
Kwanini usipozingatia hiyo section 135 inafutwa?
Sababu imesemwa hapo hapo kwenye hicho kifungu kuwa lazima itamke statement of the offence, ionyeshe maelezo muhimu ya kumuwezesha mshitakiwa kuelewa kesi inayomkabili, kwahiyo maelezo ya shitaka yasipoeleza kosa linalomkabili basi hiyo hati ni batili na inafutwa kwasababu haitamuwezesha mshitakiwa kujua kosa linalomkabili.
Sasa waheshimiwa Majaji tumeletewa kifungu cha 138 cha CPA na mkaambiwa kwa kifungu hicho hii hoja ya pingamizi haipaswi kuruhusiwa.
Waheshimiwa majaji kifungu cha 138 cha CPA hakihusu na hakina uhusiano kabisa na content za particulars of the offence.
Hii section inaeleza tu form ya Charge sheet yani muundo wa Charge sheet na haisemi Charge Sheet inatakiwa i disclose the offence hayo yamesemwa kwenye kifungu cha 135.
Ndo maana waheshimiwa Majaji hutaona mahakama ya rufani inazungimzia 138 utaona ni 135 tu kwasababu ndio inayozungumzia hati shitaka lazima ioneshe kuna kosa.
Lakini pia naomba nidraw your attention kwenye hiyo s.138 ya CPA.
Inasema hivi……… anasoma hapa.
Kifungu hicho kikasema lazima vifungu vingine vizingatiwe.
Sasa hivyo vifungu vingine ni vipi?
Cha kwanza ni s 135 ambacho kinasema lazima hati ya mashitaka iwe na maelezo ya kosa kumueleza mshitakiwa alichokosea.
Kifungu kingine ni 295 inasema pale ambapo taarifa ina makosa na haiwezi kurekebishwa under 294 itafutwa na inafutwaje kwa hoja ya pingamizi ambayo italetwa na mshitakiwa.
Sababu ya kufutwa ni kwamba inakuwa na kosa lisilorekebishika.
Kifungu kingine ni 294 inayosema kama kuna pingamizi every objection to any formal defect shall be taken immediately after the accused person charge read over.
Mapema mtuhumiwa akisomewa shitaka anapaswa kuweka hilo pingamizi na ndo nilichofanya mimi.
Hoja ya kwamba mapingamizi ya namna hii kuwa hayaruhusiwi kwa mujibu wa kifungu cha 138 ni hoja potofu kweli kweli na inatolewa na mtu asiyejua sheria pekee na si vinginevyo.
Hoja sahihi ni kwamba hati ya mashitaka au taarifa isipoonyesha kosa inafutwa. Under 295 ya CPA.
Part 32 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 30
Anaendelea Katuga,
Mshitakiwa anapaswa kupewa nyaraka hizo lakini sio kwamba nyaraka hizo unaweza kutumia moja dhidi ya nyingine.
Maelezo ya mashahidi hayawezi kutumia hati ya mashitaka kuondoa uhalali wa hati ya mashitaka.
Kutafsiri vifungu vya sheria unaweza kwenda kwenye vifungu vingine kupata maana.
Maombi yoyote chini ya sheria hii ni lazima kuwepo na Chamber summons na affidavit sasa hakuna kifungu kinasema mashitaka haya yanafunguliwa kwa hatinya mashitaka yakiwa yamesupportiwa na maelezo ya mashahidi.
Natamani siku moja binti yangu Kylie aje kuwa Wakili lakini sitaki awe kama Katuga 😂 kiukweli napata wakati mgumu hata kumsikiliza anachosema.
Anaendelea Katuga.
Hii hoja tunaona ilitakiwa kuja mwanzoni na sio muda huu.
Sasa hivi ni afterthought kwamba witness statement ilipaswa kupingwa wakati ule wa awali na sio pingamizi la leo.
Tunaomba jambo hilo lisiruhusiwe muda huu.
Kifungu cha 11 cha CPA kinasema Police officer afanye nini anapomuhoji nani? Kinachosema hicho kifungu ni kumtenganisha police officer na shahidi mwingine wa kawaida.
Na hayo yote yanahitaji ushahidi kwahiyo tunapaswa kusubiri wakati wa ushahidi.
Sasa kesi ya Jamhuri vs Mbenga Seif Kasanwa, Abdu Masibu, Abdu Rajab.
Sasa stare decis hii ni persuasive kwenu ni kesi ya mahakama kuu hii. Haiwafungi mikono.
Ni kesi pia inayozungumziwa mazingira tofauti kabisa.
Sasa kuna kesi ya Silius Mlokozi vs Jamhuri nayo haiungi mkono chochote kuhusu madai ya mshitakiwa hapa mahakamani.
Katuga anasema hata mshitakiwa alikubali kusema haya maneno.
Amesimama Lissu anasema mheshimiwa huko hatujafika bado kwamba nimekubali kuwa nilisema au sijasema.
Nilichokuwa nakiongea mimi ni kuwa hayo maneno kwa mujibu wa katiba ibara ya 18 na kifungu cha 52 cha Penal Code na sheria ya vyombo vya habari ni maoni tu na sio kwamba nilikubali.
Jaji Ndunguru anasema sasa mjielekeze msiseme vitu ambavyo havipo hakusema hivyo labda useme maneno yanayoonekana kwenye hati ya shitaka ni haya hapa.
Imeita simu ya Polisi mara mbili inapiga kelele.
Mahakama imesimama lakini hawajachukuliwa hatua yoyote.
Angekuwa mwanaChadema hapa sijui Kama hili jambo lingepita kimya kimya maana huyu askari sijui anashida gani mara ya nne simu yake inatusumbua hapa.
Anaendelea Katuga na kusema Mheshimiwa Jaji hati ya mashitaka haina shida yoyote kwasababu imejengwa kwenye kifungu cha 138 cha CPA hivyo huwezi kuweka pingamizi.
Tunaomba kumalizia kuwa tunaomba mapingamizi hayo yatupiliwe mbali na upande wetu ni hayo tu hatuna kingine..
Majaji wanaandika kidogo na kuulizana mawili matatu.
Tunasubiri sasa Rejoinder ya Mh. Lissu sijui ataifanya Leo au na yeye atahitaji muda arudi geto huko Magereza akaandae nondo za kuwajibu hawa jamaaa.
Binafsi sijaelewa Katuga alikuwa anasema nini kwa kiwango kikubwa sana.
Ngoja tuone ngoma bado ni mbichi.
Mahakama imemuuliza Mhe. Lissu amesema anaomba health break kidogo na azungumze na mawakili pia.
Mahakama imesema turudi saa saba na nusu kwa ajili ya rejoinder kutoka kwa Mh. Lissu.
Askari Magereza wameamuriwa wasije kumzuia Lissu kuonana na Mawakili kwasababu Lissu amelalamika kuwa Mawakili wanazuiwa kule lockup.
Tunatoka muda huu kwa ajili ya Break.
Tukutane saa saba na nusu mchana.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 25
Anaendelea Mhe Lissu
Sasa hii charge sheet is incapable of amendment na sio kingine.
S. 295 (1) of CPA charge sheet isiyoelezea kosa na kueleweka inapaswa kuwa quashed ni incurable defective information na witness statement nazo zinapaswa kuwa quashed wakati huu.
Naomba nimalizie kwa maneno haya:
Nimekaa gerezani leo ni siku ya 162 nikishitakiwa kwa kitu ambacho hakipo kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Nashtakiwa kwa uhaini kwa maelezo ambayo hayaoneshi kosa lolote.
Waheshimiwa Majaji nawaombeni mtumie mamlaka ya mahakama hii kufuta uonevu huu.
Whatever you do kwa haya ambayo nimeyasema naombeni mfute uonevu.
I'm an innocent man na sijakosea nchi yangu wala kumkosea mtu yeyote.
Naomba kumalizia hapo.
Majaji wanaandika hapa.
Nafikiri hatua inayofuata ni upande wa Jamhuri kuanza kutoa majibu yao (Reply Submission) na baadae wakimaliza au hata kesho Mhe. Lissu atarudi na Rejoinder wanaita majumuisho au majibu ya majibu ya serikali dhidi yake.
Kiswahi hiki na mambo ya Mahakama. Tafrani tupu.😂
Tunasubiri hapa muongozo.
Jaji anaita Upande wa Mashitaka.
Anasimama Katuga anasema tulikuwa na ombi naomba niseme kama ifuatavyo
Defective ya mashitaka inaweza kuwa ni form au substance.
Sasa tunaona kama pingamizi la mwenzetu liko sana kwenye substance..
Mwenzetu amezagaaa kwenye maeneo mengi ya form na substance na leo ameongeza hoja mpya ya pingamizi pia hatukuwa na notice nayo hilo pingamizi.
Naona anataka kuomba poo huyu.😂😂😂
Anaendelea tunaomba na sisi tupewe nafasi tuende kujiandaaa ili tujibu na ametupatia authorities nyingi sana.
Tukisema tujibu muda huu hatuwezi kujibu kwa undani kwa kila kitu alichosema, tutajibu kwa kupalaza palaza.
Tunaomba mtupatie nafasi tukapitie kwa undani sana ili kesho tuendelee au kama Mahakama hii itaona busara kutuongeza pia siku zingine tutashukuru.
Kifungu cha 302 Cha CPA, kinaipa mamlaka mahakama hii kuweza kuahirisha shauri hili.
Nawahesabu mawakili karibu saba wapo hapa eti wanapirukushana na mtu yuko jela tena mmoja tu wakat wao wapo kikundi wanasema baada ya mawasilisho yote haya hawajaona hata waanze kujibu leo na wamalizie kesho.😂
Jaji anamuuliza Lissu. Lissu anasema wasikilize tu wao wanataka muda gani mimi nimesema mambo mazito sana na kama mawakili 6 wa serikali wanahitaji huo muda na wanaona utawatosha kujiandaa acha tuone wataenda kujiandaa na nini?
Jaji anaandika hapa
Amesema tukutane Tarehe 18/09/2025 saa tatu asubuhi.
Jaji anasema anaomba leo tusiimbe sana baada ya muda wa Mahakama kuisha.
Watu wanacheka 😂😂😂
Leo tunaishia hapa, tuonane tarehe 18
Nawatakia wakati mwema.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 8
Tumerudi Majaji wameingia.
Kama kawaida wako watatu.
Kumbukumbu ni kwamba tuliahirisha ili Mh. Lissu akasome nyaraka za proceedings alizopewa leo mara baada ya zile za kwanza alipewa nusu ambazo zimeanzia Tar. 18/08 na sio kuanzia Tar. 10/04.
Ngoja tusubiri mrejesho.
Je tutaendelea na shauri au hatutaendelea nalo? Je Mhe Lissu amesema amekuta mambo gani huko kwenye nyaraka alizopewa leo na je zina utofauti gani na zile alizokuwa amepewa mwanzo. Tutajua muda sio mrefu.
Majaji waaandika kidogo hapa.
Jaji anasema naomba tuendeleee.
Anasimama Katuga anasema Corum iko vilevile na mshitakiwa yupo.
Jaji anasema ongeza sauti.
Katuga anarudia hapa alichokuwa anazungumza.
Mshitakiwa yupo na shauri linakuja kuendelea na kusikiliza mapingamizi au wasilisho wa mshitakiwa kwenye suala la mamlaka ya mahakama hii.
Lakini pia tulikuwa na concern kwamba wenzetu wa Magereza wanasema barabara haziko vizuri tunaomba tusifike usiku sana.
Ni hayo tu mheshimiwa Jaji.
Kwa maneno mengine KATUGA anatuambia barabara za nchi hii ni tatizo sana.
Anapewa nafasi Mh. Lissu.
Mh. Lissu anasema sitawaweka sana kwa leo asiwe na hofu.
Nimepata hii record saa 10 kasoro dakika mbili na mlisema tukutane saa 10 na dakika kumi. Kwahiyo nimepata dakika 12 pekee za kupitia hiyo nyaraka.
Sasa sijaenda mbali sana kwenye kuisoma hii record. Hivyo naomba niseme lifuatalo.
Ukizisoma hizi nyaraka mbili ambazo zote nimeletewa.
Ukisoma zote kuna jambo limefanyika nafikiri litakuwa ni kosa la jinai.
Kuna criminality involved.
Record mliyoagiza nipewe na nimepewa. Precedings za Tar. 18/08 nilizopewa mwanzo.
Kwenye hii mpya niliyopewa Proceedings za Tar. 18/08 zinaanzia ukurasa wa 80.
Kwahiyo kwa kuhesabu idadi ya kurasa hizi nyaraka nilizopewa zinatofautiana.
Jambo lingine from page 86 kwenye hii niliyopewa leo kuna kitu kimeandikwa proceeding halafu kuna COURT ORDER iko page 86 hadi 89 lakini kwenye hii niliyoletewa mwanzo. Hiyo ORDER haipo kabisa.
Niliyoletewa gerezani haina hizo page kabisa za hiyo Court ORDER.
From page 94 to 98 kwenye niliyoletewa mahakamani ziko page 6 to 14 kwenye niliyopewa mahakamani.
Sasa hizi nyaraka zote nimepewa zikionekana ni nyaraka za mahakama?
Kwanini zitofautiane? Kwanini niletewe nyaraka gerezani ambayo sio yenyewe na ambayo nilipaswa kupewa.
Wako watu wamegushi kuna doctoring hapa. Zimeghushiwa. Zimefanyiwa mchezo mchafu.
Part 9 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Anasimama Mhe. Lissu kuanza na suala la jurisdiction kwanza.
Ameleta pingamizi kuwa mahakama hii haina mamlaka kivipi kusikiliza kesi hii.
Mh. Lissu anaanza kwa kusema taarifa hii niliyoitoa nilishaitoa mapema huko nyuma hasahasa mahakama ya Kisutu.
Naomba niibadilishe hiyo hoja kidogo sana.
Hoja yangu isomeke mahakama hii haina mamlaka ya kusikiliza kesi hii kwasababu ya makosa mengi na makubwa yanayoonekana kwenye uso wa rekodi ya mahakama ya ukabidhi (committal Court) yaani ile mahakama ya kisutu.
Makosa hayo yameuharamisha utaratibu wote wa committal Court.
Anasema kingereza chake cha haya niliyoyasema ni hiki. Anatema ung'eng'e kwamba under section 184 of CPA on the face of record the committal proceedings includes irregularities.
Jaji anauliza tunaachana nayo kivipi? Anamjibu kuwa nilichokwambia kwa sasa ndio iwe record yako na nitazungumzia kwa namna nilivyoliweka hili pingamizi kwa sasa. Tuendelee kwa utaratibu huo tafadhali. Wanakubaliana hapa.
Mh. Lissu anaendelea anasema naomba nianze kuweka msingi wa kisheria.
What is the law on committal proceedings? Hii sheria inasemaje na ikoje?
Kif. cha 261cha CPA kinasema pale ambapo shitaka limepelekwa mahakamani dhidi ya mtu yeyote kwa kosa ambalo haliwezi kusikilizwa na mahakama ya chini basi mashauri ya ukabidhi (committal case) itafanyika katika mahakama ya huko chini.
Anasoma hapa hicho kifungu cha sheria kilivyoandikwa.
Kwahiyo committal proceedings ilipaswa kufanyika kwenye hiyo mahakama ya chini.
Kifungu cha 184 of CPA kilipaswa kusomwa pamoja na kifungu cha 261 nilichosema awali.
Ambapo kinasema hakuna kesi ya namna hii itaendelea hapa bila ya mtuhumiwa kuwa committed kwenye mahakama hii ili iweze kusikilizwa.
Sasa sheria inasema utaratibu wa Committal lazima ufuatwe ili tuendeleee vizuri hapa leo.
Mahakama ya rufani ya Tz ineweka msimamo wake kwneye nasuala haya kesi ya Jamhuri vs Dodoli Kapufi na wenzake. Criminal Rev. CAT At Mbeya.
Ninayo nakala moja niko gerezani, ukurasa wa 25 sect. 178 of the CPA creates a bar against a taking of cognizance unless the same has been investigated and the accused have been committed duly committed for trial.
Kwanza lazima iwe properly investigated na pia iwe duly yaani properly ina accordance of the law.
Hayo masharti kwa namna ya kuifanya hiyo kesi ifike hapa jwenye mahakama hii. Je masharti hayo ni yapi? Masharti gani hayo?
Kif. Cha 262(1) cha CPA kinaweka sharti la kwanza la committal processes.
Kinasema kwamba pamoja na mambo mengine sharti la kwanza unapelekewa kwenye mahakama ya eneo ulilokamatiwa.
Mimi nilikamatiwa Mbinga, mkoa wa Ruvuma. Committal proceedings zimefanyikia Kisutu Dar es salaam. KM nyingi kutoka Mbinga. Sheria ilisema nipelekwe nilipokamatiwa.
Sharti la Pili ni la kusomewa shtaka kif. 262(2) cha CPA na hatatakiwa asijibu.
Sharti la tatu, liko kwneye kifungu cha 262(3) of CPA baada ya charges kusomwa mtuhumiwa aambiwe kuwa hatapaswa kujibu na atapelekwa gerezani.
Sharti la nne ni kwamba liko 262(6) of CPA baada ya upelelezi kukamilika ataandaa information (mashtaka) kwa mujibu wa sheria na kuyafungua mahakama kuu.
Sasa waheshimiwa ma jaji sharti muhimu kwa ajili ya hoja yangu ya leo lipo kwneye section 265(1) ya CPA.
Kifungu hicho kinasema kuahirishwa kwa kesi wakati wa committal. Nitakielezea pia.
Part 6 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 2
Anaendele kuzungumza Mhe. Lissu
Mimi niliyesema hayo maneno nitajitetea na niwasikilize hao wanaosema nimefanya uhaini kuwa nimetenda makosa hayo.
Naomba pia mfahamu kabla mahakama hii haijaniteulia mawakili toka tukiwa kisutu sijawahi kuwa na upungufu wa mawakili zaidi ya 50 na baadhi yao wapo hapa leo.
Niliwaambia ambayo nimesema haya kwenye kesi kama hii sitataka mtu anizungumzie nilisema hivyo toka Kisutu na tulielewana.
Nafahamu uzito wa kesi kama hii Waheshimiwa Majaji, anayeshtakiwa ana haki ya kuwakilishwa na mawakili hata kama hana uwezo mahakama itamtafutia Wakili wa kumsaidia.
Mimi uwezo ninao na suala la kwamba sina uwezo hilo halipo. Mimi uwezo ninao.
Pili watu wanaostahili kuwekewa mawakili ni wale ambao wanakabiliwa na makosa makubwa na hawawezi kujitetea wenyewe.
Mimi nina uwezo wa kujitetea mwenyewe. Mimi ni Wakili wa Mahakama hii kwa miaka 23 hadi leo kama Wakili.
Nimefanya kazi ya uanasheria huu ni mwaka wangu wa 31, There is no question whatsoever to defend my self.
Najitetea mwenyewe kwasababu this is ultimate test, huu ndio mtihani mkubwa kwa mfumo wetu wa kisheria.
On this one, kwa heshima zote I will take full responsibility for myself.
Nitaweza to the best of my ability..
This is about my life. I will defend myself to the fullest.
Naomba niseme jambo kuhusu hili jopo la Mawakili toka Kisutu naomba katika kesi hii waendelee kuwepo wanisaidie kwenye research maana gerezani hakuna mtandao hakuna library kule.
Waendelee kuwepo ili wanisaidie nijiteteee kwa ukamilifu.
Na kama hilo litawapendeza nitafurahi kama watatambulishwa na pia hata huyu Wakili Neema Saruni atakubali na yeye awe sehemu ya jopo hilo la Mawakili wataonisaidia kufanya research.
Majaji wanaandika kidogo hapa.
KATUGA anasema tumefuatilia wenzetu mshitakiwa pamoja na Wakili wake.
Kwa mujibu wa kifungu cha 329 cha sheria ya mwenendo wa jinai kinatoa haki kwa mshitakiwa kuwa na uwakilishi kwneye kesi inayomkabili.
Ingawa haki hii sio ya lazima, busara ya mahakama ilimpa Wakili kwa ridhaa yake anaiambia Mahakama hii kujitetea mwenyewe.
Kwenye hiyo hoja ya kujitetea mwenyewe kwakuwa amesema ni mbobezi wa sheria hatuna pingamizi kwenye hilo.
Lakini upande wa jamhuri unasita kukubaliana kwenye hoja ya kuwa ana mawakili ambao watamsaidia kufanya research na watambulishwe.
Hatupingi wao kumfanyia research lakini tunapinga wao kuingia kwenye rekodi. 🤣🤣huyu Baba ana wivu hata watu kutambulishwa, utadhan wakitambulishwa kuna kitu kitapungua kwenye mwili wake.
Anaendelea pale kunapokuwa na kesi ya pande mbili. Lazima Wakili apate nafasi ya kuwa na mtu anayemuwakilisha, hawa wasitambulishwe kabisa.
Jaji anaeongoza jopo la Majaji ni Mh. Dunstan Ndunguru
Huyu Katuga anaongea watu wana hasira nae ni kama wanataka kupasuka hivi sijui hata huyu ndugu anatafuta nini kuna mambo watu wanashangaa kwanini amekuwa na akili kama za mkaanga sumu.
Wanateta jambo mawakili wa Serikali.
Mh. Lissu ameulizwa unasemaje anasema mimi sina shida hata tusipowatambulisha. Tuendelee kwenye mambo ya msingi.
Nilidhani ni jambo dogo lisingekuwa na nongwa kama wenzetu wameona ni nongwa basi tuendelee na kazi ya leo, Mimi sina shida.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii
Wana Chama Wa Chadema Na Wapiga Kura Wote Ndani Ya Chadema Tunaomba Mtuletee @TunduALissu Na Makamu wake @HecheJohn Kwenye Uchaguzi huu. Sio tu Matakua Mmekiokoa Chama Chenu.!Mtakua Mmeleta Tumaini Jipya Kwa Watanzania Ata Ambao sio Wana Chadema.
Chapaa REPOST 1000 🤞