“Rais Magufuli alilazwa March 6 Hospitali ya J.Kikwete na kuruhusiwa March 7 na kuendelea na majukumu, March 14 alijisikia vibaya na akarudi Hospitali ya Mzena kutibiwa hadi umauti unamkuta, Nchi yetu itakuwa na maombolezo ya siku 14 na bendera nusu mlingoti” ——— VP. Mama Samia.
Kwa masikitiko makubwa tarehe 17th March 2021, saa 12 jioni tumempoteza Rais Dr. John Pombe Joseph Magufuli ambaye amefariki kwa maradhi ya moyo katika hospitali ya Mzena jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi.