Mwakilishi wa ACT-Wazalendo wa Jimbo la Gando Pemba, Said Ali Mbarouk ambaye pia ni Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia nafasi za uwakilishi, ameitaka Serikali ya Muungano kufanyia marekebisho utaratibu wa Zanzibar kukopa fedha kwa ajili ya maendeleo.
Akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) inayoendelea kujadiliwa leo Juni 18, 2026, Mbarouk amesema Zanzibar imekuwa ikikumbana na changamoto ya kuhitaji idhini kutoka Tanzania Bara kila inapokusudia kukopa, hali anayodai wakati mwingine husababisha kucheleweshwa au kukwamishwa kwa mipango ya maendeleo.
Amesema utaratibu huo umekuwa ukileta โchenga za kifedhaโ na kuathiri kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kisiwani humo, hivyo akataka kuwepo kwa mjadala wa kina kuhusu namna Zanzibar inavyoweza kuwa na uhuru zaidi wa kifedha ndani ya mfumo wa Muungano.
Aidha, amegusia suala la ongezeko la deni la Taifa la Zanzibar, akieleza kuwa baadhi ya Taasisi zimekuwa zikibanwa kifedha, hali inayoweza kuathiri utekelezaji wa shughuli nyingine za Serikali.