#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 433
Jaji Ndunguru anawasha kipaza sauti anasema tumesikia hoja za mshtakiwa na Mahakama inatamka kwamba shauri kwa upande wa utetezi limefikia mwisho.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji kwa vile sasa kesi ya pande zote mbili imefungwa tunaomba Mahakama itupangie siku ya kuja kuwasilisha hoja za mwisho.
Sijawasiliana na upande wa mashtaka naomba nipendekeze tarehe yangu ya kuwasilisha hoja za mwisho.
Waheshimiwa Majaji natambua kwamba shauri limepangwa kuisha tarehe 25 September 2026 na mwenendo wa kesi una kurasa zaidi ya 1000, itakuwa kazi kubwa sana lakini naomba mimi kuanzia Jumatano ya tarehe 23 Septemba 2026 nitakuwa tayari kwa ajili ya kufanya final submission.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka mnasemaje?
Katuga: Tunaungana na mshtakiwa ila hajasema tufanye kwa maandishi au kwa mdomo.
Kwa tarehe aliyoipendekeza sisi tutajitoa Jumatano hiyo hiyo na sisi tutakuwa tayari kufanya final submission. Waheshimiwa majaji ingawa upande wa utetezi umefunga kesi ila tulikuwa na hamu sana ya kufanya cross kwa mashahidi wa Lissu waliokuwa wamebakia
Watu wanacheka sana, wanamuona Katuga kama kituko😂😂😂😂
Jaji Ndunguru: Hiyo amri mbona mahakama bado haijaitoa?
Tunakubaliana kuwa siku ya Jumatano shauri litakuja kwa ajili ya mawasilisho ya mwisho saa tatu kamili asbuhi
Imepigwa High Coooouuuuurrrrtttttt
Majaji wanatoka,
Mhe. Lissu anaangana na Mawakili wake pamoja na Viongozi wa Chama pamoja na watu mbalimbali waliojitokeza Mahakamani.
Naomba Repost yako.
Tundu Lissu ameeleza Mahakama Kuu kwamba, ameelezwa na DCI Ramadhan Kingai, hata CDF Jacob Mkunda na IGP Cammilius Wambura pia hawapo tayari kutoa ushahidi upande wa utetezi, kwa sababu ile ile wapo upande wa watu watakaoshangilia TAL akipatikana na hatia ya kunyongwa hadi kufa.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 18, 2026
Last time tuliishia part 431 so leo tunaendelea na -;
Part 432.
Mhe. Tundu Lissu ameingia Mahakamani watu wana vibe sana wanaimba Mwamba Mwamba huku wakipiga makofi mengi sana.
Majaji wote watatu wameingia na kuketi kwenye viti vyao.
Wakili wa Serikali Ajuaye amesimama na kutambulisha jopo lake na kuwa wako tayari kuendelea.
Mhe. Lissu na yeye anasema niko tayari kuendelea.
Mhe. Lissu amesimama na kusema kwamba nimekutana na Kamishna wa Polisi Ramadhani Kingai ambaye nilikuwa nimependekeza awe shahidi wangu wa leo, nimekutana nae Mahakamani kwenye chumba hiki hiki waheshimiwa majaji, naweza kuthibitisha kwamba ameheshimu wito wa Mahakama amekuja na nimezungumza nae kuhusu yeye kuwa shahidi wa upande wa utetezi na nimezungumza nae kiasi cha kutosha, baada ya kumueleza maeneo ambayo ningependa ayatolee ushahidi ameniambia kwamba yeye hawezi na hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wangu kwa maneno yake mwenyewe amesema
“Yeye yuko upande wa wale wanaoomba na watakaoshangilia nikipatikana na hatia”
Kwahiyo amesema hayupo tayari kuja kutoa ushahidi kwa niaba yangu.
Nimemuelewa Waheshimiwa Majaji kama hayuko tayari siwezi kumlazimisha kutoa ushahidi ambao hataki kuutoa.
Waheshimiwa Majaji Kingai ameniambia kitu kingine kuhusiana na mashahidi wengine wawili IGP Camillius Wambura na CDF Jacob Mkunda, amesema vilevile hata wao watakaporejea nchini na kupata wito wa Mahakama msimamo wao utakuwa ni huo huo kwamba na wao hawatakuwa tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi kwasababu ile ile kuwa wako upande wa wale wanaoombea na watakaoshangilia nikipatikana na hatia.
Katika Mazingira haya waheshimiwa majaji maana yake ni kwamba sina mashahidi zaidi kwahiyo naomba kufunga ushahidi kwa upande wa utetezi.
Ni hayo tu waheshimiwa majaji.
Naomba Repost yako.
Tundu Lissu amepanda kizimbani na kuieleza Mahakama Kuu ya Tanzania kwamba DCI Ramadhan Kingai amesema hayupo tayari kutoa ushahidi upande wa utetezi na amemueleza (yeye) yupo upande wa wale watu ambao watashangilia na kufurahi Mahakama ikimkuta na hatia ya kunyongwa hadi kufa.
Mpaka sasa Mahakama bado haijaanza lakini Mawakili wa Mhe. Lissu walishafika tangu saa tatu asubuhi.
Ramadhan Kingai na yeye yupo ila analindwa na Mapolisi wa kutosha sijui anahofia kuhusu Ukatili ambao walitufanyia Oktoba 29, 2025 so anahisi raia wanaweza lipa kisasi maana sio kwa hofu hii?
Mawakili wa Serikali wameingia muda sio mrefu na sasa tunasubiria Majaji na Mhe. Lissu waweze kuingia ili shauri liweze kuanza, tujue nini kinaendelea.
Huyu kwenye picha anaitwa Joseph Cosmas Maduka, mhitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ngazi ya Masters, hajulikani alipo tangu Jumapili September 13, 2026.
Kwa taarifa ambayo Familia yake yanayo ni kwamba, mara ya mwisho alionekana maeneo ya Posta, Dar es Salaam tangu siku hiyo hadi leo hajapatikana, na familia pamoja na ndugu zake hawajui alipo.
Familia tayari imejaribu kutoa taarifa Polisi, lakini hadi sasa bado hajapatikana.
Tunaomba msaada wa kila mmoja kupaza sauti na kusambaza taarifa hii. Mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu alipo Joseph Cosmas Maduka, tafadhali awasiliane nnasi kwa namba 0622 248 469.
KINACHOENDELEA MAHAKAMA KUU YA DAR ES SALAAM MUDA HUU.
Muda huu saa sita mchana, Jengo zima la Mahakama umeme umezimwa, kuna giza nene kama tupo kuzimu halafu njee kuna mvua inaendelea kunyesha.
Msajili wa Mahakama hii, Lyakinana anawaogopa sana Magereza na hawa Mapolisi wa Kingai utadhani wao ndo wanamlipa mshahara, kwasababu Mapolisi ndio wanaamua nani akutane na Mwenyekiti Lissu na nani asikutane nae na yeye ndo aliyepewa order na Kingai kwamba azuie Mawakili wetu wasionane na Mhe. Lissu.
Sasa hivi wanapanga kupunguza viti ndani ya ukumbi Mahakamani ambao huwa tunautumia siku zote lengo likiwa ni kupunguza idadi ya watu watakao ingia ndani ili wasingizie kwamba ukumbi umejaa, kumbe wameondoa viti.
Mazingira hayo yanaonekana toka asubuhi muda ambao Mawakili walitakiwa kuingia kumuandaa shahidi wakishirikiana na Mh. Tundu Lissu.
Tunasubiri hiyo saa nane mchana tujue nini kimeendelea.
Taarifa kutoka vyanzo vyetu hapa Mahakamani vinasema Mwenyekiti Lissu amekutana kwa muda dakika 10 na Ramadhani Kingai na inaonekana kuna jambo halijaenda vizuri japo tunahisi huenda Mhe. Lissu atakuwa amemwambia hatuwezi kuendelea bila uwepo wa Mawakili wake, ambao wangesaidia kumchukua maelezo ya maandishi ya shahidi wake kabla hajaenda kutoa huo ushahidi Mahakamani.
Ukweli wa yote tutaujua baada ya masaa mawili kutoka sasa so tuwe na subira.
‼️KUTOKA MAHAKAMA KUU DAR ES SALAAM‼️
Mwenyekiti wetu Mhe. Tundu Lissu ameshafika Mahakamani tangu majira ya saa tatu asubuhi.
Ramadhani Kingai DCI nae amefika na kuletwa na Makachero zaidi ya thelasini, anaulinzi mkali sana Hii nadhan ni kwasababu ya damu walizomwaga Oktoba 29.
Cha ajabu ni kwamba Mawakili wa Mhe. Tundu Lissu wamezuiwa kuwepo ndani wakati Mwenyekiti anamuandaa Shahidi wake Ramadhani Kingai wakati mashahidi wengine wote waliandaliwa mbele ya Mshitakiwa na Mawakili wake.
Hatujui zoezi la kumuandaa huyu Shahidi litaenda kwa utaratibu gani? Kwasababu Mwenyekiti yuko peke yake huko ndani so hatujui zoezi linaendelea kwa utaratibu upi wakati Mawakili hawajaruhusiwa kuingia.??
Vitimbwi ni vingi na hujuma ni nyingi sana halafu wameanza mapema kabisa.
Ikumbukwe kwamba Last time, Kingai alipokuja Mahakamani kwenye kesi ya Ugaidi dhidi ya Mbowe na Makomandoo alizuia watu kuingia Mahakamani, na walioingia aliwakagua yeye mwenyewe na kutaka kuwanyang’anya simu zao, alitaka nyang’anya simu hadi za Mawakili wa Mhe. Mbowe, Mawakili waligoma kuendelea na kesi, Matokeo yake kesi ilibidi ihairishwe ili upatikane ufumbuzi baada ya Mawakili wetu kukomaa ndo ikabidi Jaji aruhusu watu waingie na simu zao, kipindi hicho alikuwa RPC Kinondoni.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 431
Tumerejea Mahakamani.
Imepigwa high court
Majaji wanaingia muda huu ili tupate mrejesho wa nini kinaendelea kuhusu wale mashahidi wengine.
Anasimama Katuga anasema Corum yao ni ile ile na mshitakiwa yupo na shauri linaendelea kwa utetezi na sisi tuko tayari.
Anasimama Mhe. Lissu anasema baada ya maelekezo ya Mahakama nimewasiliana na Mhe. Msajili wa Mahakama hii amekuja kuniona na kuniambia kuhusu utekelezaji wa amri ya Mahakama kuhusu kuwaita hao Mashahidi watatu.
Mhe. Msajili amenitaarifu kuwa Mashahidi wote watatu walipelekewa wito Dodoma, hata hivyo haikuwezekana kuwaserve nakala za summons kwasababu wote watatu wapo nje ya nchi.
Mhe. Msajili amesema kati ya hao watatu mmoja ambae ni Kamishna Wa Polisi Ramadhani Kingai, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai anatazamiwa kurudi nchini leo.
Na Msajili ameniahidi kwamba siku ya Ijumaa kamishna wa Polisi Kingai atakuwepo Mahakamani ili kutekeleza huo wito wa Mahakama.
Wale wengine wawili Jenerali Jacob Mkunda na Wambura IGP hawajulikani watarudi lini?
Katika Mazingira haya napendekeza Mahakama iahirishe shauri leo hadi ijumaa saa nane na nusu Mchana ili ile session ya asubuhi niweze kuitumia kushauriana na huyo shahidi ambae atakuja, ikiwa ni pamoja na kuchukua maelezo yake.
Na natumaini Waheshimiwa Majaji by saa nane na nusu tutakuwa tayari kuendelea nae na kuhusiana na waliobaki itabidi tusubiri tumalizane na huyu tuliyenae ili tufanye maamuzi baadae na hao wengine.
La mwisho ninafahamu jinsi ambavyo ratiba ya shauri hili iko tight na naomba niwafahamishe kuwa na sisi twende kwenye final submission ili muweze kukaa baadae kutafakari na kuamua kesi hii.
Vyovyote itakavyokuwa kama watatii wito wa Mahakama ni imani yangu kwamba hatutachukua muda mrefu.
Na wasipokuja kabisa hilo litakuwa mikononi mwenu maana nyie ndio mmetoa wito wa wao kuja kutoa ushahidi, Mimi ya kwangu ni hayo Waheshimiwa Majaji.
Katuga kwa masikitiko hatuna pingamizi la kupinga ahirisho na Mahakama ilipoongeza session hii hadi Tar. 18/09
Jaji Nduguru anasema sisi tuliongeza 14 working days.
Katuga: Basi tunaomba Mahakama imsisitize Mshitakiwa Mashahidi wake waweze kufika.
Watu wanasonya 😂😂 😂
Jaji Ndunguru: Sasa jamani hao si mashahidi wa Mshitakiwa mnaguna nini? Mshitakiwa anajua namna ya kufuatilia. Hebu uwe unawaelekeza.
Katuga: Pia kuhusu ombi lake la kwamba wasipokuja hao mashahidi anaiachia Mahakama hilo hawezi kuiachia kwasababu yeye ndio mashahidi wake na Mahakama imeshatoa summons kwahiyo atasema anaiomba nini Mahakama?
Jaji Ndunguru: Anacheka kwamba the court is not your nini ile huwa mnarushiana humu.😂
Majaji wanateta hapo kidogo.
Jaji Ndunguru: Tukutane Ijumaa saa nane kamili mchana.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 430
Mhe. Lissu anasema amemaliza maswali ya Re Examination.
Job Mrema amesimama na kusema tunaleta chini ya kifungu cha 156(4) cha Sheria ya Ushahidi Sura ya 6.
Mahakama itumie mamlaka yake ili tuweze kumrecall na kufanya further cross examination na kwa mujibu wa kumbukumbu siku ya jana alitoa ushahidi wake hapa Mahakamani kuhusiana na shauri hili na akiwa chini ya kiapo alitoka Mahakamani na kwenda kuzungumza na kuzalisha ushahidi mwingine.
Tunaona ushahidi huo utaisaidia Mahakama kutenda haki na alikwenda kusema akiwa chini ya kiapo. Tupewe nafasi tumuulize maswali kuhusu ushahidi huo aliousema na Naomba kuwasilisha.
Anasimama Mh. Lissu amekunja sana uso.
Majaji wanasema kaa kwanza mshitakiwa. tunataka kujua mambo kadhaa.
Jaji Ndunguru anauliza sasa mtu akiapa Mahakamani kwahiyo akienda hata nyumbani anakuwa chini ya kiapo? Hebu tusaidie kuelewa.
Watu wanacheka sana 😂😂😂
Job Mrema: Waheshimiwa Majaji kiapo amelala nacho kwasababu alipoapa alikuwa nacho, akifika hapa anaambiwa kiapo chapo kinaendelea.
Kwahiyo shahidi huyu afanyiwe further cross examination, sisi tumeangalia ni kwamba moja ya sababu yuko kwenye kiapo na kiapo chake hakijasitishwa, shahidi huyu akiwa bado kwenye kiapo. Amezalisha ushahidi.
Jaji Ndunguru anateta na wenzake hapo.
NB. Katuga mjinga ila kwenye hili naona ujinga wake umemtuma asiliseme hili yeye amuache kilaza Job Mrema. Huyu Mrema kwa kumbukumbu zenu ni miongoni mwa Mawakili waliokwenda kutetea ndege za Tanzania zilizokuwa zimezuiwa Afrika ya Kusini halafu Serikali ikaangukia pua na Kingereza chake kilikuwa ni ZE ZE ZE ZE ZE Mwanzo mwisho. Nitawatafutia ile video niwatumie hapa muone kiwango cha ukilaza.
Jaji Ndunguru: Tulikuwa tunaangalia off record.
Cross Examination inatokana na examination in chief sasa kama kitu kimeongelewa huko kwani kipo hapa Mahakamani??? Hilo pia la kwamba kiapo ameenda nacho hadi nyumbani hiyo tafsiri yako haiko sahihi, Ushahidi uko Mahakamani na mnamuuliza mambo yaliyosemwa Mahakamani.
Hayo mengine hayapo Mahakamani. Kwahiyo ombi hilo halina mashiko.
Mhe. Lissu anasimama anasema Waheshimiwa Majaji niliomba summons kwa ajili ya mashahidi kwahiyo nataka kujua majibu kuwa mashahidi hao wako wapi na tunakwendaje mbele.
Pia siwezi kumuweka shahidi kizimbani kabla sijamuanda kwahiyo lazima nikutane nao na niwaelekeze cha kufanya ili wakija kugeuka hapo kizimbani basi niwashughulikie sawasawa.
Eneo la kuwaandalia Mashahidi na kukutana nao ni hapa hapa Mahakamani kwasababu sina eneo lingine ambalo naweza kukutana na mashahidi wangu.
Siwezi kwenda ofisini kwao wala gerezani so nilazima tuonane na kupanga hapa hapa Mahakamani.
Jaji Ndunguru anasema tulitegemea utuambie kuwa una shahidi au hauna maana ni mashahidi wako na Mahakama ilishatoa summons kwahiyo tutabreak ili msajili atupatie feedback.
Tukutane saa tano na dakika aroboini.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo September 16, 2026
Last time tuliishia part 428 so leo tunaendelea na -;
Part 429
Mahakama imeanza.
Imepigwa high coooooourt
Majaji wameingia.
Mhe. Lissu nae ameingia kama kawaida makofi mengi yanapigwa mengi kwa ajili ya kumkaribisha Mwenyekiti Tundu Lissu.
Katuga anawatambulisha wenzake.
Jaji Ndunguru anasema tuendeleee.
Anasimama Mhe. Tundu Lissu anasema naomba kuzungumza kidogo na shahidi wangu naona amenitumia ujumbe hapa kabla hatujaendelea na nitamfuata.
Wanaenda kuzungumza Mhe. Lissu na Mhe. Heche pale kwa dakika kama tatu.
Wanaongea na kutikisa vichwa wamekubaliana wamemaliza na Mhe. Lissu anarejea kwenye kizimba chake.
Majaji wanazungumza kama dakika tano sijui wanajadili nini?
Mhe. Lissu: Shahidi kuhusu suala la Utekaji na ripoti ya SADC.
Heche: Hilo suala la Utekaji ukurasa wa 6 wa ripoti hiyo unazungumzia masuala ya Utekaji.
Katuga: Ukurasa wa 6 hakuutaja wakati wa kutoa ushahidi huo.
Mhe. Lissu: Tusipotezeane muda toa neno ukurasa wa 6.
Heche: Suala la Utekaji lipo kwenye ripoti ya SADC ukisoma utaona.
Mhe. Lissu: Ulisema maneno ya utekaji, kukinukisha kwamba sio kila mahali nilitumia hayo fafanua?
Heche: Nilimaanisha maudhui ni yaleyale kuzungumzia mfumo wa Uchaguzi. Choice of words tu ndio lilikuwa ni suala linalotofautiana.
Mhe. Lissu: Kuhusu Uchaguzi wa Tarime ukasema haukuwa huru na haki na hivyo hupaswi kuwa Mbunge na haukuwa na mamlaka hayo ya kukataa kuwa mbunge au hukuwa na huo uwezo?
Katuga: Hatukuuliza hivyo.
Mhe. Lissu: Rekodi zituongoze.
Jaji: Sikuwa na uwezo wa kukataa kuwa Mbunge
Heche: Ufafanuzi wangu ni kwamba returning officer ndio anatangaza Mbunge.
Mhe. Lissu: Mkurugenzi wa Uchaguzi akawa mgombea na sasa ni Mbunge wa Butiama na ukasema haikuwa sahihi. Fafanua?
Heche: Nilisema kwamba kanuni za CCM zinataka mwanachama wake ili agombee anapaswa kuwa na uanachama wa miaka mitano.
Kwahiyo naamini alijiunga na CCM akiwa bado ni Mkurugenzi wa Tume maana asingeweza kuruhusiwa kugombea ikiwa takwa la miaka mitano bado hajakidhi.
Mhe. Lissu: Tume ya Chande uliulizwa kuhusu wewe au Chama kuitwa. Na ukaoneshwa na mabarua mengi lakini ukasema hukuitwa. Fafanua. Usiingize mambo mapya Wakili wa Serikali atanuna.
Heche: Mimi sikupokea barua yoyote ya Mwaliko kutoka tume ya Chande na kuhusu Chama hakikupokea maana kilikuwa kimefungiwa.
Katuga: Kuhusu chama isiingie maana hakusema hivyo.
Mhe. Lissu: Tusomewe record inasemaje?
Jaji Ndunguru: Alipoitwa na tume ya Jaji Chande. Barua ilikuwa ameandikiwa Katibu Mkuu na haikuandikwa kwa Chama.
Heche: Haikuwa addressed kwa Chama.
Mhe. Lissu: Uliulizwa na maswali kuhusu Chama kwenda Bungeni na kutoa maoni kuhusu muswada wa Sheria. Kuhusu kuwaondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi.???
Heche: Bado watumishi wa umma ndio wanasimamia Uchaguzi na mapendekezo yetu yalikuwa ni Tume kuwa na Wafanyakazi wake kuanzia ngazi ya kitaifa hadi chini na sio watumishi wa umma.
Mhe. Lissu: Kuhusu Thabo Mbeki Foundation na Mwalimu Nyerere Foundation tofauti yake. Fafanua
Heche: Thabo Mbeki Foundation inafanya kazi nchi zaidi ya moja tofauti na Mwalimu Nyerere Foundation ambayo inafanyakazi Tanzania tu ndo maana nilisema yenyewe ni International.
Part 430 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 428
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Re- examination, Makam Mwenyekiti Bara John Heche.
Mhe. Lissu: Ulionyeshwa video ukaulizwa kama ni wewe na kama hayo maneno yanaelekea kuwa ni ya kwako na ukasema hukumbuki kutoa hotuba ya aina hiyo.
Heche: Sikumbuki kutoa hotuba hiyo, wametumia akili mnemba kuitengeneza.
Mhe. Lissu: Fafanua Akili Mnemba
Watu kicheko😂😂😂😂
Heche: Akili Mnemba ndio Artificial Intelligence (AI)
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu magari manne ya bei mbaya ukasema una magari mawili, fafanua.
Heche: Nilimaanisha nina Prado na Hilux ambazo ndo huwa nazitumia, hiki ndo nilichomaanisha.
Mhe. Lissu: Unakumbuka kuhusu kukamatwa kwako nje ya Mahakama na kuwa unapelekwa Tarime, Uliulizwa ulienda Kenya? Ukasema nilizuliwa, fafanua.
Heche: Nilizuiliwa na immigration kwenye mpaka wa Sirari.
Mhe. Lissu: Unakumbuka uliulizwa na mawakili wa Serikali kuhusu wewe kukutana nao Oysterbay Police na walisema kwamba 70% ya waliokamatwa walikutaja wewe kuwa unahusika na kuratibu wewe hizo vurugu, ukasema hujui , fafanua.
Heche: Nilikuwa ndani tangu tarehe 22 Oktoba 2025 kwa vyovyote vile siwezi kuhusika na yaliyotokea Oktoba 29, 2025.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuhusu matibabu yangu hasa kuhusu matibabu nje ya nchi, ulijibu kwamba wakili wa Serikali alikuwa sahihi nusu na sio sahihi nusu, Fafanua
Heche: Kuna mazingira ambayo Mbunge anaweza asifuate utaratibu wa kawaida, mfano mazingira kama ya dharula.
Mhe. Lissu: Uliulizwa ni lazima Mbunge mpaka apate referral kwenda nje ya nchi? Ukasema sio lazima apate refferal
Heche: Mbunge akiwa mahututi sio lazima apewe referral
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji muda umeisha hivi sasa ni saa kumi na moja tunaomba ahirisho hadi kesho saa tatu kamili asubuhi.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji huyu John Heche ndio shahidi wangu wa mwisho kwa ambao ni raia, Kwahiyo kesho tutamaliza sio zaidi ya lisaa kwahiyo naomba kesho mashahidi wengine kesho waje ili niongee nao kujua namna tunavyoenda na ushahidi uliobaki.
Watu kicheko😂😂😂😂😂😂
Jaji Ndunguru: Shauri linaahirishwa hadi kesho saa tatu kamili asubuhi, shahidi bado hujamaliza kutoa ushahidi wako.
Imepigwa High Cooooouuuuuurrrrrtttt
Majaji wanatoka
Tukutane kesho saa tatu kamili asubuhi✌️
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 427
Mhe. Lissu ameanza kumfanyia Re- examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa uko tayari? Na tunaamini utakuwa na maswali machache.
Mhe. Lissu: Niko tayari Waheshimiwa majaji ila inategemea na speed ya nyie kuandika pia maana mimi ndo niko Gerezani kule sio Sheraton hotel Waheshimiwa majaji.???
Jaji Ndunguru: Bado una mashahidi watatu tutamaliza within time mshtakiwa maana tulitegemea Ijumaa mngewasilisha final submissions
Mhe.Lissu: Kwanza hao mashahidi wangu nahitaji kuonana nao ili tupange mkakati wa kesi yetu.
Watu wamecheka sana mpaka Majaji, kuhusu Mkakati wa Lissu na mashahidi wake yaani IGP Wambura, CDF Mkunda, na DCI Kingai.😂😂😂
Tunaendelea na Re Examination
Mhe. Lissu: Wakili Mwinuka alikuuliza yale matatizo yanayohusiana na fomu ulisema hukupata shida ya kuambiwa ulijaza fomu vibaya ila ulisema ujazaji fomu ni moja ya kigezo.
Heche: Ni kweli nilisema suala la ujazaji fomu ni sehem ya matatizo ya uchaguzi yanayotumika kuengua wagombea hasa wa upinzani kuna wakati mtu anaambiwa CDM badala ya CHADEMA.
Wakili wa Serikali Mwinuka: Jibu la shahidi lina attract sisi kuja kufanya cross examination yeye atoe tu clarification
Mhe. Lissu: Fafanua bila kutoa mifano
Heche: Kuna vigezo vingine vingi ambavyo vinatumika kuengua wagombea na vinatumika kwa wagombea wa upinzani tu hasa Chadema.
Mhe. Lissu: Umejibu vizuri
Mhe. Lissu: Uliulizwa kuwa kwavile wewe hukuenguliwa na ulishinda, ukaulizwa kwa vile ulishinda badi Uchaguzi ulikuwa huru na wa haki.
Heche: Uchaguzi niliochaguliwa haukuwa huru na haki kwasababu kuna watu waliouwawa.
Wakili Mwinuka: Waheshimiwa majaji hii kwasababu watu waliuwawa ina attract nafasi ya sisi kufanya cross.
Mhe. Lissu: Hilo hapana Wakili wa serikali hayuko sawa sawa, shahidi katika ushahidi wake aliulizwa kuhusu mauaji na alisema alishuhudia wakati wa kampeni kulikuwa na mauji Nyamongo na alishuhudia
Jaji Ndunguru: Endelea Heche
Heche: Waheshimiwa Majaji kampeni zetu ziliingiliwa na Polisi, watu waliuwawa lakini pia hata Mawakala wetu walienguliwa.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Makamu wa Rais alikuja wakati nikiwa Nairobi Hospital ulisema alikuja na alikuwa kwenye mkutano.
Heche: Ni kweli Makamu wa Rais alipoenda Nairobi kwenye kikao na baada ya kumaliza kikao ndo alienda kumuona Lissu Hospital.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kama nilikupa jukumu la kufuatilia mafao yangu ya Hospital ulijibu sikukupa jukumu ila ulikuwa kwenye Kamati ya Chama ya matibabu yangu, fafanua.
Heche: Mhe. Lissu aliposhambuliwa iliundwa kamati na Chama na mimi nilikuwa sehemu ya kamati ya kufuatilia na hakulipwa.
Mhe. Lissu: Uliulizwa kama Chadema mlikuwa na imani na Tume ya Chande, ulijibu hamkuiamini na tuliamini itaficha mauji na kulinda waliouwa.
Heche: Ni kweli hatukuwa na imani kutokana na jinsi ilivyoundwa kwahiyo tuliamini ingeficha ukweli wa kilichotokea na kusafisha watu waliohusika.
Mhe. Lissu: Shahidi wakili Katuga alikuuliza kuhusu Tone tone na michango ya chama uliyopokea, ulijibu suala la michango ya chama sio la Makamu Mwenyekiti, fafanua.
Heche: Suala la michango yote ya chama linasimamiwa na Katibu Mkuu ambaye ni accounting officer na linapita kwenye account rasmi za kichama, haiwezekani kwa vyovyote vile Makamu Mwenyekiti akahusika na michango ya chama.
Mhe. Lissu: Kwenye masuala hayo hayo ya pesa za michango uliulizwa kuhusu Salman na Nilesh, na uliambiwa kwenye account yako umekewa M10 na 20M, ulisema huwajui.
Katuga: Jibu lilikuwa siwajua kuna ufafanuzi gani? Sisi tunapinga kuanzia swali kwasababu jibu litaleta majibu mapya.
Mhe. Lissu: Wakili wa Serikali anapaswa kujua kuwa kabla ya shahidi hajajibu hapaswi kutabiri jibu. Hoja ni kwamba suala la 10M na 20M lilikuwepo hivyo lazima liwe re examined.
Jaji Ndunguru: Haya shahidi fafanua
Heche: Siwajua na sijawahi kuwaona.
Part 428 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 426
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche
Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni anaitwa Ishengoma?
Heche: Tuna kata zaidi ya 4,000 kwahiyo siwezi kujua
Katuga: Unajua kuwa huyu Katibu wa Chadema, Ishengoma alisema kuwa mlishiriki vurugu za Oktoba 29?
Heche: Sijui
Katuga: Ni sahihi Lissu asingealikwa kwenye mkutano wa Tarehe 03/04/2025 asingeongea?
Heche: Sijui
Katuga: Unajua maana ya constructive publication?
Heche: Sijui
Katuga: wewe ni shahidi wa nini kama kila kitu hujui?
Heche: Shida unakuja na majibu yako ya uongo.
Katuga: Ni sahihi ulitaja ripoti nyingi za nje kuhusu uchaguzi wa mwaka jana?
Heche: Sahihi
Katuga: Unajua kuwa opinion ya EU sio binding kwenye mahakama hii?
Heche: Najua
Katuga: Ulieleza kuwa umezilete hizo ripoti hapa mahakamani?
Heche: Sikueleza
Katuga: Njia ipi ulitumia kubadilisha jina kutoka Wegesa Charles Heche kwenda John Wegesa Heche
Heche: Kiapo na Deedpoll na zilitangazwa kwenye gazeti la Serikali
Katuga: Ni ushahidi wako kuwa kwenye kubadilisha jina ulitangaza kwenye gazeti la Serikali?
Heche: Ndio utaratibu
Katuga: Ila wito wa Tume ya Chande hukuona kwenye gazeti la Serikali
Heche: Kwani mimi naona magazeti yote ya serikali? ndio sikuliona hilo tangazo.
Katuga: Nilikusikia uliirejea taarifa ya Thabo Mbeki Foundation
Heche: Ni sahihi
Katuga: Unajua ama hujui kuwa sio Foundation ya kimataifa?
Heche: Mi najua ya kimataifa.
Katuga: Iko chini ya umoja gani wa kimataifa?
Heche: Mi najua ni ya kimataifa.
Katuga: Mwalimu Nyerere Foundation iko chini ya kimataifa?
Heche: Sijui.
Katuga: Unajua au hujui kama walichokitoa foundation ni maoni?
Heche: Ni maoni yao.
Katuga: Unajua au hujui kuwa Thabo Mbeki Foundation walichukua maoni kutoka UN na SADC?
Heche: Najua walichukua AU na SADC sio UN
Katuga: Unajua Thabo Mbeki hawakuwa waangalizi wa uchaguzi?
Heche: Nalijua hilo
Katuga: Kwa vile umesema ya Thabo Mbeki ni maoni, Je mahakama inapokea ushahidi wa maoni?
Heche: Sijui
Katuga: Waheshimiwa majaji naona mimi niishie hapa.
Sasa ni zamu ya Tundu Lissu kuuliza maswali ya Re Examination.
Part 427 itaendelea kwenye post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 425
Upande wa Jamhuri wanaendelea kumfanyia cross examination Makam Mwenyekiti Bara John Heche
Katuga: Waambie Majaji kuhusu kama Chadema mlikuwa tayari kutoa ushirikiano kwenye Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Oktoba 29..?
Heche: Hatukuwa tayari kwasababu hatukualikwa
Katuga: Ni ushahidi wako kuwa hamkuikubali Tume ya Jaji Chande?
Heche: Ndio
Katuga: Kwa jibu lako kuwa hamkuwa mmeikubali Tume ya Chande nitakuwa sahihi nikisema hamkuwa tayari kuipa ushirikiano?
Heche: Sijui.
Katuga: Kwa jibu lako, ni kweli ulikuwa hujui kama Chadema mlikuwa tayari au hamkuwa tayari kutoa ushirikiano?
Heche: Ni kweli
Katuga: Ulipata wapi mamlaka ya kumjibu mshtakiwa kuwa Tume ya Chande haikuwaita?
Heche: Ni kweli haikutuita.
Katuga: Mihimili ya dola ni ipi?
Heche: Bunge, Serikali na Mahakama
Katuga: Unajua ni jukumu la serikali kusimamia sheria..?
Heche: Najua
Katuga: Unajua ni Serikali ndio ina jukumu la kumshtaki mtu yeyote aliyevunja sheria?
Heche: Ni sahihi
Katuga: Unajua Jukumu la kulinda amani limekuwa vested kwa Serikali…?
Heche: Najua
Katuga: Waambie Majaji kama unajua ama hujui kuchoma kitu cha mpira unakifanya kitoe harufu???
Heche: Inategemea kitu chenye harufu kitatoa harufu kama hakina harufu hakitoi harufu
Katuga: Waambie Majaji kuchoma matairi yanafanya yatoe harufu?
Heche: Sijawahi kuchoma matairi kwahiyo sijui.
Katuga: Unajua au hujui kuna njia nyingi za kukifanya kitu kinuke au kukinukisha?
Heche: Sijui
Katuga: Unajua moja ya njia ya kukifanya kitu kinuke ni kukichoma???
Heche: Sijui
Katuga: Nilikusikia ukisema kuwa ulimsikia P17 yeye ndio alichapisha hotuba ya 3/4/2025.??
Heche: Niliskia
Katuga: Ulimsikia akisema kupitia wewe sisi tumechapisha?
Heche: Sikumsikia
Katuga: Unakumbuka au Hukumbuki kuwa P3 (PW13) alisema yeye alipanga kuzuia uchaguzi kwa kurusha mawe.
Heche: Sikumbuki
Katuga: Unapotisha kuvunja amani unakuwa unamtisha nani?
Heche: Sijui.
Katuga: Ulieleza kuwa kwenye hotuba ya Jaji Chande hakuna majina ya watu waliouwawa au waliokufa
Heche: Ndio
Katuga: Uliisoma hotuba ya jaji Chande?
Heche: Ndio niliisoma.
Katuga: Unajua au hujui taarifa rasmi ya jaji Chande ilikabidhiwa kwa Rais.
Heche: Najua alisema anamkabidhi na alisema ni ya kwake.
Katuga: Ushahidi wako ni kwa mujibu wa hotuba au taarifa rasmi?
Heche: Unatokana na hotuba na taarifa ile aliyoisoma.
Katuga: Unajua au hujui Chadema kupitia kwa Katibu Mkuu John Mnyika kilialikwa na kilishiriki kutoa maoni kuhusiana na mabadiliko ya sheria za uchaguzi
Heche: Najua.
Katuga: Unajua au hujui kuwa Kati ya mapendekezo ya Chadema ya kutowashirikisha watumishi wa umma kwenye uchaguzi kulipelekea Mabadiliko ya kifungu cha 6 cha Sheria ya Uchaguzi
Heche: Hayo sio mapendekezo yetu, mapendekezo yetu yalikuwa juu ya mfumo mzima.
Katuga: Unajua au hujui kwamba mwaka 2024 kifungu cha 6 cha Sheria kilibadilishwa na kuondoa wakurugenzi kusimamia uchaguzi?
Heche: Najua kilibadilishwa na kusema watumishi waandamizi ndio watasimamia uchaguzi.
Katuga: Waambie Majaji kama uliiambia Mahakama hii kuwa tarehe 29 Oktoba 2025 ulikuwa mahabusu Mtumba.
Heche: Ndio nilikuwa mahabusu.
Katuga: Ulisema ulipotoka mahabusu uliambiwa na watu kuhusu vurugu zilizotokea na hotuba ya Chande?
Heche: Sahihi
Katuga: Huu ni ushahidi wako au kwa mujibu wa hotuba ya Chande?
Heche: Hotuba ya chande
Katuga: Ni sahihi ulisema kuwa kipindi hicho ndio watu wengi waliuwawa?
Heche: Ni kweli
Katuga: Ni sahihi kuwa mali zenye thamani nyingi zilichomwa?
Heche: Sikumbuki ila alisema zina thamani fulani.
Katuga: Ni sahihi kuwa mali nyingi sana ziliharibiwa?
Heche: Sina ufahamu
Katuga: Unajua kuwa 70% ya waliokamatwa baada ya vurugu za Oktoba 29, 2025 alisema kuwa walichocheka na hotuba zenu?
Heche: Sijui wewe ndio unaniambia
Katuga: Unamjua Katibu wa Chadema kata ya Mikocheni?
Heche: Simjui
Part 426 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako