Kwa muda wa miaka minne sasa nimekuwa nikifanya utafiti wa kibiashara ya kuku wa kienyeji hapa UK, kwani moja ya kazi ninayoipenda ni ufugani wa Kuku. Kuna kipindi nilimualika ANKALI @MalemboLE Zanzibar aje anipe ushauri juu ya suala la ufugaji. Na bado mimi nae tuna ‘Unfinish Project’
Andas yangu kwenye mradi huu ni kufuga kuku wa kienyeji ambao ni “wachache sana” kwenye upatikanaji wake! Na wa aina ya kipekee.
Mmoja mbegu za kuku ambao ningependa kufuga ni:
1. Ayam Cemani, Indonesia
•Bei: Hadi £2,000 kwa kuku mmoja
•Sababu ya kuwa ghali: Kuku huyu ni mweusi kabisa, manyoya, ngozi, macho, hadi kwenye viungo vya ndani, kutokana na hali ya kinasaba inayoitwa fibromelanosis. Huaminika kuwa na nguvu za kimiujiza katika baadhi ya jamii za Indonesia.
2. Dong Tao (Kuku wa Miguu ya dragon) – Vietnam
•Bei: £1,000–£1,500
•Sababu ya kuwa ghali: Ana miguu mikubwa sana yenye magamba makubwa, kama miguu ya dragon. Alikuwa akitunzwa kwa ajili ya mlo wa kifalme. Ni vigumu sana kumlea na kumzalisha.
3. Kadaknath, India
•Bei: £200–£400 kwa kuku mmoja (bei inaweza kuongezeka kwa waliothibitishwa)
•Sababu ya kuwa ghali: Ana nyama nyeusi kama Ayam Cemani, na anaaminika kuwa na virutubisho vingi – protini nyingi, mafuta kidogo. Ni maarufu sana kwa tiba mbadala na mapishi ya kifahari.
4. Liege Fighter – Ubelgiji
•Bei: £250–£500+
•Sababu ya kuwa ghali: Kuku wa zamani waliotumika kwenye mapigano ya jogoo, lakini sasa wanatunzwa kwa ajili ya uhifadhi. Wana mwili mkubwa wenye misuli na sura ya kupendeza.
Hawa ni baadhi tu ya mbegu za kuku wa kienyeji ambao ni ghali kununua na kuwatunza pia.
Utajiri kama ilivyo uongozi ni dhima ambayo inaambatana na wajibu wa kugusa maisha ya wasionacho, wenye uhitaji, na wale ambao rizki zao zinapitishiwa mikononi mwa aliyebarikiwa utajiri. Tajiri ni wakala wa Mwenyezi Mungu wa kusimamia na kusambaza rizki kwa waja wake.