@frank_matondane@Dr_Thadeus_19 Networking ya bank kwasasa haiitaji matawi kila kijiji cha Tanzania, mawakala ndiyo wanapaswa wapeleke huduma za benki katika kila kijiji cha Tanzania. Ni wajibu wa wizara ya fedha kuja na mikakati rafiki kwa wafanyabiashara za uwakala ili waweze kusambaza huduma hizo vijijini.
@ngwalenjekileti@Dr_Thadeus_19 Naongea kwa uzoefu ndugu yangu, nimeanza kuitumia wakati nafanya kazi ya sales. Niligeuza kama kibubu changu, kila commission niliyokuwa napata kwa juhudi za ziada nilikuwa naweka hapo, na wakawa hawakati. Baada ya mwaka, nilipata mtaji wa biashara yangu binafsi bila mkopo.
@Sativa255 CHAMA kina hitaji watu wengi zaidi, sidhani kama kinapaswa kuchagua wanachama. Ila wanachama wanahaki ya kuchagua viongozi, kwahiyo siku Msigwa akitaka nafasi ya uongozi, wanachama wake wanahaki ya kumkataa. Hiyo ndiyo Demokrasia ya kweli. CHADEMA inapaswa ipokee wanaorudi.
@zoetjesheeftX Nilinunua tshirt yenye picha ya Martin Luther π, kwenda kuiweka kwenye maji, rangi yote ikapotea. Nililia sana, hafu nilikuwa kijana mdogo, pesa yangu changama, nilijinyima ili nipendeze hafu ikanitokea puani. Sema nilinunua tshs. 200 kwa wakati huo.