Imamu wa kwanza duniani aliyejitangaza hadharani kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja, Muhsin Hendricks (57), ameuawa kwa kupigwa risasi nchini Afrika Kusini huku ripoti zikisema ameuawa baada ya kufungisha ndoa ya Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.
Imamu huyo alikuwa anaongoza Msikiti mmoja JijiniCape Town uliolenga kuwa mahali salama na kimbilio kwa Waumoni wa kiislamu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na wale waliotengwa na jamii ambapo alipigwa risasi Jumamosi asubuhi baada ya gari alilokuwa akisafiria karibu na jiji la kusini la Gqeberha kushambuliwa.
Polisi wamesema βWashukiwa wawili wasiojulikana wakiwa wamefunika nyuso zao walitoka kwenye gari nyingine na kuanza kulimiminia risasi nyingi gari hiloβ
Habari za kifo cha Hendricks zimeleta mshtuko mkubwa katika jamii ya Watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (LGBTQ+ ) na kwingineko, huku kukitolewa salamu nyingi za rambirambi kutoka sehemu mbalimbali za dunia.
Taarifa za tukio hilo zimeonekana kupitia video za CCTV zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii ambapo video hiyo inaonesha gari likisimama na kuziba njia ya gari alilokuwamo Hendricks kabla ya kuanza kushambuliwa.
#MillardAyoUPDATES
Kwa dhati kabisa, NAMPONGEZA Mheshimiwa Askofu JOSEPHAT GWAJIMA, Mbunge wa Kawe, kwa UZALENDO wake wa KUMFUFUA MTOTO kanisani. Namuomba sasa, UFUFUO, USIISHIE KANISANI TU, bali UENDE MPAKA MOCHWARI. Watanzania WAMECHOKA KUFA.
Kitendo cha kuaga kwa kumbatiana kihisia kwa muda mrefu wakati wa safari ni jambo la kawaida kwa Watu na Watu wao katika Viwanja mbalimbali vya Ndege duniani lakini Wasafiri watakaokua wakitumia Uwanja wa Ndege wa Dunedin Nchini New Zealand wamepewa onyo kuwa sasa watalazimika kukumbatiana harakaharaka kwa dakika zisizozidi tatu katika eneo la Uwanja wa Ndege.
Mamlaka za Uwanja huo zimeweka sheria ya kikomo kipya cha dakika tatu pekee na kubandika mabango nje ya Uwanja huo ili kuzuia Wasafiri kubembelezana na kukumbatiana kwa muda mrefu na kusababisha msongamano wa magari.
βKukumbatiana kwa sekunde 20 ni muda mrefu wa kutosha kutoa homoni za ustawi wa oxytocin na serotoninβ Mmoja wa Wasimamizi wa uwanja huo amenukuliwa na Vyombo vya Habari na kuongeza kuwa wamefanya dakika tatu baada ya kushutumiwa kukiuka haki za kimsingi za Binadamu.
#MillardAyoUPDATES
Nafahamu, hupendi kusoma ila Ukiisoma post hii hadi mwisho, utagundua mambo 10 muhimu kuhusu Baba wa Taifa yatakayokutia moyo na kukuinua kifikra. π
10 Facts Kumhusu Mwalimu Julius Nyerere πΉπΏ
1οΈβ£ Mwasisi wa Taifa:
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Rais wa Kwanza wa Tanganyika (1961) na baadaye Tanzania (1964), baada ya kuungana kwa Tanganyika na Zanzibar.
2οΈβ£ Alipewa Jina la "Mwalimu":
Alikuwa mwalimu wa shule ya msingi kabla ya kuingia kwenye siasa, na jina lake la βMwalimuβ lilitokana na kazi hiyo aliyopenda.
3οΈβ£ Kiongozi wa Ujamaa:
Nyerere aliunda sera ya Ujamaa na Kujitegemea mwaka 1967, akilenga kuleta usawa wa kijamii kupitia kilimo na kujenga uchumi wa taifa kwa msingi wa kijamaa.
4οΈβ£ Aliamini Katika Elimu kwa Wote:
Mwalimu Nyerere aliamini kuwa elimu ni ufunguo wa maendeleo, na alianzisha sera ya elimu bure kwa watoto wote wa Tanzania.
5οΈβ£ Mwanamapinduzi wa Afrika:
Nyerere alikuwa miongoni mwa viongozi waliounga mkono harakati za ukombozi wa Afrika, akishirikiana na viongozi wa nchi mbalimbali katika harakati za kumaliza ukoloni barani Afrika.
6οΈβ£ Alifanikisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar:
Mnamo mwaka 1964, Nyerere aliongoza muungano wa Tanganyika na Zanzibar, na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muungano wa kipekee barani Afrika.
7οΈβ£ Amani na Utulivu:
Chini ya uongozi wa Nyerere, Tanzania imejipatia sifa ya kuwa taifa la amani na utulivu, ambalo halikuwahi kuwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe.
8οΈβ£ Alistaafu Kwa Hiari:
Nyerere alikuwa mmoja wa viongozi wachache wa Afrika ambao walistaafu kwa hiari mwaka 1985, akiweka mfano wa demokrasia na mabadiliko ya uongozi barani Afrika.
9οΈβ£ Mwanadiplomasia wa Kimataifa:
Mwalimu Nyerere alikuwa na sifa kubwa kimataifa kwa uwezo wake wa kuongoza majadiliano ya amani, hususan katika migogoro ya Afrika. Alisaidia katika kutafuta amani kwa nchi kama Msumbiji, Uganda, na Rwanda.
π Anakumbukwa kwa Mchango Wake:
Mwalimu Nyerere anaheshimiwa ndani na nje ya Tanzania kwa maono yake, upendo wake kwa watu, na falsafa zake za usawa, haki, na maendeleo kwa wote.
πΉπΏ Mungu Ibariki Tanzania, Mungu Ibariki Afrika, Mungu Ibariki Urithi wa Mwalimu Nyerere!
#HappyNyerereDay
#VIDEO Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA- Bara Tundu Lissu amesema Vijana wawili waliompiga risasi aliwatambua na anafahamu kuwa wapo licha ya kwamba wanahisi hawajulikani lakini muda ukifika atawataja.
Akiongea na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam leo September 25,2024, Lissu ameelezea pia masikitiko yake kwakuwa Serikal bado haijamlipa hela yake ya matibabu.
βKatika Watu wanaotakiwa kuchunguzwa kijinai kuhusu tuhuma yangu ni Paul Makonda, kuna mengine nitayasema baadaye hata walionipiga risasi wale Vijana wawili bado wapo, wanajiita hawajulikani wapo, muda wake ukifika tutawataja labda waende walipo wakawanyongeβ βββ Tundu Lissu. #MillardAyoUPDATES
44 days.
Thatβs all the time we have left until Election Day.
@KamalaHarris has the vision, strength, and compassion to lead this country forward. Make your voice heardβmake a plan to vote early, vote by mail, or head to the polls. https://t.co/bBcatjmEym
Mkuu wa Majeshi (CDF) wa Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ambaye pia ni Mtoto wa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amesema amesitisha mpango wake wa kugombea Urais Nchini humo katika Uchaguzi ujao wa mwaka 2026 na badala yake ametangaza kumuunga mkono Baba yake Rais Museveni kuwa ndiye anastahili kuendelea kuwa Rais wa Nchi hiyo kwa muhula wa saba mfululizo.
Muhoozi amesema βNatangaza kuwa sitogombea Urais 2026, Mungu ameniambia niweke nguvu kwenye Jeshi lake kwanza, namuunga mkono Rais Museveni kwenye Uchaguzi ujao, kwangu hakuna kitu kitakatifu zaidi Duniani kushinda Jeshi la Uganda, siwezi kufikiria heshima nyingine zaidi ya heshima ya kuwa ndani ya Jeshi la Uganda, Mungu libaliki Jeshi letu na uitakase Uganda mileleβ
Katika hatua nyingine Muhoozi amesema βHakuna Raia wa kawaida ataiongoza Uganda baada ya Rais Museveni kumaliza muda wake, Vyombo vya Usalama havitokubali hilo, Rais ajaye wa Uganda atakuwa Mwanajeshi au Polisiβ
Itakumbukwa March 16,2023 Muhoozi alitangaza nia ya kutaka kumrithi Baba yake kiti cha Urais wa Uganda ambapo alisema atagombea Urais mwaka 2026 huku akisema inatosha sasa kuendelea kuongozwa na Wazee lakini siku chache baadaye Baba yake Rais Museveni akamjibu akisema Wananchi wa Uganda wataamua kama Mtoto wake Muhoozi anafaa kuwa Rais wa Nchi hiyo muda utakapofika ama laah na akaongeza kuwa Viongozi wa Uganda hawachaguliwi Twitter.
Kwa sasa Museveni anaiongoza Uganda kwa muhula wa sita mfululizo, hii ni baada ya kushinda uchaguzi wa January 14, 2021 kwa kuwashinda Wagombea wengine 10 katika nafasi ya Urais (akiwemo Robet Kyaluganyi maarufu Bobi Wine) kwa ushindi wa 58% na endapo atagombea tena mwaka 2026 itakuwa ni muhula wake wa saba mfululizo.
#MillardAyoUPDATES
Ubaya ni kwamba wengi wanaamini kuwa mtu anabakwa tu na watu wasiojuana. Wengi sana. Mara nyingi mtu anabakwa na mtu wa karibu sana na inamfedhehesha balaa sababu akisema anaonekana muongo ila akinyamaza pia anakuwa na maumivu ya moyo na hasira.
Kwa kifupi hajui wapi pa kulisema la moyoni ambapo anajua wazi watalisimamia kwa uzito wa maumivu yake. Kama ni mdogo ndo kabisa tunasema hili wakalimalize kama familia. Sasa tunatengeneza jamii ya watu wenye hasira kali sana kwa yaliyowakuta maishani.
Kauli mbaya kuliko zote ambayo jamii tunasema sana kwa aliyebakwa βSasa wewe kwanini ulienda kwake? Nyie mnajuanaβ.