Kwa wale ambao hamjui kwanini huyu MALAYA tunamuita "BIMSUMI" sikiliza HAPA.
HUYU kakataliwa DUNIANI, MNINGUNI NA KUZIMU. Huyu Maiti yake yake hata BAHARI itaikataa.
"Kwanini hayo mabomu yametupwa ndani ya eneo la kanisa la Jimbo Kuu Katoliki Musoma? waliotupiwa ni hawa kina mama ila walioathiriki si hawa kina mama tu, kulikuwa na watoto wadogo, mabibi na wazee wanatoka kanisani na wengine wanaingia misa ya pili." Askofu Michael Msonganzila
KANISA KATOLIKI linakemea uovu mbele ya dunia bila kujali WAKOLONI WEUSI WATAPENDA AU LAAH.
Hili kanisa linaongozwa na watu WASOMI na wenye akili timamu ndiomaana hata wakiongea wanaongea vitu ambavyo vinaingia akilini.
Leo hii MWAMPOSA zee la wese linaweza kuongea hivi dhidi ya WAKOLONI WEUSI?
Asante kanisa kuwa upande wa HAKI SIKU ZOTE.
MARA: Askofu wa Jimbo Katoliki la Musoma, Michael Msonganzila, amesema hayo Jumanne Machi 10, 2026, wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini Musoma kuhusu tukio la Jeshi la Polisi kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wanachama, wafuasi na viongozi wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA (BAWACHA) katika eneo la Kanisa Kuu la Jimbo hilo siku ya Machi 8, 2026.
Soma zaidi https://t.co/7NQ3H9PYtk
#JamiiForums #Utawala #Uwajibikaji #JFMatukio
Tuna linchi la kipumbavu sana aisee. 😁
Hawa waandishi wanapelekeshwa sana. Hakuna tena ubunifu kwenye hii sekta ni kama KUSANYIKO LA MAZOMBIE TUU.
Msikilize muandishi Pascal Mayala ambae ameshtakiwa na SERIKALI HARAMU YA DIKTETA JIKE.
Ila madelu kamaindi kuambiwa anavaa vaa maskafu na hapendwi🤣🤣
Mvutano wa kijeshi katika eneo la Ghuba ya Uajemi umeongezeka kufuatia taarifa za mashambulizi ya makombora na ndege zisizo na rubani yanayodaiwa kufanywa na Iran dhidi ya Saudi Arabia.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kimataifa, makombora kadhaa yalirushwa kuelekea maeneo ya kimkakati, yakiwemo mji mkuu wa Riyadh na ukanda wa mashariki wa nchi hiyo.
Hata hivyo, mamlaka za Saudi Arabia zimesema mifumo yao ya ulinzi wa anga ilifanikiwa kuyadhibiti na kuyatungua makombora hayo kabla hayajasababisha madhara makubwa.
Serikali ya Saudi Arabia imelaani vikali tukio hilo, ikilitaja kama ukiukwaji wa sheria za kimataifa na tishio kwa usalama wa eneo zima la Ghuba.
Aidha, imeonya kuwa itachukua hatua stahiki kulinda mipaka na raia wake endapo mashambulizi yataendelea.
Mashambulizi hayo yanatajwa kuhusishwa na mvutano mpana wa kisiasa na kijeshi unaoendelea kati ya Iran na mataifa washirika wa Magharibi pamoja na Israel, hali inayoongeza hofu ya kupanuka kwa mzozo katika Mashariki ya Kati.
Jumuiya ya kimataifa inaendelea kutoa wito wa kujizuia na kutafuta suluhisho la kidiplomasia ili kuzuia hali hiyo isigeuke kuwa vita vya wazi vinavyoweza kuathiri uchumi na usalama wa dunia.
“Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo alisikitishwa na matukio ya tarehe 29.10.2025 na kutoa wito wa kuliombea Taifa bila ubaguzi wa dini, chama, kabila au chochote kile.”-; Jude Thadeus Ruwa'ichi,
Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki Dar es salaam,
Napendezwa na jinsi familia ya POLEPOLE ilivyoamua kusimama kidete kupigania HAKI YA MPENDWA wao.
Kama familia zote zilizopoteza wapendwa wao kwa utekaji zingekuwa VOCAL kama hii ya Polepole hakika kuna mahali tungefika kama TAIFA.
TUTAKUWEPO🫵😎
Kijana wa BANJO kaongea kiume sana.
Jana usiku ilitoka taarifa kuwa waliomuuwa Baba yake ni police wakiongozwa na OCCID ARUSHA MAHITA- na ushahidi ukawekwa.
Huyu kijana ataishi maisha yake yote akiwa na hasira kifuani mwake juu ya waliofanya haya kwa baba yake milele.
Tunatengeneza TAIFA lenye CHUKI isiyoisha vifuani mwa vijana wadogo wenye kesho kubwa. Hawa kesho wakija kuandamana msianze kusema ni watu kutoka nje wamelipwa kuja kuandamana.
Malipo ni hapa hapa duniani siku inakuja MTAVUNA MNACHOPANDA.
TUTAKUWEPO🫵😎
Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amefariki dunia usiku wa Februari 19, 2026, wakati akipatiwa matibabu katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI).
Taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Thaddeus S. Ruwa’ichi, imeeleza kuwa mipango ya mazishi itatangazwa baadaye baada ya maandalizi kukamilika.
Jimbo Kuu la Kanisa Katoliki la Dar es salam limetangaza kifo cha Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa jimbo hilo, kilichotokea leo saa 4 usiku akiwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) .
Taarifa iliyotolewa na Askofu Mkuu wa Dar es Salaam, Thaddeus S. Ruwa’ichi, imesema kuwa taarifa za mazishi zitatangazwa baada ya mipango kukamilika. #MillardAyoUPDATES
VIDEO:
Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo @ChademaTZ2 Dkt. Rugemeleza Nshala akiteta jambo na Wakili Brooke Lee Montgomery ndani ya chumba cha Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala ndogo ya Dar es Salaam kabla ya kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Lissu kuanza leo Februari 19, 2026.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Stephen Wasira, amepuuza madai kuwa Tume ya Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman inaweza kuwa na upendeleo kwa Serikali, akifafanua kuwa lengo la tume hiyo si "kuichunguza serikali" bali ni kuchimbua chanzo cha ghasia zilizotokea wakati na baada ya uchaguzi wa Oktoba 2025.
Katika mahojiano na gazeti Mwananchi, Wasira amewatetea wajumbe wa tume hiyo, akisema viapo vyao vya utumishi havikuwahi kuwa na utiifu kwa Rais bali kwa Jamhuri na Katiba.
“Hao wanaosema hayo maneno, ukiwasikiliza vizuri, wao wanadhani tumeunda tume ya kuichunguza serikali, ile tume haikuundwa ili kuchunguza serikali, ile tume imeundwa ili kuchunguza kilichotokea, chanzo halafu mengine yote ndio yatokanayo”, amesema Wasira.
Akijibu hoja kuhusu uadilifu wa Jaji Chande, Wasira amekumbusha kuwa Jaji huyo anaaminiwa na dunia nzima, akiwahi kuteuliwa na Umoja wa Mataifa (UN) kuchunguza kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa UN, Dag Hammarskjöld. Ameongeza kuwa hata kama Rais ndiye aliyewateua, majaji wastaafu ni watu huru ambao hawaajiriwi tena na serikali na hawawezi kupewa maelekezo ya namna ya kuandika ripoti.
Wasira ameeleza kusikitishwa kwake na vifo vilivyotokea, akisema kuwa haki namba moja ya binadamu ni haki ya kuishi, na ghasia zinapotokea, haki hiyo inapotea. Amesisitiza kuwa kilichotokea mtaani kilikuwa ni uhalifu uliopangwa na si maandamano ya kawaida ya kisiasa.
Hata hivyo, amesisitiza kuwa lazima kuwe na uwajibikaji si kwa serikali tu, bali kwa viongozi na makundi yaliyowaingiza vijana mtaani kufanya uharibifu.
“Uwajibikaji katika jambo hili haiwezi kuwa mikononi mwa serikali pekee yake, ni pamoja na wale walio-organize maana huwezi kulimaliza bila kujua lakini hawa watoto hawa waliingia mtaani, waliingizwa na nani? Hivi hao wenyewe hawawajibiki? Waliowaingiza? nani aliwaingiza? Maana hawawezi kuzuka tu wakaingia mtaani wakafanya uharibifu walioufanya”, ameeleza Wasira.