Captain Ibrahim Traoré, scored a hat-trick to give the Presidency victory against former African Stars. Full time: 8-2! 🚨🇧🇫
#africanfootball#burkinafaso
Mkuki Kwa Ngurue Mtamu Ehee.
Baada ya serikali ya Afrika Kusini kupiga marufuku shughuli za kampuni ya Elon Musk, Starlink, kutokana na kutokidhi vigezo vya leseni za umiliki wa hisa, Elon Musk amejibu kwa ukali.
Thread: ⤵️
"NILIMKATA LUMUMBA VIPANDE 34"
Katika giza la usiku wa Afrika, kikundi cha wanajeshi wa Kibelgiji walikuwa wakifanya kazi ambayo hata shetani mwenyewe angehofia kushuhudia.
Wakiwa wamelewa, wakicheka kwa kejeli huku harufu ya damu ikiwaangukia mashavuni mwao, walikuwa wakifanya kazi moja tu!.
Kuufuta kabisa mwili wa Patrice Émery Lumumba kutoka katika uso wa dunia.
Na mmoja wao, Gérard Soete, hakuficha jambo hilo. Miaka 40 baadaye, kwa sauti tulivu lakini ya kushtusha, aliwaambia waandishi wa habari wa Ubelgiji.
“Niliukata mwili wa Lumumba na kuunguza kwa tindikali. Katikati ya usiku wa manane, tulianza kwa kulewa ili kupata ujasiri.
Sehemu ngumu zaidi ilikuwa kuukata vipande vipande kwa msumeno kabla ya kuweka kwenye asidi.
Hakukuwa na chochote kilichobaki, ni meno machache tu. Nilioga mara tatu na kila wakati nilijiona mchafu.”
Kwa mara ya kwanza, dunia ikasikia kwa undani unyama wa kihistoria uliokuwa umefichwa kwa miongo minne.