Habari 👋 Naitwa Alex,mfugaji wa nguruwe.
Ukurasa huu ni kwa ajili ya kushirikiana mbinu rahisi, changamoto na faida za ufugaji wa Nguruwe 🐷
Kama ni mfugaji mchanga au unafikiria kuanza, basi hii ndiyo sehemu sahihi.
Karibu tuanze safari hii pamoja! 🌱"
#UfugajiWaNguruwe#
🌱Dalili za Shida ya Upumuaji kwa Nguruwe
1)Kukohoa/kupiga chafya
2)Kupumua kwa shida au haraka
3) Homa
4)Uchovu na kukosa hamu ya kula
Chukua hatua mapema,wasiliana na daktari wa mifugo.
#UfugajiWaNguruwe#
🌱Ni Rahisi Sana Kuzuia Magonjwa
📌Usisubiri kuona dalili,zingatia chanjo kukinga magonjwa
📌Usiazime vifaa vya shambani kutoka au kwenda shamba jirani
📌Ikitokea mnyama amekufa,mzike au mchome kwa moto
📌Watenge nguruwe wapya angalau kwa siku 10
#UfugajiWaNguruwe#
PS:Kwa kuangalia aina, ukubwa na uchakavu wa meno, unaweza kujua kwa urahisi kama nguruwe ni mchanga, kijana, mzima au mzee.
Ukijua meno, unaujua umri! 🐖🦷
📌Endelea kuwa karibu na ukurasa huu kwa kulike,kushare,kukoment na kutufollow
#UfugajiWaNguruwe#
📌Kujua umri wa nguruwe ni jambo muhimu kwa mfugaji yeyote
📌Moja ya njia rahisi ya kutambua umri wa nguruwe ni kuangalia meno yake. Meno ya nguruwe hubadilika hatua kwa hatua kadri anavyokua, na kila hatua huacha ishara inayoonekana
👉Meno husaidia kutambuakama ifuatavyo
🧵👇
4)Nguruwe mzee(miaka 5 na zaidi)
-Meno ya chonge huwa marefu sana na yamepinda
-meno ya mbele na meno mengine huchakaa
-Meno huwa ya njano au kuvunjika
3)Nguruwe mkubwa(miaka 2-4)
-Wana meno ya kudumu ambayo ni imara sana
-Meno ya chonge huanza kukua na kupinda
-Meno ya mbele na meno mengine huanza kuchakaa sababu ya kula
Kuepuka Magonjwa ya Nguruwe
📌Badili viatu/nguo unapoingia na kutoka kwenye shamba
📌Nyunyiza dawa ya kuua vimelea kwenye vifaa mara kwa mara
📌Zuia wageni wasiokuwa lazima kuingia ndani
📌Tenga wanyama wapya kabla ya kuwaunganisha na kundi
📌Dumisha usafi wa mabanda kila siku
Vitamini Muhimu kwa Nguruwe Kabla na Baada ya Kuzaa 🐖
1)Kabla ya kuzaa
🌱A,Dna E-kuimarisha ngozi,mifupa na kinga za mwili
🌱B complex-kuimarisha shughuli za kubadilisha chakula kuwa nishati
🌱Selenium na madini chuma
2)Baada ya kuzaa
🌱B complex
🌱Vitamin C
🌱Makosa Ya Kuepuka Wakati Wa Kutoa Chanjo
1)Kutumia chanjo iliyoharibika
2)Kutoweka chanjo kwenye barafu
3)Kurudia kutumia sindano chafu
4)Kutoa dozi isiyo sahihi
5)Kutokurudia chanjo muda unaotakiwa
6)Kutoa chanjo kwa nguruwe mgonjwa
7)Kumshika nguruwe vibaya wakati wa chanjo
4)Hatua ya nne
📌Muwekee nguruwe uliyempa chanjo alama na urekodi
-Andika namba ya nguruwe,chanjo aliyopewa,dozi na tarehe
👉Endelea kusapoti ukurasa huu kwa kulike,kushare na kufollow ili uendelee kupata dondoo mbalimbali za ufugaji wa nguruwe
#UfugajiWaNguruwe#
3)Hatua ya tatu
📌Chagua njia sahihi ya kuchoma chanjo
👉Kuchoma kwenye misuli(intramuscular)
-Tumia eneo la shingo au paja,choma sindano engo ya 90°
👉Kuchoma chini ya ngozi(subcutanous)
-Tumia ngozi nyuma ya sikio au mkunjo wa shingo,engo 45°
-choma taratibu kupunguza maumivu
2)Hatua ya pili
-Andaa chanjo husika,tikisa chupa
-Soma maelekezo vizuri au uliza kuhusu dozi kwa daktari wa mifugo
-Vuta dozi inayotakiwa kwenye bomba la sindano ie mls 1-2 kwa nguruwe mmoja
1)Hatua ya kwanza
📌Pata vifaa vyako vyote kwaajili ya chanjo
-Sindano,itumike mpya kila baada ya nguruwe watano
-Gloves na dawa ya kuuwa vimelea
-Chanjo iliyowekwa kwenye sanduku la barafu au friji
-Notebook au fomu ya kurekodi taarifa za chanjo
🌱Chanjo Zinazohitajika Kwa Nguruwe
Kama tulivyojadili kwenye andiko lililopita kuwa chanjo ni kama ngao dhidi ya magonjwa.
Hivyo basi tuangalie chanjo za muhimu zinazohitajika kwa nguruwe
🧵👇