Kesho ushindi ni 95% , Hoja za kusema Jimbo la Konde hili twapewa ni Propaganda. Sababu CCM yenyewe inajua kwamba miaka yote hawawezi kushinda Pemba. Na ushindi wa ACT wazalendo kesho ni kwa kura za wananchi sio hisani, sababu hatujawahi tegemea hisani ya mtu yeyote.Abdul Nondo
Niliondolewa Ofisini kinyume na taratibu kwa sababu nilikuwa nasimamia na kufanya kazi kwa kufuata taratibu na miongozo ya kazi na sio maelekezo ya mtu,kuna mahali viongozi wetu wanashindwa kusimamia wanachokiamini kwa hofu ya kuporwa V8, wanahofu kukosa riziki" Prof.Mussa Assad
Matokeo
#Ucl
FT PSG 2-0 Man City
FT RB Leipzig 1-2 Club Bruges
FT Porto 1-5 Liverpool
FT AC Milan 1-2 Atlético
FT Dortmund 1-0 Sporting
FT Real Madrid 1-2 Sheriff
#BM24 NEWS
Kiungo Kinda wa klabu ya Yanga Omary Chibada ameshajiunga na klabu ya Biashara United ya Mara kwa mkopo wa msimu mmoja. Biashara United msimu huu itashiriki kombe la shirikisho barani Afrika (Caf Confederation Cup).
Beki wa kulia wa klabu ya Simba, David Kameta Duchu ameshajiunga na klabu ya Biashara United ya Mara kwa mkopo wa msimu mmoja. Biashara United msimu huu itashiriki kombe la shirikisho Barani Afrika (CAF Confederation Cup).
"Kesho Agosti 25, 2021 klabu kubwa ya @yangasc1935 itakuwa inazindua jezi zake kwa ajili ya msimu wa 2021 /2022. Narudia ni uzinduzi wa jezi bora sio jezi yenye makorokoro, tutazindua jezi tatu zenye ubora" @HajiManara
Ombi langu kwa mamlaka na wanasiasa, japo wanasema siasa ni mchezo mchafu lakini pamoja na uchafu wake msifanye mambo mpaka yakavuka mipaka, sababu watu wa Mungu watainua sauti zao na wale wanaoonewa watainua sauti zao na Mungu hatakaa kimya, atawajibu- Dk. Frederick Shoo
Najua kuna mioyo ya watu inaugua hata kama hawana mahali pa kusemea, inaugua kwa mambo yanayoendelea katika jamii, tunahitaji kufuata amani kwa bidii na ili iwepo haki lazima itendeke- Mkuu wa KKKT, Dk. Frederick Shoo
Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, imepanga tarehe 1 Oktoba 2021, kutoa hukumu ya kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, inayomkabili aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili. Tarehe hiyo imepangwa baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza ushahidi.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amenza ziara ya kikazi nchini Rwanda leo Jumanne ikiwa na lengo la kuimairisha na kuongeza zaidi uhusiano na ushirikiano mzuri ambao umekuwepo kwa muda mrefu kati ya Rwanda na Tanzania.