Watu watafanikiwa upende usipende.
Watu watatajirika uwe unawaunga mkono au la.
Watu watashinda ukiwapigia makofi au la.
Chuki na Wivu wako haucheleweshi baraka zao.
MUNGU sio mjomba wako.
Kama ukiona mtu anapambana anafanikiwa moyo wako unakuuma unachukia, weka mkono wako wa kulia kifuani, tazama juu na jigonge gonge kifuani ukisema
“Ee Mungu mimi ni mchawi naomba niokoe na dhambi hii Baba”.
Good morning hustlers 👊🏾
Ukiwa una shinda Bar, utaanza kuona tabia za kuomba watu pombe ni za kawaida.
Ukiwa una garage utaona tabia za matusi ni kitu cha kawaida.
Ukiwa unashinda vijiweni utaona tabia za umbea na uchonganishi ni kawaida.
MANZINGIRA, MAZINGIRA, MAZINGIRA.
Ukiwa una deal na "Watanzania wa Kawaida" kila siku, ndivyo utajua namna bado tupo nyuma, ukiachana na Ujinga na Umaskini, hatuna character wala identity.
Low quality population.
Ukitaka kuishi na watu vizuri mtaani;
1. Lipa deni lako kabla hujadaiwa.
2. Usilazimishe urafiki
3. Ata kama uko busy kiasi gani hakikisha unapata muda wa kushiriki matukio ya kijamii mtaani kwako( Misiba na N.k)