SERIKALI YABORESHA USAFIRI NA USAFIRISHAJI MAZIWA MAKUU
TANZANIA
Katika kuimarisha huduma za usafiri na usafirishaji majini, hususan katika Maziwa Makuu, Serikali ya Awamu ya Sita imeweka historia ya kuendelea kujenga na kukarabati meli mbalimbali.
Mathalan, katika kuendelea na ujenzi wa meli kwa vitendo, ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza umeendelea na hadi kufikia Machi, 2025 umefikia asilimia 96 kutoka asilimia 40 iliyofikiwa mwezi Machi, 2021 wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia Madarakani.
Mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Mei, 2025. Aidha, meli ya MV. Umoja yenye uwezo wa kubeba kwa wakati mmoja mizigo yenye tani 1,200 ukarabati wake umekamilika na kuanza kutoa huduma, ambapo kwa sasa inafanya safari kwenda nchi za Uganda na Kenya.
Serikali pia imeanza ukarabati wa meli ya kihistoria ya MV. Liemba ambayo hadi kufikia mwezi Machi, 2025 umefikia asilimia 15; ukarabati wa meli ya MT. Sangara umefikia asilimia 98; na ukarabati wa meli ya MT. Ukerewe umefikia asilimia 17.
Picha mbalimbali za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Chief Mkuu, Chief Hangaya Dkt. Samia Suluhu Hassan akishiriki tamasha la utamaduni la Bulabo linalofanyika wilayani Magu mkoani Mwanza.
YALIYOJIRI ZIARA YA RAIS SAMIA SIMIYU
Serikali imetumia TZS bilioni 107.36 kusambaza umeme katika vijiji vyote 474 mkoani Simiyu. Sasa miradi inaendelea kwenye vitongoji 638 kati ya 1,408 vilivyopo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa amekaa kwenye kiti cha Kitemi mara baada ya kutembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitembelea Kituo cha Utamaduni na Makumbusho ya Wasukuma Bujora kujionea shughuli mbalimbali za kabila la Wasukuma, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.
DKT. SAMIA CHIFU HANGAYA AKISHIRIKI TAMASHA LA BULABU
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Chifu Hangaya, ambaye ni Mkuu wa Machifu nchini, akishiriki Tamasha la Kiutamaduni la Bulabu, katika Uwanja wa Bulabu, Kisesa, Magu mkoani Mwanza. Kushoto kwa Mhe. Rais ni Chifu Antonia Tonisizya, Mwenyekiti wa Umoja wa Machifu, Tanzania na kulia kwake ni Chifu Nyamilonda II, Aron Mikomangwa, ambaye ni Katibu wa Machifu.
Mhe.Rais Dkt Samia Suluhu Hassan (Chifu Hangaya) atazindua tamasha la utamaduni la Bulabo (linalofanyika Kila mwaka Kanda ya ziwa Katika Mkoa wa Mwanza) Leo Juni 21,2025 ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya kikazi Mkoani humo.
Tutakuletea matangazo Mubashara kutoka Katika Viwanja vya kisesa Bujora Mwanza.
Kaa tayari kupitia mitandao yetu ya Kijamii Facebook, Instagram,X, TikTok na YouTube
Shamrashamra wakati wa Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Bujora, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akishiriki Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya ziwa, leo tarehe 21 Juni, 2025.
Matukio mbalimbali wakati wa Tamasha la Utamaduni la Bulabo la Kanda ya Ziwa lililofanyika katika uwanja wa Bujora, Kisesa Mkoani Mwanza tarehe 21 Juni, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akipunga bendera kuashiria kuanza kutumika rasmi kwa Daraja la JP Magufuli (Kigongo-Busisi) lenye urefu wa km 3.0 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa km 1.66 mkoani Mwanza.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan azindua Mradi wa Maji Butimba
Neema ya lita milioni 48 kwa siku kwa wakazi 450,000 wa Mwanza. Maendeleo yanamwagika.
#kaziNaUtu#TunasongaMbele
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mradi wa maji wa Butimba mkoani Mwanza tarehe 20 Juni, 2025. mradi huu wa maji una uwezo wa kuzalisha maji lita milioni 48 kwa siku na hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika Jiji la Mwanza kwa kuwanufaisha wakazi wa wapatao 450,000 katika maeneo ya Nyegezi, Mkolani, Buhongwa, Lwanhima, Fumagila, Sahwa, Igoma, Kishiri na Nyamhongolo.
#TikiKwaSamia
Rais Samia Suluhu amezitaka halmashauri zote kusaidia vikundi vinavyoshindwa kujaza fomu ili mikopo iwafikie walengwa kwa urahisi.
#MamaAnafanikisha#KaziNaUtuTunasongaMbele
Taifa Moja. Maendeleo Zaidi. Kazi Zaidi.