“Kizuri kuhusu Nyerere ni kuwa licha ya kuwa na Mamlaka Makubwa aliachia madaraka kwa hiari bila kuhusishwa na wizi, Ufisadi au Uchafuzi wa mali za Umma. Aliondoka madarakani na mikono misafi, huwezi kumtuhumu Nyerere kwa wizi, hakutuibia tena aliondoka bila Pension” Tundu Lissu
"Kwenye kuposa na kujadiliana mahari wanakwendaga wachache ila kwenye harusi wanakuja wengi. Ndivyo maisha yalivyo, utahangaika na wachache ukifanikiwa watakujalia wengi. Iko hivyo na itabaki kuwa hivyo. Kubaliana tu na
hali halisi." ~Togolani Mavura.
"Mwenyezi Mungu ameficha katika macho ya binadamu mambo 3, umri, rizki na kiama. Hatujui tutaishi miaka mingapi, hatujui rizki yetu ya kesho na hatujui mwisho wetu na maisha yetu akhera yatakuwaje. Hekima yake ni tuwe wanyenyekevu." ~Togolani Mavura.
"Maisha yakikunyoosha nyoka nayo, yakikukunja kunjika nayo. Ukiwa huna usiishi kama unazo. Usijitutumue wala usishindane nayo. Wakati mwingine yanakunyoosha au kukukunja ili utoshe na uweze kupenya kwenye upenyo wa kuelekea kwenye neema yako." ~Togolani Mavura.
"Hata kama unamjua mtu, ukikuta foleni panga foleni, ukiiruka unamuweka huyo unayemjua katika wakati mgumu dhidi ya walioko kwenye foleni. Mpe nafasi huyo unayemjua atafute njia bora ya kukusaidia isiyokwaza watu. Ukiondoka yeye atabaki nao". ~Togolani Mavura.
Ushuru unatakiwa upande kwenye mambo yasio na lazima kama vile mawigi, zile nyusi za bandia, mikorogo.... na kadhalika.... kwasababu unapotumia laki nane kwa ajili ya nywele bandia wakati hauna kipara, kwakweli ni swala ambalo mimi sijawahi kulielewa!
Anayetaka kuzozana na wewe, anaamini bado suluhu yaweza kufikiwa kwa mazungumzo. Jadiliana nae. Ni heri kutofautiana mdomoni kuliko kila mmoja kujichukulia maamuzi yake kivyake moyoni. Yanayotatulika ni yale yanayojadiliwa. Wanaozungumza, hawagombani. Hakuna lisilozungumzika!
Ukiona umeomba kwa Mwenyezi Mungu msaada na haupati majibu, jua kuwa hiyo shida bado iko ndani ya uwezo wako kuitatua. Ukimya wa Mwenyezi Mungu nao ni jibu.