Hiki ni chungu cha kuzalisha wabeba sumu, majambia na marungu, kwamba za kunyongea, mabunduki na kauli za vitisho. Ile kauli ya jamaa wa Bukoba inaakisi hulka za wengi waliomo kundini.
“Acheni Unafiki– Mauaji ya Enock ni zao la mfumo wa CCM”
Kuna jambo moja la kusikitisha kuliko mauaji ya kijana Enock Mhangwa ni unafiki wa viongozi wa UVCCM kujifanya wameshtushwa na jambo walilolilea.Enock hakuuliwa na majambazi. Ameuliwa na watu waliovaa mamlaka ya serikali ya CCM. Viongozi wa mtaa waliopaswa kumlinda ndio waliompiga hadi kufa kwa tuhuma tu. Huo ndio mfumo wa hofu, ubabe na uonevu ambao CCM mmeutengeneza kila ngazi ktk Nchi.Sasa mnakuja na kauli za “kulaani” wakati mmejenga mfumo wa kutokuwajibika, mmegeuza vyombo vya dola kuwa silaha za kisiasa, na mmelea utamaduni wa kujichukulia sheria mkononi.Hamna haki ya kusema “tunalaani” wakati mmewasha moto wenyewe. Kauli zenu hazina maana kama hamko tayari kusafisha mfumo wenu.Watanzania wanajua ukweli. Na hawadanganyiki tena.
Wananchi siyo wajinga. Wanaelewa maana ya NO REFORMS, NO ELECTION. Wameipokea kwa mikono yote. Wamepima kati ya porojo za mbogamboga na NRNE, wanajua ipi pumba. Sikiliza ufafanuzi wa mwananchi kwa ufupi. #NoReformsNoElection
NB; Mwamba ubongo wake ni timamu kuliko wa MADELEKA
@fatma_karume kipindi Cha chaguzi enzi ya Salmon Amour komandoo na Aman karume junior yaliyotokea unayatofautishaje na tukio hilo la Geita? Tupe darasa hapa.
Nimeiangalia hii clip kwa huzuni.
Kuna wanaume 4 wanaangalia mwenzao akimpiga mtu kwa UKATILI na moja anapiga video kwa Raha yake.
Hata moja wao haja sema BASI utamuumiza! 😢
Jamii yetu ina TATIZO kubwa ya kuona UKATILI ni jambo la kawaida.
Tunahitaji MAFUNZO ya Jamii.
@MabalaMakengeza Baba alivyo ndivyo mtoto alivyo. Rejea matukio yaliyotokeakisutu mpaka kule maporini tulikoambiwa. Kijana naye alifungwa mikono na kupelekwa porini. MAJI YANATOKA MLIMANI KUSHUKA BONDENI. Familia hairithi kutoka kwa jirani, bali mali ya familia. Tuendelee tu mwl @MabalaMakengeza
VIDEO:
Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, amesema kuwa Serikali ya Mkoa inatarajia kujenga mnara wa kumbukumbu kwa heshima ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ikiwa ni sehemu ya kuenzi mchango wake mkubwa katika maendeleo ya mkoa huo.
Akizungumza Ijumaa Julai 4, 2025 jijini Dodoma wakati wa mkutano na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita, Dendego amesema mnara huo utajengwa katika kipindi cha pili cha Serikali hiyo na utasimama kama alama ya kutambua jitihada za Rais Samia ikiwamo ujenzi wa uwanja mpya wa ndege mkoani Singida.
"Haya yatakapokuwa yanaendelea na kukamilika, basi ndoto ya Singida inaenda kutimia, tayari tumeandaa miradi ya kimkakati ya kipaumbele, na tunaendelea kujipanga kuhakikisha tunakwenda sambamba na kasi ya maendeleo ya nchi," amesema Dendego.
2020 Niligombea...Nililinda kura zangu....Nikakusanya Matokeo yangu...Returning Officer wa Jimbo hakuhitaji matokeo yangu ili kujumlisha kura za jimbo.Alikuwa na matokeo yake kwenye laptop. Na alisema wazi kwamba Tayari ana matokeo. Na akaniandikia Barua kwa Kiburi kabisa kwamba Niende kokote ninakotaka.
Nikaenda Mahakamani walipopokea Petition yangu na kuona nimeomba scrutiny ya kura zilizopigwa Mkurugenzi wa Halamashauri( Hapa soma Returning Officer aliye apishwa ) tuliambiwa kiapo kinawafanya watakatifu.
Akaagiza wafanyakazi...wakafungua masanduku ya Kura wakaanza kuchoma kura zangu na kupiga kura upya. Nikakimbilia Tune ya Taifa ya uchaguzi.Wakasema kwakuwa niko Mahakamani hawawezi kuingilia...Mahakama Ikaniambia hatufanyi chochote mpaka udeposit Milioni 12 taslimu.
Ndugu yangu ,Hauwezi kulinda kura kwa Rungu na Majabali kura zinalindwa kwa Sheria na Kanuni zinazo hakikisha uwazi wa Zoezi Zima.
YEYOTE ANAYEKWAMBIA UTALINDA KURA NI TAPELI.
Huyohuyo afande alisusa kuongea na maafisa uhamiaji katika suala la mke wake, akakimbilia mahakamani. Anajizima ufahamu kwa kudhani pesa ya Mwarabu itaondoa njaa ya familia yake.
SITOCHOKA KUKUFUNDISHA, AFANDE!
Nilifikiri kwa kuwa ni WAKILI, umesoma HISTORY kama mandatory subject. Lakini kila nikisoma maandishi yako naona somo hilo lilikuwa mama mkwe kwako.
Nitakupiga msasa hapa. Je, unajua lolote kuhusu SWADESHI MOVEMENT? Somo la siku nyingine hilo. Unajua kuhusu Mahatma Gandhi’s boycott movement?
Gandhi’s Boycott Movement - Vuguvugu la kususia la Gandhi lilikuwa sehemu muhimu ya Non-Cooperation Movement lililozinduliwa mwaka wa 1920….
Vuguvugu hilo lililenga kupata uhuru wa India kutoka kwa utawala wa Waingereza kupitia upinzani wa amani (peaceful resistance), bila kumwaga damu….
Vuguvugu lilihusisha kususia bidhaa, taasisi na huduma za Uingereza ili kutoa shinikizo la kiuchumi na kisiasa kwa serikali ya Uingereza waliokuwa watawala.
Vuguvugu lilijumuisha kuwashawishi Wahindi waondoe kazi zao katika shughuli yoyote ambayo iliendeleza serikali ya Uingereza na pia uchumi India….
Kupitia ‘non violence’ waandamanaji wangekataa kununua bidhaa za Uingereza, kutumia kazi za mikono za mitaa, na maduka ya pombe ya kachumbari…..
Tofauti na kuongeza kujitegemea kwa kusokota khaddar (kitamba cha Gandhi), kununua bidhaa zilizotengenezwa na Wahindi, na kugomea bidhaa za Waingereza..,
Non-cooperation movement (vuguvugu la kususia) lilitoa wito wa kusitishwa kwa mpango wa kuigawa Uturuki (Khilafat movement) and the end to untouchability.
Khilafat movement ilikuwa kampeni ya kisiasa iliyoanzishwa na Waislamu wa Kihindi - India iliyokuwa ikitawaliwa na Uingereza dhidi ya Turkey……
Huu ulikuwa mpango wa kuvunja Milki ya Ottoman (Ottoman Empire) baada ya Vita vya Kwanza vya Dunia (World War I) na vikosi vya washirika (Allied forces).
Hii ilisababisha mikutano na migomo mfululizo iliyofanywa hadharani, ambayo ilisababisha kukamatwa Jawaharlal Nehru na baba yake, Motilal Nehru…..
Waziri Mkuu wa Kwanza wa India, Jawaharlal Nehru katika autobiography yake “Toward Freedom” aliandika akiwa gerezani 1934/35 ameandika na kueleza;
“Hili vuguvugu la kususia (The non-cooperation movement) ndiyo lilikuwa vuguvugu kubwa katika kutafuta uhuru wa India kutoka kwa Waingereza.”
Hivyo, katika historia, Mahatma Gandhi alifanikiwa vizuri tu kuondoa matatizo na changamoto kwa KUSUSA. Waingereza walikuwa KATILI. Lakini ALISUSA….
Ukijitikisa kidogo ndugu Afande, nitakupa mfano mwingine wa ‘Maandamano ya CHUMVI’. Hapa nitakueleza kuhusu SWADESHI MOVEMENT…..
NB; Ubunge siyo makalio kwamba kila mtu atapewa.
Aliyekua Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG) Dr.Adelarus Kilangi (LLD) akiwa na makada wenzie wa CCM waliotia nia ya ubunge jimbo la Nyamagana. Juzi tumemuona aliyekuwa Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi (NEC) Dr.Wilson Mahera akichukua fomu ya ubunge Butiama kupitia CCM, leo tumemuona aliyekua Mwanasheria Mkuu. Enyi Watanzania, mnataka mumuone nani tena ndio muamini kwamba reforms ni muhimu kabla ya uchaguzi? Ndio maana tunasema #NoReformsNoElection
CCM walishasema Ina wanachama milioni 13, wapiga kura waliojiandikisha ni laki ngapi ukiondoa hao wa CCM, CCM B a. a. k. a ACT inawapigakura wake wangapi Tanganyika hasa Kigoma na mikoa ya kusini? ACT Tanganyika vs ACT Zanzibar. Toilet brush.
JIBU KWA MSEMAJI WA SERIKALI – TAARIFA YA KUPUUZA INAPUUZIKA
Msemaji wa Serikali ametoa taarifa kwa umma akikanusha kuwepo kwa mpango wa kumdhuru kwa sumu Mhe. Tundu Antipas Lissu, ambaye kwa sasa anashikiliwa gerezani akisubiri hatima ya kesi yake. Hii ni taarifa ambayo kwa haraka sana inataka Watanzania waiamini kama ilivyo, bila kuuliza maswali yoyote. Hilo haliwezekani.
Kwanza, ni jambo la kushangaza kuwa Serikali ya Tanzania inaona taarifa kuhusu usalama wa mtu aliyeko gerezani ni jambo dogo la kupuuza, badala ya kuchunguza kwa kina na kuwapa Watanzania uhakika wa kisheria na kibinadamu kuwa hakuna mtu anayeweza kuumizwa akiwa chini ya uangalizi wa dola. Mtu yuko gerezani si kwa mikono ya familia, bali kwa mikono ya dola yenye dhamana ya uhai wake.
Pili, Serikali inataka wananchi “wapuuze” taarifa zinazoibuliwa na watu walio huru kuhoji, lakini inashindwa kueleza hatua madhubuti zinazochukuliwa kulinda usalama wa Lissu, hasa ikizingatiwa historia yake ya kushambuliwa kwa risasi na kuachwa karibu na mauti mwaka 2017 – jambo ambalo hadi leo halijapata majibu ya kitaifa yanayoridhisha.
Tatu, kauli ya Serikali kwamba “haijawahi kuwa na mpango wa kumwekea sumu mtu yeyote” ni ya kisiasa kuliko ilivyo ya kisheria. Hakuna aliyedai kuwa kuna “waraka wa Serikali” unaoonyesha mpango huo, lakini kuna hofu inayoibuliwa na mazingira, mienendo ya kisiasa, na historia ya ukandamizaji dhidi ya viongozi wa upinzani. Badala ya kuropoka “taarifa hizo ni za kupuuzwa,” Serikali ifungue uchunguzi huru wa kimataifa kuondoa hofu hiyo.
Mwisho, taarifa ya Msemaji wa Serikali haina majibu ya msingi, haina dhamira ya kujibu hoja kwa hoja, na badala yake imejaa dharau kwa fikra huru. Hali ya Mhe. Lissu inazua taharuki kwa watu wengi ndani na nje ya Tanzania. Serikali inayojali maisha na heshima ya watu wake haina sababu ya kukasirika inapoulizwa, bali inatoa majibu yenye uthibitisho na hatua thabiti za kiusalama.
Tanzania ni yetu sote, si ya msemaji wa Serikali.
@zittokabwe kwa kuwa unajuaga kujikomba kwa viongozi, nisaidie kuwauliza Kirangi na Mahela walikuwa wanafanya kazi wakiwa wanachama wa chama gani?
Uanachama wao uliathili watu wengine kwa kiwango gani? Zitto miaka yako ikiongezeka ndipo akili na uelewa wako unapungua?
Hata Nnape alipigiwa simu kusitisha zoezi la kuchukua/kuzama form ya ubunge, ila tayari alikuwa na intel, akakacha kuipokea, kisha akajaza na kuwasilisha form yake, lawama zikafuata baadaye.
@mwaipungu24 endelea kuuza utu wako kwa kuwashangilia wauaji. Clubhouse unaelezwa lakini masikio umeziba. Ni aibu sana kwako kujitambulisha kwa jina lenye kunasabiana na Mbeya. Mzee Mwaikambo alisema kwamba haiwezekani kwa Mnyakyusa kulala kitanda kimoja na maiti.
"Mikopo Migi iliyosainiwa humu Bungeni niya Awamu iliyopita" :~ Rais Wa BahatiNasibu😁
Usikute Dkt. John Pombe Magufuli anaendelea Kukopa huko alipo na Sisi Hatufahamu Masikini... 😁
Serikali ya mizimu Ina kitengo cha misukule. Sasa hivi hiki kitengo kinashughulika na kuua watu, kinaombewa kibali kifanye kazi mahakamani, kinaandika barua za kufungia makanisa, kinateka watu, kinabaka wanaharakati. Mzee #Mangula uko wapi, njoo uone angalao we una akili.
Kweli taarifa ambayo ipo YouTube ya Jambo TV and channel nyingine za Youtube unahitaji shahidi wa siri wa nini? Wakati haya maneno kila mtu kayasikia, wasiojulikana wanataka kuja mpaka mahakamani sasa! Hatutakubali kamwe, hakuna mahakama za giza!!
Ujumbe huo wa Makinda umfikie popote alipo @zittokabwe . Huyo mama ni mkuu mstaafu wa mhimili mmojawapo wa dola, akumbuke kuwa kwa Tanzania hii, kila kauli ya mkuu wa mhimili ni Sheria inayotakiwa kutekelezwa. Kama atabisha amuulize Ask Gwajima.
"Hata Mkiwachagua Wengine Hawatashinda" :~ Bi Anne Makinda
"Hata Mkipiga Kura Kwingine CCM itaunda Serikali tu" :~ Samia Suluhu Hassan
Ewe Mtanzania unaesoma Post hii Usipoteze Muda wako Kwenda Kupiga Kura bila ya Mabadiriko kwenye Mifumo ya Uchaguzi.
#Reforms zifanyike kwanza
"If you fight, you die! You do
not fight, you die! What do you do? You fight!”
[Ukipambana, utakufa!Usipopambana, utakufa! Utafanya
nini? Unapambana!]
Hivyo, tunatamka na kusisitiza kwa Watanzania wa Tanganyika na Zanzibar; wa Unguja na
Pemba; kwamba TUTAPAMBANA!
TUPAMBANE!
"If you fight, you die! You do
not fight, you die! What do you do? You fight!”
[Ukipambana, utakufa!Usipopambana, utakufa! Utafanya
nini? Unapambana!]
Hivyo, tunatamka na kusisitiza kwa Watanzania wa Tanganyika na Zanzibar; wa Unguja na
Pemba; kwamba TUTAPAMBANA!
TUPAMBANE!
Miaka ya 70s tulitumia sana hiyo miti kuruka Kama kivukio cha mito . Pia tuliitumia kufanya mashindano ya kuchupa ktk shule za msingi. Tulikuwa tunaziita UPONDO. Huyu dada kanikumbusha hukooo. Hongera zake
Naamini Kabisaa Kuna Siku isiyokua na Jina WATANZANIA Wataamka. ninachoamin kwenye Maisha yangu Hakuna Unyonge na WOGA wa Milele ipo Siku isiyo na Jina Yaja.
Serikali ya @ccm_tanzania endeleeni Kusema tu kua Watanzania ni Waoga, Vijana wana Hasira, ajira Ugumu wa Maisha ipo Siku