Che Malone Fondoh:
“For our families and the whole of Tanzania. We are playing for Tanzania, for Simba.”
“So we are representing Tanzania here now.”
“I am proud to say we lifted the flag of Tanzania up and we will do that until the end.”
#NguvuMoja#CAFCCwithMicky
Ili Yanga afuzu anatakiwa amfunge muarabu na Hilal, na hilali amfunge muarabu na muarabu amfunge Hilal na Hilal asitoe sare na muarabu amfunge Mazembe ila Mazembe asifungwe na Muarabu. Mmeelewa ? 🤣🤣
Kwa muda mrefu sasa nimekua nafanya utafiti juu ya uchezeshaji wa mechi kutoka kwa marefa, uwezo wao wa kumudu mchezo, na kutawala hisia za wachezaji, kuhimili presha
n.k
Kuna jambo 1 ambalo limeota mizizi sana kwenye ligi yetu linafanywa la kawaida sana ila halitakiwi kuwa kawaida na linatakiwa litengenezewe sheria au kanuni kali.
Refa akishaamua tukio aidha ni penati au faulo imekua ni tabia kwa wachezaji kumfuata refa kumsukuma, kumvuta mikono, na kutumia nguvu isivyo kawaida. Kimsingi hilo ni kosa.
Niwakumbushe kisa kimoja cha Ronaldo kufungiwa mechi 4
August 13, 2017 mechi kati ya Real Madrid vs Barcelona mkondo wa kwanza, Madrid alishinda 3-1. Ronaldo alipokea red card kutoka kwa refa Ricardo De Burgos baada ya mwanzo kuvua shati alipofunga goli, na kupewa kadi ya njano, na baadae alipigwa kadi ya njano ya pili kutokana na kumsukuma refa kwa mikono yake baada ya kukataa maamuzi ya refa. Ronaldo alikula umeme mmoja safi, na akatolewa nje ya uwanja.
Sio hvyo tu, Ronaldo alipewa adhabu ya kufungiwa mechi 4 na Chama cha marefa Spain kupitia taarifa ya La liga sababu kubwa ya kufungiwa mechi 4 ilikua ni kumsukuma refa.
Kisa hiki kiwe rejea tosha kwa TFF / Bodi ya ligi kupitia Chama cha Marefa Tanzania. Refa ndiye pilato wa mwisho uwanjani, maamuzi yake yawe mazuri au ya hovyo anatakiwa aheshimike kwa wachezaji na madaraka aliyopewa.
Mfano mzuri ni Mechi ya jana - Singida vs Simba, refa mara kadhaa alikua anasukumwa sana na wachezaji wa Singida mithili ya kutaka kumpiga kwenye matukio zaidi ya matatu tofauti. Kilichofanyika kilikua ni kosa kwa wachezaji kufanya hvyo, na haitakiwi kuishia tu kwenye kadi za uwanjani, ila mchezaji akimsukuma refa au kuvuta jezi yake inatakiwa apewe adhabu kutoka kwa TFF ( Bodi ya ligi)
Barua yangu ifike kwa wenye mamlaka, lazima tuwe na kanuni/Sheria ambayo ni kali kuwalinda marefa na utovu huu wa nidhamu kutoka kwa wachezaji. Hii tabia ikikomaa ya kusukuma marefa, ipo siku refa atapasuliwa kwa kupigwa ngumi, au vibao vya uso.
@shaffihdauda1 Leo umenena kiufasaha zaid kwenye ukwel tuuseme na hapo nadhan bodi ya ligi pamoja na chama cha MAREFA walipitie hili na kulifanyia kazi sio kuishia kuangalia sheria ichukue mkondo wake
Wanavyoacha itakuja kumletea mtu madhara na majeraha
Hiki nikitendo kwa kukemewa
"Michango yetu ina nafasi kubwa na kuthaminika katika mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii zetu" Mwatima Issa, Mjumbe wa Bodi TAMWA-ZNZ.
#16DaysOfActivism#stopGBV