Bendera ya Taifa imepewa heshima kubwa, ahsanteni mashujaa wetu kwa heshima na Ushindi mkubwa mliotupa kama Taifa.
Nimefarijika sana kama mdau wa michezo na kipekee nimpongeze Rais Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na Rais wa TFF ndugu Wallace Karia.
Ahsanteni Mashujaa wetu ๐น๐ฟ
Kipindi hiki cha likizo ya Msimu wa Ligi Tanzania nimependa na nimesapoti namna vijana wetu wanarudi na kuipa jamii ilowalea kidogo walichovuna.
Nimewaunga mkono baadhi, ni muhimu kuwa na aina hii ya mioyo kwenye michezo, unapata kwa jasho kisha unarudisha Tabasamu la watu wako.
Hongereni Vijana wote, mmeweka kando Uyanga na Usimba, mmeweka mbele Uungwana michezoni na kwenye Jamii.
Mmeonesha ukomavu.
Wanasimba hatuna Haja ya Kutoka Mchezoni, hatujafanya vibaya kiasi cha kupoteza Imani bali tumeteleza nje ya Malengo.
Tusimame tupige Kazi, Tujipange kwa Ushindi.
#SoloTalks
Hongera Yanga kwa kuingia Fainali, sipo katika siasa rahisi, natambua ukubwa na umuhimu wa hili kombe kwa Taifa letu.
Mmepigana Kiume, Mmeshinda Kiume, ni nguvu ya uwekezaji katika usajili, mmekua bora sana Msimu huu.
You Deserve it all.
Sisi ni wa Allah na kwake tutarejeshwa, nimepokea kwa mshituko mkubwa kifo cha aliyekua waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Ndugu Bernard Membe.
Alikua mtumishi mahiri kwa Serikali na Chama chake cha Mapinduzi, alikua anasimamia anachokiamini na hakika amekufa na Heshkma yake.
Yanga wametoa somo, tukajifunze, Yanga wanapigana kwa namna yao, wamekua bora kwa misimu hii miwili.
.
Kuna mambo mawili hapa, kujifunza na kujirekebisha ili tuwe bora zaidi na zaidi. Wachezaji wetu wawekewe akili ya mapigano.
.
Hongera Wananchi.
#SoloTalks
Maisha ya Kibu Denis yawe funzo kwa Vijana wote wapambanaji, unapona unakata tamaa mtazame Kibu namna amekabiliana na changamoto.
Maisha yake yanatufundisha kuwa juhudi ndio msingi wa mafanikio, Ukiwa na imani kwamba maneno ya waja hayasumbui ila kwa Kudra za Allah.
#SoloTalks
Leo naadhimisha siku yangu ya kuzaliwa, Umri unavyoenda najifunza mengi kama mzazi, mume, rafiki na mfanyakazi.
Moja mambo muhimu ni jamii ya watu wanaotuzunguka ambao kila siku wameamua kuwa bora kwenye maisha yetu.
Ahsante Marafiki, Mimi ni ndugu yenu na sitobalika.
Tumeshinda mechi na tumeonesha kwa nini tunacheza robo fainali ya ligi ya Mabingwa barani Afrika.
Ahsante wanasimba kwa wingi mliojitokeza uwanjani, tumeonesha ukubwa na maana ya #NguvuMoja.
Sisi ni Simba
Tanzania ya leo inapaswa kulitazama suala la maadili kama vita kamili.
Inahitajika nguvu kulinda akili na miili ya watoto wetu, Walimu mashuleni ni muhimili mkubwa.
Mwisho kila mmoja acheze nafasi yake kuhakikisha tunashinda hili pambano.
#SoloTalks
Jumatatu ya Wazee kwa vijana, wanawake na watoto, ni Jumatatu ya wote na iwapo tutatimiza majukumu Yetu Basi Taifa litanufaika na uwepo wetu
Ila tukiamua kuwa jamii ya kulalamika basi Taifa litapata hasara ya uwepo wetu, sababu Taifa la walalamishi HALITOBOI.
#SoloTalk
PICHA KUBWA, MAANA KUBWA.
Sio ajabu kwa maisha yetu, mitaa yetu imetulea kwa umoja.
Kama Yanga na Simba, Muislam na Mkristo tunaishi nyumba moja kwa nini isiwe vyama vya siasa..?
Sisi ni Tanzania itakayodumu milele, Ipepe bendera yetu ya โUhuru na Umojaโ
#SoloTalk