#UPDATES_SHAURI_LA_UHAINI
Part 1
Mahakama imeamuru kuwa committal itasomwa yote bila kurushwa live.
Wakili wa Serikali Katuga anaendelea kusoma kwa sasa.
Maajabu yaliyotokea ni kwamba mawakili wa serikali waliomba maelezo ya mashahidi wa siri yasirushwe live.
Lakini cha ajbu mahakama imesema maelezo ya mashahidi wote yafichwe na yasiwe live.
Kifupi mahakama imetoa uamuzi ambao hata serikali haijaomba. Imefunga kila kitu na kesi kuzimwa.
Katuga anaendelea, amemkumbusha Mtuhumiwa Shitaka lake na kumkabidhi taarifa ya mashitaka.
Anasema Jamhuri itakuwa na mashaidi 30 na vielelezo vya myaraka 9.
Maelezo yataanza kusomwa na Thawabu Isa wakili wa serikali.
Anasimama na kuanza kusema SSP Kangio, atakuwa shahidi wa kwanza. Ameapa kusema ukweli na maelezo yake ni kama ifuayavyo.
Nimeajiriwa 2003 polisi na mikoa mbalimbali ninefanya. Nimekuwa na vyeo tofauti na sasa ni mrakibu wa polisi kanda ya Dar es salaam. Nafanya majukumu ya kusimamia askari katika majukumu ya kiupelelezi.
04/04/2025 nikiwa ofisi afande Kaaya anayefanya Doria mtandaoni nilimtaka anipe picha mjongeo kuhusu maudhui yakiyokuwa yanatoa taarifa yenye uchochexi.
Maudhui hayo ni mapolisi wanakuja na mabegi ya kura feki kwenye vituo. Jambo ambalo ni uongo. Majukumu yetu ni ulinzi na sio kuiba kura.
Pia maelezo yaliyokuwepo ni kuhusu majaji ni MACCM hivyo wanafanya kazi kwa mujibu wa CCM. Na sio kweli kwamba majaji wanafanya kazi kuwaonea wapinzani. Na hivyo taarifa hii ni uongo na yalilenga kuleta chuki.
Pia alisema kuenguliwa kwa wapinzani ni mkakati wa serikali hivyo zilikuwa ni uongo na kutengeneza chuki dhidi ya Rais.
Na msimamo wetu ni wa uasi. Ni kweli ni msimamo wa uasi kwani tunaenda kukinukisha na huu uchaguzi tunaenda kuuvuruga kwelikweli.
Katika picha mjongeo hiyo mzungumzaji alikuwa ni LISSU. Na aliyokuwa anafanya yalikuwa na nia ya kuitishia serikali ili ayapate yeye na wafuasi wake.
Niliamuru Insp. Kaaya aanze kufanya uchunguzi wa jalada hilo na taarifa hiyo ndio akafungua kesi na kuanza uchunguzi. Na akaanza kujaza PF500
Baada ya kutoa maelekezo kutafuta mjengeo iliyoerekodiwa eneo husika nilitoa taarifa kwa mabosss wangu na kuhusu kile alichosema TUNDU LISSU mtandaoni. Niliripoti kwa afande DCI akasema tuendeleee
Nilimtafuta kiongozi wa JAMBO TV anipe video ile na baadae akasema video anayo P ambae kasafrir. Hivyo nikatoa taarifa kwa maboss kuwa video tutaipata kwa P ambayo yuko Dodoma.
DCP NG'ANZI nilimpa taarifa kuwa tutaipata kwa kijana wa Jambo TV ambae yuko Dodoma.
Haya ni maelezo ya George ambae ni kaimu mkuu wa upepelezi kanda ya Dar es salaam. Yansomwa maelezo yake hapa mahakamani.
Nikaeleza lifunguliwe kosa la uhaini kwasababu aliesema TUNDU lisuu hayo maneno yake, yeye ni Askari ambae ana cheti cha Kujenga taifa kutoka jeshi la JKT hivyo alikuwa na wajibu wa kulinda amani ndani ya Taifa letu. Kusema maneno kama hayo ni kosa kisheria.
Hayo ndio maelezo yangu yote. Yameisha maelezo ya George na anasemaa anayo maelezo ya nyongeza Ya huyo SSP George akasema pia nilikabidhiwa TUNDU LISSU akitokea RUVUMA.
Nilimpokea Lissu na wakati nafanya mahojiano walikuja mawakili wake pia Tulienda kwenye ofisi yenye utulivu na nikamuonya kuwa anatuhumiwa kosa la uhaini. Na kumpa haki zake za msingi.
Huyu George ni msaidizi wa Mafwele. Anasemaa Lissu aligoma kutoa maelezo yoyote.
ASP. John. Ni shaidi wa pili ambae ni mkazi wa Temeke. Amekula kiapo na ushaidi wake ukaanza kuandikwa.
Nimeajiriwa 2005 na nina elimu ya computer na mfanyakazi wa polisi. Nimesoma vyuo ikiwemo Chuo Cha Polisi kurasini.
Nafanya kazi kwa DPP dawati la Doria mtandaoni. Na huwa napeleleza makosa yanayofanywa mitandaoni.
Huyu sasa ni shaidi wa pili baada ya yule wa kwanza ambae ni George.
Part 2 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Retweet yako.
UPDATES SHAURI LA KUPINGA MASHAIDI KUFICHWA KWENYE KESI YA MHE. LISSU
Part 4
Wakili @Advocate_Jebra anasimama, Mwamba ni mrefu na kipara chake. Anasubiri Judge amalize kuandika anamuangalia kwa kuibia hivi.
Sasa anaanza.
Wasilisho langu litakuwa kwenye msingi wa haki ya haki yakusikilizwa na kuendesha mashauri kwa haki. Ukisoma katiba yetu ibara ya 13(6)(a).
Wakati hakimu anafanya maamuzi haya hakuzingatia kwmaba uamuzi wake utamuathiri mteja wetu katika haki yake ya kusikilizwa kwa haki na kupewa nafasi ya kuona shauri lake linaendeshwa kwa uwazi.
Kwenye maamuzi yale hakufanya uchambuzi wa kwamba kuthibitisha mashtaka inapaswa kuwa beyond reasonable doubt yaani bila kuacha shaka yoyote wakati kuthibitisha kesi za jinai.
Kama angefanya proper analysis angegundua kuwa wasiwasi ulioibuliwa na Dr. NSHALA angefahamu kuwa hakukuwa na maana yoyote ya kutoa order ile aliyoitoa. Maana alishaonyeshwa hatari iliyopo mbele.
Upande wa jamhuri wanapaswa kutimiza wajibu wao wa kama kuna shahidi ametishwa wawakamate wanaowatisha. Sio wameshindwa kutimiza wajibu wao halafu aumie mteja wetu kwa kukosa haki ya kusikiliza kesi yake kwa uwazi na haki ya kuwajua mashahidi na kuwaona.
Mh. Jaji hatuna uhakika hata kama Hakimu alijiuliza hivi mashitaka yanayomkabili mteja wetu ya uchochezi hata adhabu yake ina option ya fine. Na makosa hayo sio serious offence kabisa. Sasa unasemaje kwamba mashahidi watakuwa hawako salama wakati hata mashitaka ni kusema taarifa za uongo sasa si angeweza kuja ambae anajua kuwa ukweli ni upi na kutoa clarification ya ukweli wenyewe.
Makosa hayo kwanza yangeweza kushitakiwa kwa defamation lakini pia hata mpaka sasa hatujaona athari za maneno yaliyosemwa na mteja wetu hadi leo.
Anaanza Mtobesya sasa.
Ni msingi wa kisheria kwamba fair trial inahitaji mshitakiwa akutane na wanaomshitaki na mashahidi na kunakuwa na exception pale ambapo yako maombi maalumu ya kuomba kufichwa.
Mashahidi wakifichwa demeanor haitaonekana kabisa. Na yapo maamuzi ya mahakama ya rufani yanasema demeanor inaangaliwa sana na trial Court na kutokaana na shahidi alivyoonekana basi credibility yake nimeitia mashakaa hivyo ushahidi wake naitulia mashaka.
Maamuzi ya mahakama ya rufani Trazias Evarista alias Deusdedith Vs Republic kesi ya 2020
Kwanini tunasema credibility na demeanor ya shahidi ni muhimu sana. Zoezi la kuficha mashahidi linaweza kutumika kuathiri haki za mtuhumiwa. Sasa mahakama ni muhimu kuwa makini sana wakati inafanya maamuzi ya kukubali kuficha mashahidi.
Sababu za kufanya hivyo zinatakiwa kuwa ni nzito sana. Na uzito wake unapaswa kuwa umeambatanishwa na viapo vya wahusika kama vile ile report ya kiintelijensia ya MAFWELE ilipaswa kuwa imeambatanishwa na kiapo chake.
Sasa tunasubmit kwamba sababu zilizotolewa haziwezi kuondoa umuhimu wa mahakama kuwaona mashahidi na kuangalia demeanor yao.
Mtuhumiwa atashindwa kuielezea demeanor ya shahidi kuishawishi mahakama.
Wasilisho letu ni kwamba hata kama maombi yalisikilizwa exparte yaani upande mmoja tu. Mahakama ilikuwa na wajibu wa kutokukubali kila kinachosemwa na Jamhuri yaani waleta maombi katika maombi yake kule mahakama ya Kisutu.
Ilipaswa kuyasikiliza na mahakama kutumia akili yake na sio kukubali tu. Hili ni kosa la kimsingi na limesemwa na katika kesi nyingi za mahakama kuu na mahakama ya rufani.
Kwa kumalizia tunaomba kusema fair trial inataka mshitakiwa awaone mashahidi na ku access demeanor yao na ukiangalia nature ya ushahidi unaonesha mahakama haikupaswa kuondoka kwenye msingi wa kisheria wa mashahidi kuwa wazi.
Hivyo mahakama ibatilishe uamuzi ule na tuendelee kusikiliza shauri hii kwa taratibu za kawaida na mashahidi tuwaone wanavyoonekana, sura zao, sauti zao na watakayokuwa wanayasema wayaseme tukionana uso kwa uso ili tuone wana ujasiri wakuyasema au wanaona aibu au vinginevyo.
Tunaomba kumalizia hapo kwa upande wetu. Tuwaachie mawakili wa serikali.
Part 5 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye post hii.
I arrived at Daresalaam Mwalimu Julius Nyerere International airport at nine am , and immigration referred my passport to the supervisor who has kept me waiting for an hour as she consults her superiors 1/3
VIDEO:
Kufuatia uwepo wa taarifa ya kwamba Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini @orpptanzania ametengua uteuzi wa vigogo wanane (8) wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA @ChademaTZ2) waliokuwa wameteuliwa na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu @TunduALissu na kisha kuthibitishwa na Baraza Kuu la Januari 22.2025, Wakili Maduhu William kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC @humanrightstz) ameeleza kushangazwa na hatua hiyo aliyoitaja kuwa kinyume cha sheria
Akihojiwa na Jambo TV, Wakili Maduhu amesema kwa mujibu wa sheria, Msajili wa Vyama vya Siasa ni mlezi wa Vyama vya Siasa na kwamba hana mamlaka ya kisheria ya kuingilia shughuli za ndani ya vyama, kuteua au kutengua uteuzi wa kiongozi yeyote wa chama chochote cha siasa
Wakili Maduhu ameenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hata yule aliyepeleka suala hilo kwa Msajili wa Vyama vya Siasa alikosea badala yake alipaswa kufuata taratibu za ndani ya chama chao na kama bado angeona hajatendewa haki ni vyema angekimbilia Mahakamani
Ikumbukwe kuwa, viongozi wa CHADEMA wanaotajwa kutenguliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa ni Wajumbe wa Kamati Kuu Godbless Lema @godbless_lema, Salma Kasanzu, Sheikh Hafidh Ali Saleh, Rose Mayemba @RoseMayemba na Dkt. Rugemeleza Nshala @rugemeleza (ambaye pia aliteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA), na Wajumbe wa Sekretarieti watatu (3) wakiongozwa na Katibu Mkuu John Mnyika @jjmnyika, Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara Amani Golugwa @amanigolugwa na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Wakili Ali Ibrahim
"Serikali ya Umoja wa Kitaifa ni jambo jema sana kwa nchi kama Zanzibar, lakini lazima itokane na uchaguzi ulio huru, wa haki na wa kuheshimika. Isiwe serikali inayotokana na ujambazi wa dola." Anaandika Mohammed Ghassani akiyarudia maisha ya Ahmed Rajab.
https://t.co/IfDNkk4EBD
#TANZANIA: FORMER BBC JOURNALIST, AHMED RAJAB PASSES AWAY
Ahmed Rajab, a former BBC journalist and political commentator, has passed away.
Rajab was known for his insightful analysis on Middle Eastern and African politics.
His contributions to journalism and his deep understanding of complex political landscapes will be remembered.