Sijui kuhusu ishu za forex lakini nimesikiliza jamaa nikajifunza yafuatayo kutoka kwake;
1. Amekuwa honest na vulnerable ku-share story yake, kitu ambacho ni ngumu sana kwa watu wengi.
2. Amekuwa muwazi kuwa, "Strategy" ni mchakato ambao ukirudia utapata MATOKEO yale yale au yanayokaribiana. Vinginevyo itakuwa ni gambling, au kubahatisha.
→ Amekiri wazi kuwa Video yake aliyoweka YouTube ya kutengeneza dola 4,000 ndani ya wiki 2 kwa kutumia 200 ilikuwa ni misconception na kubahatisha. Kwa sababu probability ya kufanikiwa kwa kufanya hivyo ni 1% out 100%.
3. Kukubali pale unapofeli au unaposhindwa. Ni ngumu lakini, that is the only way.
4. Kuishi flashy life ili kuaminisha watu kuwa umetoboa. MG anasema hicho ni kitu ambacho kimemgarimu sana. Epuka, na kuwa honest.
5. Kutengeneza pesa ni kitu kimoja na kuwa na hekima ya kumanage hela ni kitu kingine.
6. Jifunze ku-balance risk to reward ratio. Siyo katika trading tu. Hata katika biashara au uwekezaji wa kawaida. Kwa ni KUTOBOA ipo katika ya hofu (fear) na tamaa (greed).
7. Kuitwa mtaalam na tapeli ni kama pande mbili za shilingi hasa kwenye ishu ya hela.
8. Siku zote kuna yule rafiki mmoja ambaye atakuelewa na kuwa a shoulder to cry ukipatwa na majanga.
9. Ili kuwa mbele, unahitaji uwe kwanza kupiga hatua ambayo wengi huogopa. Ukiteleza utachekwa, ukitoboa utafuatwa.
10. Zaidi ya yote, nimejifunza mengi hasa kuhusu udhubutu na risk taking kwa jamaa. Na amekuwa honest kuwa, kwa vijana wanaojitafuta usiache shule, chonga nji ukiwa chuoni bado, uku unapambana pia.
11. Mwisho, maisha ni safari. Kusimama na kuanguka. Kushinda na kufeli. Tunaishi au kufanya jambo siyo kuepuka makosa au kufeli, bali kupunguza risk na rate ya kurudia makosa yale yale tena.
Nimejifunza hayo machache kati ya mengi.