Leo tarehe 4 Agosti, 2020 Mgeni rasmi katika maonesho ya Wakulima nanenane Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso alitembelea banda la MORUWASA ambapo ameishukuru Mamlaka kwa kuendelea kupambana na Changamoto ya maji kwa kubuni njia mbalimbali zinazotatua changamoto za maji.
Leo tarehe 8 Julai, 2020 MORUWASA imekabidhiwa Mabwawa ya Majitaka yaliyokua yakifanyiwa Ukarabati na Kampuni Tanzu ya Shirika la Mzinga Makao Makuu Morogoro baada ya Ukarabati kukamilika, Mabwawa hayo yamekabidhiwa mbele ya Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Dkt. Tito Kazige.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Juma Aweso na Uongozi wa MORUWASA wamefanya ziara ya kuona maendeleo ya Mtambo wa Kuzalisha maji Mambogo, Maboresho ya Mabawa ya Majitaka Mafisa, Mradi wa Ujenzi wa Tanki la Maji la Mguru wa Ndege tarehe 2 Juni,2020.