MAMA yako anaweza kukwambia mabaya ya BABA yako ila kamwe BABA yako hawezi kukwambia mabaya ya MAMA yako, unajua kwanini?
Akikwambia mabaya ya MAMA yako ni sawa na kukwambia alikosea KUOA.
Wazazi wetu kosa kubwa walilofanya ni kutufundisha kuwa watu wema na tukaamini kila mtu ni mwema!
Ila ukiingia mtaani ndio unakuja kugundua watu ni wabaya sana kuliko wanyama,unajikuta unajifunza in hard way!
Tumeondoka nyumbani kuja Mjini sio kwamba tuna uhakika sana na michongo ila tumeamua kuondoa kiwingu Maskani, Ndugu na Jamaa waamini tu kuwa tupo tunapiganisha kubutua kombe.
Sisi ndio wale tunapokea simu kutoka home za Fedha ama Majukumu, mfukoni hatuna hata thumni ila tunawaahidi kesho tutaituma hiyo pesa, ni sisi hao.
Tunaishi kwa ajili ya leo, kuna muda tunalala na jero tu! Mungu ametujalia afya hajatupa deni, tuondokeni Wanangu tukavuje jasho, MPAKA MWISHO.
Sikia Bro
Hakuna anayejali magumu unayopotia
Hakuna anayejali ni kiasi gani unakaza kupindua meza
Hakuna anayejali upweke na stress za maisha ulizonazo
Hakuna anayejali kama ulishindia mihogo
HAKUNA ANAYEJALI, cha msingi tafuta sana PESA
Ukiwa nazo wataanza kukujali
FACTS!
@FKihamu Maisha yamebadilika sana, kwenye umri mdogo, Vijana wameondoka home kwenda kusaka rizki mbali na home, hawana uhakika ila wanaishi kwenye MATUMAINI.
Ukiona Kijana mdogo kwenye harakati hajachagua kuwa Mwizi bali kushika biashara na kutembeza, ukishindwa kununua basi mpe salute zake tu.
Ukiona Kijana Mdogo ofisini anapambana usiwe kikwazo kwake, hujui nyuma wapo wangapi wanamtazama, akikosea mshike mkono usimtazame kama Mshindani.
Ukiona Kijana Mdogo yupo tu mtaani hana issue usianze kusema Madogo hawajitumi, hao wameshasukuma sana milango iliyoandikwa vuta ila vyuma vimekaza.
Maisha yamebadilika sana, kwenye umri mdogo, Vijana wameondoka home kwenda kusaka rizki mbali na home, hawana uhakika ila wanaishi kwenye MATUMAINI.
BACK BENCHA tunawakumbusha kuwa punguza kujipa UMUHIMU kweny MAISHA ya watu ile huwezi ishi bila mm haitumiki tena watu WANAISHI na WANAZEEKA bila ww.
Morning Africa.