#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Anaendelea Mhe. Lissu
Sheria inasema mtuhumiwa akikataa kusign mahakama iseme kuwa amekataa kwa kuandika.
Sasa mimi sijasign sijaweka gumba na wala hakuna paliposema nilikataaa kusign. Mambo yamevuruga kiujumla jumla tu.
S. 266(6) of CPA.Inasema mtuhumiwa ana haki ya proceedings kupewa hizo nyaraka zote.
Mimi nilichopewa rekodi ya Ukonga hii ambayo nimeikatalia na hii nyingine mlinipa hapa jana.
Kwahiyo sheria ilitaka nipewe kule Kisutu. Sasa nililetewa nyaraka ya uongo na nyingine nimepewa hapa wakati nilitakiwa kupewa zamani kabla ya mambo ya huku juu.
Kwenye rekodi niliambiwa nina haki ya kuita mashahidi nikifika mahakama kuu.
Angalau hizi nyaraka nilizopewa zinasema hivyo.
S. 266(3) of CPA nilipaswa kupewa hati ya mashitaka na hiyo hati haionekani kila mahali.
Anaonesha manyaraka yote aliyonayo kuwa hati ya shitaka haipo kama sheria inavyosema.
Kwahiyo nataka kusema nini?
Yote ambayo nilipaswa kupewa sikupewa. Na sio tu sikupewa havipo kwenye nyaraka tulizonazo.
Sasa hii ilikuwa ni committal proceedings au ni kitu gani?
Kesi ya Dodoli Kapufi inasema hakimu wa mahakaama inayosikiliza committal proceedings, majaji wa mahakama ya rufani wanasema hakimu huyo hapaswi kujiamulia anavyotaka mambo hayo. Afuate kanuni na taratibu.
Mamlaka ya hawa mahakimu kwenye committal iko limited, haiwezi kuamua kwenye masuala ya kisheria.
Naomba nimalizie sasa.
Tunakwenda wapi kuanzia hapa.
On the basis of all what I have said hakukuwa na committal. Ni ujinga mtupu.
Hii mahakama haiwezi kuendelea kusikiliza kesi hii kama committal haikufuata utaratibu na haikuchukuliwa kwa mujibu wa sheria.
Naomba mahakama ifutilie mbali mwenendo mbali wa ile committal.
Na kama itawapendeza mtoe amri kwamba hakukuwa na committal na mfute kila kilichopo ili leo na mimi nikalale nyumbani kwangu baada ya kuwa nimeshikiliwa kwa siku zaidi ya 150 nalala magereza.
Tusiendeleee kuhangaishana na haya makaratasi waliyotupatia hawa watu wa jamhuri na namna ambavyo mahakama ya ukabidhi chini ya Hakimu Kiswaga ilivyotuharibia mambo.
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 7
Jaji anasema sisi tukizonazo kama Majaji zinaonesha colum ya kwanza tar. 10/04/2025. Na anasoma waliokuwepo siku hiyo.
Upande wa utetezi pia anawasoma waliokuwepo.
Jaji anasema au tukupe kwanza ili uendeleee. ?
LISSU anakubali.
Wameenda kuzitafuta huko ili wamleteee aweze kuendelea.
Sijui kwanini walizificha.😂
Ili tuwe fair tunaomba uzipate kwanza halafu useme unazionaje.
Lissu anasema mkinipa hizo nyaraka nitahitaji dakika 30 tu nipitie na nitakuwa na cha kusema.
Anasimama KATUGA anasema busara tumpe muda wakutosha
Leo Katuga amekuwa mtetezi wa Lissu kwa mara ya kwanza. 🤣🤣🤣🤣
Eti upande wetu tunaangalia fair hearing. Watu wanacheka. 🤣🤣🤣🤣
Katunga anasema wao wanaiachia mahakama apate.
Jaji anasema hiyo nusu saa kwani kaomba nani? Si yeye wewe una shida gani?
Lissu ameulizwa amejibu anasema kwa kuwa leo Katuga ameamua kunipenda sana naomba nipewe lisaa limoja.
Jaji anauliza tukirudi saa 10 unahisi tunaweza kuendelea?
Lissu anasema niko tayari mimi labda nyie majaji mseme hamko tayari.
Jaji amesema tukupe lisaa limoja halafu turudi hapa.
Anamuuliza Katuga yeye anasemaje watu wanacheka sana. 😂😂😂
Katuga amesimama tunasubiri sijui atajibu nini?
Katuga amesimama haongei.
Watu humu mahakamani wanasema KATUGA piga simu uuloze kwamba LISSU aruhusiwe kukaa humu ndani ya mahakama ya lisaa limoja au akasomee lockup? 😂😂😂
Maana Mh. Lissu amesema akipewa hizo nyaraka azisomeee humu humu ndani na Mawakili wanaomsaidia research asiende kule lockup.
KATUGA amefikisha dakika kadhaa hajasema kitu.😂😂😂
Jaji anasema utapelekwa sehemu unayostahili na mawakili watakuja huko. Na saa 10:10 tutarudi hapa kwa pamoja.
Tukutane hapa saa 10 ndugu zangu.
Naomba Repost yako kwenye tweet.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Amemaliza Wakili wa Serikali Mrema
Naona Majaji wanajadili jambo kidogo hapa
Jaji Nduguru anasema kila upande una wajibu wa kuiambia mahakama sio useme navumilia.
Kama kuna jambo lilionekana mapema kuna lina shida ulipaswa kusema na sio kusema nilikuwa navumilia.
Naomba tuwe guided na sheria maana sheria iko hapo.
Wote tunajua kuwa tunabanwa na pleadings na pleading ni ile PO yenyewe.
Msemaji unakuwa kwenye jicho la unasema mambo mengi ambayo yako on face of records.
Anaendelea Mhe. Lissu sasa.
Waheshimiwa majaji nimezungumza sana kuhusu records.
Sasa naomba nirudi kwenye sheria ya ukabidhi.
S. 262 of CPA Nilisema pia kuhsuu kesi ya Dodoli Kapufi kuwa lazima mwenendo wa committal lazima ufuate sheria.
Maombi yaliyopelekwa kwa Jaji mtembwa inasema yaliambatana na viapo viwili.
S. 266[3] ya CPA ndio hoja yangu.
Inazungumzia nini kinapaswa kuwepo kwenye record of proceedings.
Sheria inasema kila records inayopelekwa kwa mshitakiwa inapaswa kujumuisha nyaraka zote ikiwemo zilizotumika kwenye jambo lolote mahakama kuu au mahakama zingine. Hawajaniambatanishia hayo manyaraka yote.
Waheshimiwa majaji hizo nyaraka kupewa mtuhumiwa iko sababu.
Sababu yenyewe iko kanuni ya 5(1) na 5(2) ya kanuni za ulinzi wa mashahidi.
Zinasema mahakama itatoa amri endapo itaridhika kuwa mtu ambae amelindwa kuna hatari atakuwa kwenye tishio la usalama.
S. 263(4) of CPA (CRIMINAL PROCEDURE ACT yaani sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai)
Inamtaka mahakama kumuelezea mtuhumiwa atakapotoa taarifa yake asiwe na hofu na wala asitegemee upendeleo wowote.
Whatsoever he says may be given in evidence at the trial. Lolote atakalosema chochote alachosema kinaweza kutumika kama ushahidi katika trial yaani kesi ya msingi huko mahakama kuu.
S. 265(5) inasema yote ambayo mtuhumiwa atakachosema kirekodiwe na asomewe.
Sasa Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kwenye records kuhusu chochote nilichosema je kiliruhusiwa? Je kilirekodiwa? Je nilisomewa? Twende sasa.
Kwenye rekodi ya Ukonga, kuna maneno ukurasa wa 5 kuna maneno ambayo yamesemwa na mahakama.
Ukisoma sheria hayo maneno yanapswa kuonekana kwneye rekodi na hayapo.
.sheria inasema aambiwe na asome.
Rekodi haioneshi kama aliambiwa. S. 263(5) of CPA nilipaswa kurekodiwa kwenye kila nitakachosema.
Sasa kwneye rekodi hii hakuna mahali kokote mtuhumiwa aliambiwa maelezo yako ni haya na ulichosema ni hiki unachochote cha kuongeza? Sijawahi ambiwa hivyo na hayapo kwenye records.
Na wala sijawahi kuulizwa una chochote cha kuongeza. Mimi sio vyakuongeza hata vyakwangu sikumaliza.
Sasa tuje rekodi ya mahakama hii kuanzia ukurasa wa 93 niliyosema yalipaswa kuwepo hayapo pia hata hayo.
Sijawahi kuambiwa kwamba haya ni maelezo yako. Nakusomea na kuulizwa una nyongeza sijawahi kuulizwa.
Maelezo haya ni ushahidi sio urembo kabisa.
S. 263(6) of CPA maelezo ya mtuhumiwa ni lazima mtuhumiwa aseme ni kweli au sio kweli? Ni maelezo yake na anayakubali.
Hakimu wa ukabidhi ni lazima athibitishe hiyo rekodi. Ukurasa wa 13 wa rekodi ya Ukonga. Pia Ukurasa wa 98 wa rekodi ya mahakama hii angalieni.
Ni lazima nyaraka hizo ziwe certified. Hakimu anasema maelezo hapo juu nathibitisha kuwa ni ya mtuhumiwa na amekiri ni yakwake. Kifungu ameweka 263(3) wakati kiuhalisia kifungu halisi ni 263(6). Anapothibitisha kuwa nilisema mimi na kukiri kuwa ni yangu. Ni wapi nilisema hayo?
Haya yaliyopo yaliandikwa wapi na lipi na lini na nani aliandika?
Sheria iansema mtuhumiwa anapaswa kusign or attest baada ya yale niliyoyasema.
Sahihi yangu wala dole gumba halipo wakati sheria inasema iwe hivyo.
Part 7 itaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 6
Anaendelea kuongea Mhe. Lissu
Kifungu kinasema hicho cha 265(1) of CPA kinasema kama kuna haja ya kuahirishwa kwa shauri basi mahakama itaamuru mtuhumiwa apelekwe gerezani kwa siku 14.
Mahakama inapaswa kusema kwanini kesi imeahirishwa? Kila siku lazima iandike hivyo.
Naomba niwapeleke sasa kwenye hizi records za kutoka Kisutu.
Mimi nilikamatwa tar. 09/04/2025 usiku Mbinga hadi Dar es salaam usiku kwa usiku nakufika Dar es salaam niisafirishwa.
Niliwekwa pale Shimoni police central.
Tar. 10 hiyohiyo nilipelekwa mahakama ya hakimu mkazi kisutu kusomewa hili shtaka la uhaini.
The treason charge was read on 10/04/2025 pale Kisutu.
Nikapelekwa gereza la Keko hiyo tar. 10/04/2025.
Ilisema kesi itakuja tar. 24/04 tena.
Hawa majaji hawamuingilii kabisa Mhe. Lissu tofauti na kule Kisutu labda wabadilike kwenye eneo hilo huko mbele.
Ta. 24/04 wakati naenda Kisutu nilikuwa natokea Ukonga sio Keko tena.
Waliahirisha kesi siku hiyo hadi 19/05/2025 kwamba upelelezi bado.
Walisema pia upelelezi bado ikaahirishwa 02/06 na mara zote nimerudishwa gerezani na leo ni 153 siku niko gerezani.
Tar. 16/06 ikaahirishwa tena, upelelezi bado ndio sababu yao.
Tar. 01/07 nikapelekwa ikaahirishwa tena na mahakama ikasema tar. 15/07 ikaahirishwa tena walikuwa hawajajiandaaa ndio walichosema mahakamani.
Tukarudi tar. 30/07 ikaahirishwa tena na muda wote napelekwa gerezani na ninakaa na wafungwa waliohukumiwa kifo.
Tar. 13/08 tukarudi tena Kisutu ndio upande wa mashitaka wakasema wako tayari.
Ikaahirihswa tena lakini mpaka tarehe 18/08 ndio mahakama ikafanya kile kinachoitwa Commitall hearing.
Sasa Wah. Majaji imeahirishwa mara 10 kuanzia 10/04 na 18/08 mwaka huu.
Muangalie hiyo record kuanzia tar. 10 hiyo yote yaliyofanyika yako wapi kwenye hii record yako wapi?
Yaliyopo humu ni ya tarehe 18/08 tu ndio yameletwa huku mahakama kuu.
Hayo mengine yote yako wapi?
Kwanini wameficha wanaficha nini?
Kesi imeahirishwa zaidi ya mara 10 lakini kwenye hizi records hayapo kabisa.
S. 265(1) ya CPA ukiahirisha hata mara moja lazima uandike sababu za kuahirisha.
Records ziko kimya tena UKIMYA WA KABURINI.
Hazisemi chochote kuhusu hayo mengine yaliyotokea huko nyuma.
Waheshimiwa Majaji naomba niwapeleke kif. Cha 266(3) cha CPA
Amesimama KATUGA anasema Mh. Tunaona kama mwenzetu amepewa proceeding fupi tofauti na tulizonazo na sisi.
Mh. Lissu amemjibu kuwa nilichopewa ndio hicho na ndio ninachokisema hapa Mahakamani kuwa nimepewa nyaraka zinazoanzia tarehe 18/08.
Mahakama imeibua vicheko. 😂😂😂
Jaji anasema wahudhuriaji wawe watulivu tafadhali. Majaji wanaandika kidogo.
Mh. Lissu amewapa proceedings ambazo amepelekewa ili majaji nao wazipitie na kusoma kama kweli ziko sahihi au haziko sahihi.
Kimya kimetanda hapa. Hali ya hewa imeshachafuka.
Kuna wahuni nafikiri walishafanya kazi yao.
Ngoja tuone. 🤣🤣🤣
Majaji wanateta na kushauriana.
KATUGA yeye anazo proceedings zilizokamilika.
Halafu Mh. Lissu wamempelekea gerezani proceedings ambazo hazijakamilika.
Part 7 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 5
Mhe. Lissu anamuuliza Katuganga nani anaevunja amri ya mahakama kati ya Wakili Mkuu wa Serikali na team yake yote ambao wamewaweka wazi wote.
Kile walichoambiwa na Mahakama Kuu wasikifanye ndo wamekifanya, mwenye kosa ni nani hapo mimi au wao?
Walishawaweka hadharani wao.
Nisingejua makazi yao, makabila yao na mitaa yao. Wameleta wenyewe.
Halafu hapa wanasema wakitajwa hawatafika.🤣🤣🤣🤣
Majaji wanateta kidogo hapa.
Ngoja tusubiri.
Kumenuka.
Kazi ishakuwa ngumu hapa.😂
Majaji wanateta.
Kimeumana.
Jaji: anawasha kipaza sauti kinapiga kelele hakiwaki. Vurugu tupu mahakamani.
Anasema tumewasikia.
Mahakama inasema tayari kuna amri ya mahakama hii hii hiyo amri inaendelea kuwa valid kama ambavyo ilivyo.
Kwahiyo tuiheshimu tu hiyo amri maana haijatenguliwa.
Anatuomba pia tuwe watulivu hapa mahakamani.
Mhe. Lissu : Anasema sasa niendelee. Sitawasoma hao watu.
Nawaomba muangalie kwenye rekodi maelezo ya shahidi P2,3,4,5,6,7,8,9,1 na 11.
Maelezo yao yanafuatana na maelezo yote hayo yanakiuka amri ya Jaji Mtembwa kuna mahali wametoa namba za simu, mitaa kazi, familia, hadi idadi ya wake na watoto wamesema.
Amri ilisema wafiche mambo hayo.
Anasimama tena KATUGA anasema pingamizi linahusu mahakama hii haina mamlaka kusikiliza shauri hili.
Anachotuletea hapa ni kama anatoka kwenye point ya kisheria.
Naona mwenzetu anachallenge namna information inavyokuwa challenged.
Tunaweza mkamatia mbali sana tukimuacha hivi au tusimkamate kabisa.
Mahakama 🤣🤣🤣
Katuga anasema tunaweza chukua siku saba au sita.
Anamkaribisha Wakili Job wa serikali anasema upande wetu turejee kwenye shauri la Mahakama ya rufaa Civil Application No 656/2021 ilisema
Pingamizi linapaswa kuwa la kisheria huyu mtu (Lissu) mkimuacha ataenda mbali sana.
Angalieni namna ya kumdhibiti, atatuacha nawaambieni waheshimiwa majaji.
Mhe Lissu : Hoja ya pingamizi lao haina msingi wowote kisheria.
Kama niliyosema jana mahakama hii haina mamlaka juu ya shauri hili on the face of records kuna irregularities.
Kwahiyo kusema kwamba hizo zinaonekana kwenye rekodi ya mahakama zisisemwe hiyo hoja haina maana yoyote.
Pia hiyo kesi waliyoitaja wangejua kesi maarufu ni Mukisa Biscuits anataja citation yote kutoka kichwani anasema hiyo kesi inasema PO ni nini?
Sasa wao wanacite kesi gani sijui hapa. Haya mambo yapo kwenye Mukisa.
Jamaa hii kichwa yake sijui ikoje. 🤣🤣
Ningekuwa naingiza mambo mapya lakini nazungumzia kuhusu makaratasi ambayo nimepewa jana hapa mahakamani wanayakataaje sasa?
Dr. Nshalla ameenda kuongea na Lissu kidogo wamemaliza.
Na majaji nao wanateta.
Mahakama iko kimya majaji wanateta kuna POLISI moja hapa simu yake imepiga wimbo wa BONGE LA DADA ameona sana aibu. 🤣🤣🤣
Lissu anasema sasa nimetaja sheria kuhusu namna committal proceedings inavyopaswa kufanya. Hizi rules ni zao wamezitengeneza juzi hapa wao wenyewe sio mimi.
Tusipozungumzia makosa yao ambayo hawataki nizungumzie wanataka tuzungumzie makosa ya nani? Either nazungumzia nini kama hoja yao iko sahihi maana yake yote yafutwe. Ninachosema ni kwamba toka jana nilikuwa nazungumzia nini? Basi kama ni hivyo futeni hadi niliyosema jana.
Jaji anamuuliza KATUGA kama ana rejoinder.
Katuga anasema anachokufanya yeye ni kwamba yuko aggrieved na maamuzi ya mahakama kwahiyo naomba tena Mahakama jamani Mheshimiwa imuelekeze. Tumeona hadi yamejadiliwa hadi maamuzi ya mahakama kuu. Muelekezeni kuendana na kilichopo tu tafadhali.
Naomba Wakili Mrema aongezee, anasimama na kusema tunatofautiana nae kwasababu baadhi ya mashahidi aliowasema kwamba wangekuwa ni mashahidi wake kwenye proceedings hawapo na amesema kanuni ametungiwa yeye lakini hazipo kwneye proceedings.
Huyu mtu asipodhibitiwa anaingiza mambo mengi hapa. Yanatuvuruga sisi. Hayapo kwenye makaratasi. Anachomeka sana vitu. Anasema jambo moja ukizubaa anachomeka mengine tisa. Adhibitiwe.
Part 6 itaendelea post inayofuata,
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 4
Anaendelea Mhe. Lissu
Sasa hayo ni rahisi
Nataka nianze na Magumu.
Ukurasa wa 86 to 89 kuna amri ya hakimu wa mahakama ya kisutu ulibadilisha kabisa maudhui na maana ya uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kuficha mashahidi.
Mahakama kuu ilitoa amri sita za kinachoitwa kulinda mashahidi ambazo kwa msimamo wangu ni amri za kuficha na kuendesha mashauri gizani.
Hizo amri zote ziko ukurasa wa 7 na Kiswaga alizibadilisha na kuweka amri zake mwenyewe.
Anazisoma zile Order za Jaji Mtembwa kuhusu kuficha mashahidi halafu aje aseme nini alikifanya Mhe. Franco Kiswaga.
Amri za Kiswaga nae akatoa amri zake kuhusu commital page 89.
1. Mashauri haya hayatatangazwa mtandaoni live au kwenye namna yoyote ile na chombo chochote kile. Ni wapi alipata haya mamlaka.
2. Mwenendo ubaki wazi kwa watakaohudhuria na waandishi wataruhusiwa kuingia ndani tu. Sasa je Mahakama kuu iliwataja wapi members wa public kuhusu kuhudhuria mahakamani?
3. Yeyote atakayeenda kinyume na amri hii atachukuliwa kuwa amefanya kosa la kuidharau mahakama.
Haya nayo aliyatoa wapi Kiswaga?
Mahakama kuu ilitoa amri sita ambazo hazihusiani kabisa na haya anayosema Kiswaga.
Televisheni Camera zikazimwa kwasababu ya amri hii na Kiswaga alisema ole wake atakaejaribu kuchapisha mwenendo huu.
Hicho kitendo cha kiswaga ni kinyume cha Sheria.
Katikati ya hii kesi zilitungwa kanuni za ulinzi wa mashahidi za mwaka 2025.
Tangazo la Serikali No. 430/2025. Zilitungwa ili hisia zangu zinaniambia mimi ndio nilitungiwa.
Mahakama ya Ukabidhi haikujali kwamba kuna kanuni za namna hii.
Utaona kwenye ruling ya jaji Mtembwa kwamba Mahakama Kuu Mahakama kuu katika uamuzi wake ilifanya marejeo kwenye hizo kanuni ukurasa wa 5 kutokea juu.
Pia katika ukurasa wa 3 wa uamuzi wa Jaji Mtembwa alizitambua.
Sasa hakimu alipaswa kuzitambua hata mawakili wa serikali walishasema huko nyuma kuwa wanazitambua hizo kanuni.
Cha ajabu sasa kwenye kanuni ya 7(3) na 7(4) zinasema mashitaka yaendeshwe kwa mujibu wa amri iliyotolewa na mahakama kuu na uamuzi wa mahakama kuu unapaswa kuambatanishwa.
Wao hawajaambatanisha amri ya Hussein Mtembwa Jaji wao wameambatabisha amri ya Kiswaga sio ya Jaji tena.
Ujasiri wa Hakimu kubadili uamuzi wa Jaji katika miaka yangu 30 ya kufanya sheria sijawahi kuona kwenye sheria.
Nimeiona mwaka huu kwenye kesi yangu ya Uhaini.
Kwahiyo Waheshimiwa Majaji tulichonacho ni kwamba mnaenda na amri gani ya Jaji mwenzenu Mtembwa au mnaenda na amri ya huyu hakimu Franco Kiswaga.
Chagueni wenyewe.
Sasa Naomba kwa uzito wake niseme kwanini ilifanyika hivi? Kwanini hakimu alibadili uamuzi wa Jaji?
Hilo ombi lilitoka kwa KATUGA na Hakimu akalikubali.
Sasa nataka niseme kwanini alipindua uamuzi wa Jaji?
Mkiangalia kwenye rekodi jibu ni kwamba upande wa Mashitaka haukuwa na lengo lolote la kulinda mashahidi.
Amri ya Jaji Mtembwa ilisema kwamba wasiweke taarifa za mashahidi kama vile majina, namba za simu, cheo, wanapoishi na kadhalika.
Sasa hicho walichokiomba hawakukitekeleza.
Kuna shahidi anaitwa P
Kazi mwandishi wa habari, msambaa, mwanaume. Huyo P anasema mimi ni mfanyakzi wa Jambo TV nilipewa maagizo na Boss wangu John Marwa
Mimi natembea na hawa JAMBO TV kwa miaka zaidi ya miwili unaniambia eti umemficha.
Huyu Msambaa wa Jambo TV nashindwaje kumfahamu? Je umemficha hapa?
Kuna nyaraka inaitwa hati ya makabidhiano na jeshi la Polisi
Anasimama Katuga anasimama anasema anachofanya TUNDU LISSU anavunja amri ya mahakama kuu kwasababu sisi kwa bahati mbaya tulisahau kuondoa hilo jina. Sasa anataka aanze kuwatishia mashahidi hapa.
Katuga anakubali walifanya makosa na anaomba mahakama imzuie Tundu Lissu. Kumtaja huyo shahidi anavunja rekodi ya Mahakama. Azuiwe asimtaje naomba.
Part 5 itaendelea post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 3
Anaendele Mhe. Lissu
Kesi iliahirishwa 15/07 na siku hiyo kulikuwa na ugomvi kuhusu kuahirisha kuanzia page 53 to 60.
Hii siku pia aliandika a reasoned ruling kwneye page 68 to 73 na hiyo ikawa mara ya tatu kwa Hakimu kutoa sababu za msingi za kuahirisha kesi.
Waheshimiwa majaji tar. 30/07 kesi ilikuja na ugomvi wa kuahirisha ukawepo tena mkubwa.
Mtaiona hiyo kwenye page 74-79.
Maneno ya Hakimu kwenye page 79 yanasema "uamuzi kwamba hii kesi ifutwe au vipi tutaitoa tar. 13 August" je hiyo ndio reasonable cause ya kuahirisha kesi?
Hapa napo hakukuwa na sababu za kuahirisha kesi.
Ilipofika hiyo Tar. 13 August wakasema tuahirishe tena na hakimu aliwakubalia bila kutoa sababu.
Hayo yapo ukurasa wa 80 na 85. Kulikuwa na rival submission pale mahakama ya Kisutu.
Kwamba mashauri haya yataoneshwa mtandaoni au la yataamuliwa tarehe nyingine.
Sasa hii nayo ni sababu kweli ya kuahirisha kesi?
Suala la adjournment akaliacha hakulisemea.
Hizo adjournment ambazo zilikuwa granted unlawful, in blantant controversial of sec. 265.
Kila walipoahirisha I paid the price ya kurudishwa gerezani ya kwenda kufungwa na watu waliohukumiwa kifo.
Mtaona kwenye rekodi kuwa niliilalamikia sana inakuwaje mahabusu anachanganywa na condemned prisoner.
So kila walipoahirishwa nilirudishwa kwenda kuchanganywa na wanaosubiri kifo kule magerezani.
Mh. Lissu anaendelea.
Leo amepiga Kombati ya Chama mikono mifupi.
Leo anafuraha jana ni kama alikuwa amekasirika sana.🤣🤣🤣
Maaskari wa Magereza nao wameacha kujifunga usoni.
Leo nawaona wawili tu waliojificha sura. 🤣
Wengine wote tunawaona uso kwa macho.
Sasa tuendelee.
Siku 131 nilikaa hadi siku niliyosomewa commitall ndio maana nilimwanbia asije akawa kama Jaji aliyemuhukumu Jomo Kenyata. Asije akafanana nae.
Jambo lingine dogo linachekesha.
Kwenye rekodi mliyonipa hapa Hakimu Franco Kiswaga page 74 kunaonekana kulikuwa na mashauri tar. 31/07 sasa hiyo tarehe hakukuwa na mashauri yoyote.
Nenda kwenye ukurasa wa 81 hadi 85 kuna submissions. Zilipoanzia ni Tar. 13/August lakini ukweli ni kwamba zilifanyika tarehe 18 August.
Mambo ya Tarehe 18/08 yeye ameandika kuwa yalifanyika tarehe 13/08 sasa natamani kusema kuwa haya yalikuwa ni makosa ya kibinadamu lakini kwa namna yalivyoenda pale kisutu nasema huu nao ulikuwa ni mwendelezo wa uhuni uliofanyika pale Kisutu.
It is not accidentall it is deliberate fabrication.
Part 4 itaendele post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Part 2.
Anaendelea Mhe. Lissu
Waheshimiwa majaji ahirisho la kwanza ni Tar. 10/04/2025.
Page. 2 ya rekodi ya mahakama hii para ya mwisho Mahakama ilisema since this Court has no jurisdiction to hear this matter na hiyo ndio ilikuwa sababu ya kuahirisha.
Hiyo sio sababu ya msingi kuahirisha kesi. Sasa committal Court haina mamlaka huwezi ahirisha kesi kwasababu hiyo maana mahakama hiyo haina hiyo mamlaka.
Hilo ahirisho hali ku comply na kifungu cha 265(1) cha CPA sababu ilipaswa kuwa labda upelelezi haujakamilika na kwasababu zipi ni wasilisho langu hicho kifungu hakikuzingatiwa kabisa.
Ahirisho la 2 la Tar. 24/04/2025. Rekodi ya Mahakama hii mtaona kulikuwa na mvutano mkubwa wa kisheria na huo mvutano upo page 5 hadi page 18 ile rekodi nyingi ya Ukonga haya hayapo kabisa.
Kwasababu ya huo mvutano Mh. Hakimu aliandika uamuzi page 13 hadi 18.
Kilichokuwa kinabishaniwa haikuwa uahirishaji tena ikawa ni inshu ambayo kesi isikilizwe vipi?
Mambo ya kusikiliza kesi kwa njia ya mtandao.
Ahirisho lilisema Tar. 06/05 na mtuhumiwa abaki anashikiliwa.
Hapa napo sababu ziko wapi za kuahirisha hii kesi?
Hazikuwepo kabisa sijui alimpelekea nani au aliziandika kwa nani?
Tar. 06/05/2025 na ikaleta mvutano mwingine mkubwa ambao upo page 19 to 20 ya rekodi ya mahakama hii kulikuwa na submissions za kutosha.
Ahirisho lililotolewa na mahakama lilisema hivi sababu za upande wa mashitaka hazina maana.
Anasema page 20 kwamba duty to prosec to expedite the investigation of the case na ninawataka waje waeleze wamefikia wapi Tar. 19/05
Sasa hii ni sababu ya kuahirisha kesi? I don't think so.
Mahakama imetulia sana. Watu wanasikiliza kwa umakini.
Tunaendelea sasa.
Tar. 19/05 kulikuwa na mvutano mkubwa juu ya adjournment kulikuwa na mvutano mkubwa sana ukisoma 21 to 25 pages ikaahirisha bila sababu yoyote tena.
Nawakumbusha sheria inasema watoe sababu.
Ukisoma page 24 mahakama ilisema this Court is still insist the Republic to expedite investigation.
Kumbe huyu Hakimu alikuwa anatambua wajibu wa jamhuri kuharakisha upelelezi. Lakini ameahirisha upelelezi bila sababu.
Cha ajabu Tar. 02 June walipoomba ahirisho mheshimiwa hakimu alitoa ahirisho na akatoa sababu page 34 to 38 akatoa sababu kwa maoni yangu that was reasonable cause. Naomba nisimuoneee hapa akatoa sababu.
Ikaahirishwa to 16/06/2025 wakaja tena ahirisha lakini hakutoa sababu hiyo sababu. Page 40 to 44.
Mahakama ilisema kwenye page 44 the accused person concerns is taken into consideration and will be handled administratively.
Kwamba amevaa joho la kimahakama eti atadeal na hoja za kisheria kiutawala.
Huyo ni hakimu anasema hivyo. Hizo ni sababu za msingi? Yeye ni mtawala wa wapi huyu Hakimu? Kazi yake ni nini?
Kesi ikaja tena 01/07 vile vile ukawepo ugomvi mkubwa kuhusu adjournment (kuahirisha)
Utetezi mara zote tulilalamikia kuahirisha kwa kesi na mvutano hiyo tarehe ulikuwa mkubwa sana lakini aliwapa adjournment na kwa mara ya pili alitoa sababu siku hii. Page 46 alifanya hivyo.
Part 3 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako kwenye tweet hii.
#UPDATES_KESI_YA_UHAINI
Leo Septemba 9, 2025
Part 1
Kesi imeanza Mhe. Lissu ameingia. Katuga amesimama na kutambulisha jopo lake na mshitakiwa amesema yuko tayari.
Jaji amesema naomba nitoe mrejesho wa tulianzia wapi jana na tuliishia wapi? Ametoa huo mrejesho kuwa sasa tuendelee na lile pingamizi la endapo mahakama hii ina mamlaka ya kuendelea.
LISSU: Mh. Jaji nashukuru, jana nilipewa nafasi nikasome. Sasa hiyo kazi nimeifanya usiku kucha kwahiyo naomba kwa kuanzia nieleze tofauti zilizopo kati ya hizi nyaraka mbili na ili nisiwachanganye ninaposema rekodi ya Ukonga maana yake ni ile niliyoletewa na hakimu wa mahakama ya Kisutu na hakimu FRANCO KISWAGA ndio alimpa Kamishina mSaidizi wa Polisi Rabi Stima.
Rekodi ya Ukonga nina maana ni hiyo nyaraka niliyoletewa na Hakimu Kiswaga.
Kwahiyo nikisema rekodi ya Mahakama hii nitakuwa namaanisha ile niliyopewa jana.
Sasa naomba nianze.
1. Utofauti wa rekodi ya Ukonga ina kurasa 16 tu. Rekodi ya Mahakama hii ina kurasa 101. Sasa hizo kurasa zingine zilikuwa wapi? Nyaraka za mahakama zinawezaje kuwa na utofauti wa namna hii? Katuga hawakumpa hii niliyonayo mimi.
2. Rekodi ya Ukonga haina ile scanned berg (kibox pembeni kulia) inamaanisha ni original. Sasa ya ukonga haina lakini niliyopewa jana inazo hizo scanned berg. Sasa ililetwa na mahakama lakini sio original.
3. Rekodi ya ukonga inaanza tarehe 18/08 na inaishia Tar. 18/08. Kwa kifupi ilianza siku hiyo hiyo na kuishia siku hiyohiyo. Kesi ilianza na kumalizika siku hiyohiyo. Rekodi ya Mahakama hii imeanzia April 10, 2025 na kuishia Agosti 18, 2025. Mliyonipa hapa ilikuwa imekamilika kwa kila kitu.
4. Ukurasa wa 1 wa rekodi ya Ukonga na Ukurasa wa 86 wa rekodi ya Mahakama hii. Ukiangalia ile ya Ukonga page 1 ni kwamba commitall proceedings ilianza immediately. Yani mwanzo pale committal proceedings open, evident on itself lakini kwenye rekodi ya mahakama hii ukurasa wa 86 kulikuwa na ubishani mkubwa sana ambao umerekodiwa. Utaona baada ya corum kuna heading inaitwa Proveedings Mr. Katuga alielezea mambo kadhaaa.... ilianza hivyo. Kinachofuata kuanzia page 86 hadi 89 ni submissions kati ya prosecution na mimi mwenyewe. Rekodi ya ukonga mabishano hayo hayapo kabisa. Lakini hii niliyopewa hapa kila kitu kipo.
Utaona kwa mfano ukurasa wa 87 rekodi ya mahakama hii Hakimu alisema nimezingatia mawasilisho ya pande zote. Na akatambua uamuzi wa mahakama kuu. Mambo hayo kwenye document nikiyoletewa hayakuwepo na hakuambatanisha.
6. Kwenye ukurasa wa 15 wa rekodi ya Ukonga kuna orodha ya mashahidi halafu kuna maneno kuwa na mimi mshitakiwa I WILL CALL THE FOLLOWING WITNESSSES
Lakini kwenye ukurasa wa 100 wa rekodi ya Mahakama hii inasema I will call my witnesses and I will have my Advocates.
Kwenye rekodi ya ukonga na kwenye orodha ya mahakama hii hawajaandikwa mashahidi wangu.
Sio kwamba hawakuwepo, niliwataja lakini nyaraka hizi hazina majina hayo.
1. Samia Suluhu Hassan
2. Isdory Mpango
3. Kassim Majaliwa
Hao wote niliwataja lakini hawakuandika kabisa.
Nitarudi kwenye hilo la majina baadae.
Lakini ieleweke kuwa majina hayo nilitaja mchana kweupe kila mtu alisikia na ilikuwa kwenye Open Court. Aliamua kwa matakwa yake mwenyewe kutokuyaandika.
Hizi nyaraka zote zimetoka Kisutu na zinadai kuwa ni committal proceedings.
Which one is forgery and which one is original.
Mahakama hii inapaswa kujibu why this differences?
Jana niligusia kidogo kwamba kulikuwa na maahirisho mengi sana.
Nilisema yalikuwa zaidi ya 10 hayo maahirisho. Niliposoma usiku nimegundua iliahirishwa mara 13.
Kesi inapoahirishwa kwenye commitall proceedings s. 265(1) the court must record the reason of adjournment and for reasonable cause that adjournment can be granted.
Na hiyo sababu ya msingi lazima iandikwe katika mwenendo.
Sasa nataka nioneshe namna mahakama ya Mh. Franco Kiswaga ilivyoheshimu huo utaratibu wa kisheria.
Part 2 inaendelea post inayofuata.
Naomba Repost yako kwenye tweet hii.