Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemwambia Makamu wa Rais Deogratius Ndejembi kwamba ameteueliwa nafasi hiyo bila kushauriwa.
Akizungumza leo Agosti 29, 2026 mara baada ya kumuapisha Rais Samia amesema “Mheshimiwa Ndejembi katika umri mdogo, tumekutwisha jukumu kubwa, tena bila hata kukushauri, pole sana”
“Uamuzi huo umefanyika baada ya kuzingatia sifa na vigezo alivyonavyo, pamoja na umri wake ambao kwa kweli, bado ni Kijana mwenye nguvu, ari na kasi ya kujituma katika kutekeleza shughuli za Serikali,”
“Sasa kijana, tunakuomba ukakue, si kwa umri, lakini ukue kwa akili, usiwe samaki, Karume aliwahi kutuasa sisi Vijana, akisema “Msiwe kama samaki, kila mnapokua, akili inaharibika.”
#MillardAyoUPDATES
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa imemuachia huru Mfanyabiashara wa Mbao wa Mafinga, Moses John Madege, katika kesi ya Uhujumu uchumi namba 23655 ya mwaka 2025 iliyokuwa ikimkabili kwa tuhuma za kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Shilingi Bilioni 2.5 kupitia madai ya ukwepaji Kodi.
Kwa mujibu wa hati ya Mashtaka iliyowasilishwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Madege alidaiwa kuwa kati ya mwaka 2022 na 2024 aliwasilisha taarifa za uwongo kwenye ritani za biashara yake kupitia mfumo wa TRA, kinyume cha Kifungu cha 84(1)(b) cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi, Sura ya 438, Marejeo ya mwaka 2019. Upande wa Mashtaka ulidai kuwa vitendo hivyo vilisababisha Serikali kupoteza Mapato yanayokadiriwa kuzidi Shilingi Bilioni 2.5.
Katika mwenendo wa shauri hilo, mshtakiwa alitetewa na Wakili Geofrey Mwakasege, huku upande wa Mashtaka ukiwasilisha ushahidi wake mbele ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa.
Akitoa uamuzi wa kesi hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Honorious Kando, alimuachia huru Madege baada ya kuridhika na mchakato wa usikilizwaji wa shauri hilo kwa mujibu wa sheria.
Uamuzi huo unahitimisha rasmi kesi hiyo iliyokuwa ikifuatiliwa kwa karibu kutokana na uzito wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili Mshtakiwa na kiwango kikubwa cha fedha kilichokuwa kinatajwa katika Mashtaka.
#KitengeUpdates
kwenye Ndoa, ndo Sehemu pekee inabidi uache hela ya chakula ata kama wewe na mwenzio HAMUONGELESHANI .,Utaratibu Adui yako anatakiwa ale Ashibe ili mgombane vizuri ...😅😅😅😅