Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mama yetu, Mama Fatma Karume, mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, kilichotokeo leo tarehe 21 Septemba, 2026.
Kifo chake ni pengo kwa familia na Taifa kwa ujumla, kwani alikuwa sehemu muhimu ya historia adhimu ya Zanzibar kuanzia wakati wa harakati za kupigania uhuru, Mapinduzi Matufuku ya Zanzibar na kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Daima tutaendelea kukumbuka, kuenzi na kuheshimu mchango wake katika kuhifadhi kumbukumbu na urithi wetu, pamoja na kuchochea maendeleo ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ya Taifa letu.
Ninatoa pole kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume, familia ya Hayati Sheikh Karume, ndugu, jamaa, marafiki, wananchi wa Zanzibar na Watanzania wote. Ninawaombea Mwenyezi Mungu awajalie subra, faraja na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un.
Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na viongozi mbalimbali kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuondoka nchini, kuelekea Luanda, Angola ambapo anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya Uzinduzi wa Hospitali iliyopewa jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, tarehe 31 Julai,
2026.
Mwakilishi wa Familia ya Baba wa Taifa, Ndugu. Madaraka Nyerere akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Hospitali Kuu ya Rufaa ya Rais Julius Nyerere (Hospital dos Queimados Presidente Julius Nyerere) iliyopo Kilamba, jijini Luanda, Angola, tarehe 01 Agosti, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, Spika wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu, Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Sivangilwa Mwangesi katika picha na Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi Ajira na Mahusiano) Dkt. Evaline Wilbard Munisi, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma tarehe 06 Mei, 2026.
Mheshimiwa Rais na Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Dkt Samia Suluhu Hassan akiendelea kuonyesha uongozi wenye hekima, utulivu na maamuzi yenye maslahi mapana kwa Taifa letu.
CCM imara, Tanzania yenye maendeleo na wananchi wenye matumaini zaidi. ✊✨
Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan inaendelea kuifanya Tanzania kung’aa kwa uwekezaji mkubwa wa nishati ya maji, jua, upepo na gesi. Lengo ni moja tu umeme wa uhakika kufika kila kijiji, kila kitongoji. Hii ndiyo Tanzania ya kazi na maendeleo.