As we look forward to end HIV/AIDS by 2030, International solidarity remains indispensable. The promise of scientific innovation can only be fulfilled when its benefits are accessible to all who need them, regardless of geography or income. We therefore call for renewed global commitment, predictable financing and equitable access to medicines, diagnostics and emerging technologies.
Ubalozi unashukuru kwa taarifa ya ndugu @DuniaSlaveDunia kuhusu Watanzania waliokamatwa nchini Afrika Kusini na kupelekwa Lindela Repatriation Center, kwa kosa la kuishi bila Vibali nchini Afrika Kusini.
Aidha, katika utaratibu wa kawaida wa Ubalozi, tarehe 19 Mei, 2026 Ubalozi ulitembelea Kituo hicho ili kubaini iwapo wapo Watanzania wenzetu wanaoshikiliwa. Zoezi la Utambuzi lilibaini uwepo wa Watanzania 60 wanaoshikiliwa katika Kituo hicho kwa kuishi nchini Afrika Kusini bila ya Vibali. Ubalozi uliwapa Watanzania hao Hati za Dharura za Kusafiria (ETD).
Mwisho, Ubalozi unaarifu kuwa namba alizoweka ndugu @DuniaSlaveDunia kwenye taarifa yake ni za simu ya mezani isiyo ya Ubalozi. Ubalozi unapenda kuarifu kuwa, namba sahihi ya Ubalozi ni +27 12 342 4371. Barua Pepe ya Ubalozi ni [email protected] au [email protected].
Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini
Leo, tarehe 22 Mei 2026, Mhe. Balozi James G. Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Botswana, Lesotho na Sekretarieti ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), amemwakilisha Mheshimiwa Balozi Mahmoud T. Kombo (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, katika Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za SADC ulioanza leo jijini Mpumalanga, Afrika Kusini.
Mkutano huo umefunguliwa rasmi Mhe. Ronald Lamola,l(MP). Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano ambaye is ni Mwemyekirj wa Baraza la Mawazi wa Maaasiai wa Mambo wa Nje wa kilwa Kimataifa wa Afrika Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Mambo ya Nje wa Jumuiya hiyo.
Lengo kuu la Mkutano ni kutathmini hali ya siasa za Kikanda na kimataifa na athari zake katika ukanda wa SADC, ikiwemo namna mabadiliko ya mazingira ya kidunia yanavyoleta changamoto na pia fursa kwa nchi za ukanda wa SADC kujenga uimara, kuimarisha mshikamano wa kikanda, na kuandaa mwitikio wa pamoja.
Leo tarehe 24 Mei, 2026 Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamehitimisha wao Mkutano Maalum uliofanyika kuanzia tarehe 22 hadi 24 Mei 2026 katika Hoteli ya Skukuza iliyopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Kruger nchini Afrika Kusini.
Katika Mkutano huo, Mawaziri hao wamekubaliana Kichua hatua mbalimbali zitakazoisaidia Nchi Wanachama wa SADC kukabiliana na athari zilizosababishwa na changamoto za Kijiopolitiki na kupandisha gharama za bidhaa na huduma.
Mkutano huo Maalum uliitishwa kufuatia uamuzi uliofikiwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri wa SADC uliofanyika Pretoria, Afrika Kusini, mwezi Machi 2026, uliojadili Siasa za Kimataifa na athari zake kwa Nchi Wanachama wa SADC.
Aidha,Mkutano wa Mawaziri uliohitimishwa leo ulijadili masuala mbalimbali kuhusu namna ya kufadhili Utangamano, Uwekezaji, Usimamizi wa Madeni ya Umma na Ukusanyaji we Mapato ya Ndani; masuala ya Viwanda, Biashara na Uongezaji wa thamani; Miundombinu na Usafirishaji; Nishati na Rasilimali za Madini; Masuala ya Kilimo, upatikanaji wa pembejeo za Kilimo, Masoko, pamoja na usalama wa chakula.
Mkutano huo ulihitimishwa kwa Mawaziri kuweka dhamira ya kuendelea kutekeleza Dira ya SADC ya Maendeleo ya mwaka 2050, inayokusudia kufanikisha Maendeleo ya Kiuchumi; Kuinua Hali ya Kipato ya Wananchi; Kuongeza ubora wa maisha, Uhuru, Haki na Amani na Usalama kwa watu wa Ukanda wa SADC.
Ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mhe. James G. Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, aliyemwakilisha Mheshimiwa Balozi Mahmoud T. Kombo (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
#FinalCount
My final count of my four and a half years as Ambassador of the United Republic of Tanzania to the Republic of Korea.
I have paid a visit to the Ministry of Foreign Affairs 43 times. I traveled and met 10 Governors of Provinces and Mayors of Cities across Korea, and done 15 media interviews. I visited 21 Universities and delivered 24 Lectures, and visited and talked with students in 11 schools. I have had 72 Lunch Meetings, 93 Dinner Meetings, and attended 9 Korean weddings.
To attend to all that, I made 52 KTX train trips and 65 flights within Korea. Overall, I had a total of 1,309 activities, 742 of which were meetings, 145 events, and the rest comprised of National Days, luncheons, and dinners.
In the course of four and a half years, I have received in Korea my President, Her Excellency @SuluhuSamia, our then Vice President, then Prime Minister, 17 Ministers, and 50 Senior Official visits. This resulted in 6 bilateral agreements and 24 MOUs signed, with 12 more in progress. All these translated into 2.5 billion USD of soft loans, over 20 million USD in ODA, and many business-to-business visits between the Tanzanian and Korean private sectors.
Thank you so much Mama Yvonne Chaka Chaka and Mr. Sipho Mabuse for your time today, when we celebrated the 62nd Anniversary of the United Republic of Tanzania, here in Pretoria.
*Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan apendekezwa kuwa Kinara wa Umoja wa Afrika wa Nishati Safi ya Kupikia*
Mawaziri wa nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Uchukuzi wamempendekeza rasmi Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Kinara wa Afrika (Champion) wa ajenda ya nishati safi ya kupikia.
Hatua hiyo imefikiwa wakati wa Mkutano wa 5 wa Mawaziri wa nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika unaoshughulikia Nishati na Uchukuzi, uliofanyika jijini Johannesburg, Afrika Kusini, tarehe 30 Aprili 2026.
Katika Mkutano huo, Ujumbe wa Tanzania katika ngazi ya Mawaziri uliongozwa na Mheshimiwa Deogratius Ndejembi (Mb), Waziri wa Nishati. Aidha, Mhe. James G. Bwana, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini alikuwa sehemu ya Ujumbe ulioambatana na Mheshimiwa Waziri Ndejembi (Mb).
Akizungumza katika mjadala kuhusu Programu ya Nishati Safi ya Kupikia Afrika, Mheshimiwa Ndejembi alieleza kuwa mafanikio ya Tanzania katika sekta hiyo yametokana na uongozi madhubuti wa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kusukuma ajenda ya nishati safi ya kupikia ndani na nje ya nchi.
Pendekezo hilo ni ishara ya kutambua mchango wake mkubwa katika kuhamasisha na kuendeleza matumizi ya nishati safi ya kupikia ndani na nje ya nchi, sambamba na juhudi za kupunguza athari za kiafya na kimazingira na kuboresha maisha ya Wananchi wa Afrika, hususan Wanawake na Watoto.
Katika ngazi ya wa
Wataalam, ushiriki wa Tanzania uliongozwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, aliyekuwa akiongoza ujumbe wa sekta katika majadiliano ya kimkakati yanayolenga kuimarisha maendeleo ya miundombinu ya nishati na uchukuzi Barani Afrika.
Wataalam wengine walioshiriki ni Bi. Stella Katondo, Mkurugenzi wa Usalama wa Usafiri na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bw. Mohamed Salum, Mkurugenzi Mkuu wa TASAC.
Maadhimisho ya Miaka 62 ya Muungano jijini Pretoria.
Tarehe 30 Aprili, 2026 Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini umewaongoza Wanadiplomasia na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa nchini Afrika Kusini kusherehekea Miaka 62 ya Muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar.
Hafla ya maadhimisho hayo ilihudhuriwa na Mabalozi kutoka nchi mbalimbali; Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa; Viongozi wa Jumuiya za Watanzania nchini Afrika Kusini; pamoja na Watu Mashuhuri, akiwemo Mwanamuziki Bi. Yvonne Chakachaka pamoja na Bw. Sipho Mabuse (Hotstix), Mtunzi wa wimbo maarufu wa 'Zanzibar beautiful Island of Africa'.
Mgeni Rasmi alikuwa Mhe. Mkhuleko Hlengwa (Mb); Naibu Waziri wa Uchukuzi - kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Afrika Kusini. Ameishukuru Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake kwa Afrika Kusini, wakati wa Ukombozi, na kwa kuwa mbia muhimu wa biashara wa Afrika Kusini, Barani Afrika.
ZANZIBAR KUWA MWENYEJI WA TUZO ZA WORLD TRAVEL AWARDS AFRICA 2026
Kuanzia tarehe 13 hadi 15 Aprili 2026, jijini Cape Town, Afrika Kusini, Tanzania ilishiriki katika Maonesho Makubwa ya Utalii ya World Travel Market Africa 2026. Kupitia ushiriki huo, sambamba na juhudi za kuitangaza Tanzania na vivutio vyake vya utalii, Zanzibar imepata mafanikio makubwa kwa kuchaguliwa kuwa mwenyeji rasmi wa Tuzo za World Travel Awards Africa 2026 zitakazofanyika tarehe 28 Agosti 2026. Hii ni hatua muhimu inayothibitisha nafasi ya Zanzibar kama mojawapo ya vivutio vinavyoongoza duniani katika sekta ya utalii.
Makubaliano haya muhimu yalifikiwa wakati wa maonesho hayo ya World Travel Market Africa jijini Cape Town, na yanaakisi matokeo ya jitihada za pamoja zinazofanywa na Taasisi za Umma na Binafsi katika kuendeleza sekta ya utalii nchini Tanzania.
Aidha, Zanzibar kuwa mwenyeji wa tuzo hizo kutaiwezesha Tanzania kujitangaza zaidi kama kitovu cha utalii wa kipekee, chenye mvuto mkubwa kwa wawekezaji na wageni kutoka mataifa mbalimbali.
Exceptional views for the most beautiful people on earth. 🌍
Join Collins Tarimo on a day trip to the breathtaking Materuni Waterfalls in Moshi. Nature at its finest!
Karibu TANZANIA. 🇹🇿
#TanzaniaUnforgettable#Moshi#MateruniWaterfalls
Leo tarehe 09 Aprili, 2026 Mheshimiwa Frederic T. Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika na kupokelewa na Mhe. Balozi James G. Bwana pamoja na Maafisa wa Ubalozi.
Wakati wa Mkutano wake Ubalozini, Mheshimiwa Waziri Mkuu Mstaafu ameipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kuzitunza vema Balozi za Tanzania nje ya nchi. Aidha, ameupongeza Ubalozi kwa kuendelea kuwa Daraja bora la mahusiano ya kidiplomasia, kijamii na kiuchumi, kati ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Afrika Kusini, Jamhuri ya Botswana pamoja na Falme ya Lesotho.
Today, I was honored to welcome Eng. Charles J. Sangweni, the Director General of Petroleum Upstream Regulatory Authority (PURA), and his delegation at Tanzania High Commission to South Africa.
We discussed various activities executed by PURA in upholding the importance of Oil and Gas Sector in the United Republic of Tanzania. We also discussed matters related to Petroleum upstream operations; monitoring of Petroleum upstream activities, as well as PURA's function in monitoring and regulating all activities relating to Liquefied Natural Gas (LNG) projects for export.
The Benchmarking Visit by a delegation from the National Examinations Council of Tanzania is taking place in Pretoria, Gauteng, from today, 7 April to Friday, 10 April.
This engagement reflects a shared commitment to strengthening cooperation between South Africa and Tanzania, especially in education, through collaboration, knowledge exchange, and the sharing of best practices in assessment, examinations, curriculum development, teacher training, learning and teaching materials, and introducing Kiswahili in South African schools.
During her opening address, Ms Hleki Mabunda, Director for International Relations and Multilateral Affairs at the Department of Basic Education, emphasised that this partnership builds on a cooperation agreement signed to deepen bilateral ties and focus on practical ways to work together going forward, with a special focus on finally advancing discussions on assessments and examinations after progress in other areas of collaboration.
#BenchmarkingVisit #PartnersInEducation #EducationZA #GovZAUpdates
DAR CITY Wanapeperusha vema Bendera yetu 🇹🇿 Michezo ni afya, michezo ni kazi, na Diplomasia ya Michezo inasaidia kuitangaza vema Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kimataifa.
Ubalozi unaipongeza Timu ya Mpira wa Kikapu DAR CITY kwa kutuheshimisha hapa Afrika Kusini kupitia umahiri wenu katika Mpira wa Kikapu wakati wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Barani Afrika.
(Basketball Africa League). Ubalozi upo pamoja nanyi.
“Mhe. Rais Mstaafu Kikwete na Dar City Afrika Kusini”
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na Timu ya Mpira wa Kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Katika mazungumzo na Timu hiyo iliyoambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabit pamoja na Viongozi wengine kutoka Serikalini, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ameipongeza Timu ya Dar City kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya Mashindano, akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya kukua kwa kiwango cha Mpira wa Kikapu nchini Tanzania.
Aidha, amewatia moyo na kuwapa ari Wachezaji wa Dar City kupambana katika Mchezo wao unaofuata mnamo tarehe 31 Machi, 2026 kabla ya kufika fainali, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, kujituma na kujiamini wanapoingia Uwanjani. "Kwa hatua mliyofikia, nina imani kabisa mnaweza kutinga Fainali na hatimaye kubeba Kombe hili", alisema Dkt. Kikwete akizungumza na Wachezaji hao.
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, ambaye amewahi kuwa Mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) huku akiwa mstari wa mbele katika kuendeleza Mchezo huo wakati wa Uongozi wake, ametumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa Uwekezaji mkubwa unaofanyika katika Sekta ya Michezo nchini. Aidha, ameipongeza Wizara yenye dhamana ya kusimamia Michezo pamoja na Shirikisho la TBF kwa kusimamia vizuri maendeleo ya Mpira wa Kikapu, huku akibainisha kuwa mafanikio ya Timu ya Dar City ni ya Watanzania wote.
Mheshimiwa Dkt. Kikwete yupo nchini Afrika Kusini kwa Ziara ya Kikazi ambapo tarehe 29 Machi, 2026 alikutana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, kama sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya Kikanda akiwa kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC, pamoja na jukumu lake jipya chini ya Umoja wa Afrika la kusaidia kutafuta suluhu ya Mgogoro wa Sudan Kusini.
📍 Pretoria
▪️“JK na Dar City Afrika Kusini”
Rais Mstaafu Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Panel of Elders - POE), na Mwakilishi wa Ngazi ya Juu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika katika juhudi za kutatua mgogoro wa Sudan Kusini, amekutana leo na timu ya mpira wa kikapu ya Dar City inayoshiriki Michuano ya Ligi ya Mpira wa Kikapu Afrika (Basketball Africa League (BAL) 2026, inayoendelea jijini Pretoria, Afrika Kusini.
Katika mazungumzo na timu hiyo iliyoambatana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabit pamoja na Viongozi wengine kutoka Serikalini, Rais Mstaafu Dkt. Kikwete ameipongeza Timu ya Dar City kwa kufikia hatua hiyo muhimu ya mashindano, akieleza kuwa mafanikio hayo ni ishara ya kukua kwa kiwango cha mpira wa kikapu nchini Tanzania.
Aidha, amewatia moyo na kuwapa ari wachezaji ya kupambana katika mchezo wao mmoja uliosalia kabla ya kufika fainali, akisisitiza umuhimu wa nidhamu, kujituma na kujiamini wanapoingia uwanjani. "Kwa hatua mliyofikia, nina imani kabisa mnaweza kutinga fainali na hatimaye kubeba kombe hili, labda itokee miujiza", alisema Dkt. Kikwete akizungumza na wachezaji hao.
Rais Mstaafu Dkt. Kikwete, ambaye amewahi kuwa mlezi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF) huku akiwa mstari wa mbele katika kuendeleza mchezo huo wakati wa uongozi wake, ametumia fursa hiyo pia kutoa pongezi kwa dhati kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa unaofanyika katika sekta ya michezo nchini. Aidha, ameipongeza Wizara yenye dhamana ya kusimamia Michezo pamoja na Shirikisho la TBF kwa kusimamia vizuri maendeleo ya mpira wa kikapu, huku akibainisha kuwa mafanikio ya timu ya Dar City ni mojawapo ya matunda ya Serikali kuwekeza katika michezo.
Mheshimiwa Dkt. Kikwete yupo nchini Afrika Kusini kwa ziara ya kikazi ambapo amekutana na Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, kama sehemu ya kutekeleza majukumu yake ya kikanda akiwa kama Mwenyekiti wa Jopo la Wazee la SADC, pamoja na jukumu lake jipya chini ya Umoja wa Afrika la kusaidia kutafuta suluhu ya mgogoro wa Sudan Kusini.