Mamlaka ya nchi ni ya wananchi, na viongozi wanayashikilia kama amana tu, kwa niaba ya wananchi — Maalim Seif Sharif Hamad
#WananchiKwanza#UrithiWaMaalimSeif
Yaleli Kipenzi - Kalamu ya Mohammed Ghassani @GumzolaGhassani akimkumbuka Kiongozi wa Wazanzibari asiyesahaulika.
Miaka Mitano bila ya Maalim Seif (2021 - 2026)
Hawli ya Al Marhum Maalim Seif kesho Jumanne, tarehe 17 Februari, 2026, Saa 10:00 Alasiri, kwa kisiwa cha #UNGUJA itafanyika MSIKITI BARZA, MKUNAZINI.
Tujitokeze kwa wingi kwenda kumuombea Kipenzi chetu.
#MaalimSeifLegacy
Hawli ya Al Marhum Maalim Seif kesho Jumanne, tarehe 17 Februari, 2026, Saa 10:00 Alasiri, kwa kisiwa cha #PEMBA itafanyika MSIKITI WA NYALI, MTAMBWE.
Tujitokeze kwa wingi kwenda kumuombea Kipenzi chetu.
#MaalimSeifLegacy
"All over the world the winds of change for a just cause always come at higher price. People go through political hardship and sacrifice to achieve their rights and democratic freedoms. Ultimately, it is the taste of a hard-won Struggle for Democracy that prevails over the rest."
- Maalim Seif Sharif Hamad
19 May, 2020
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad akiwa na Dr. Salim Ahmed Salim wakati wa ufunguzi wa jengo la Chuo cha Mwalimu Nyerere, (Kampasi ya Zanzibar) mwaka 2012. Maalim Seif na Dr. Salim walikuwa marafiki na zama wakiwa CCM walikuwa pamoja kwenye harakati zao.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza Chatham House (Royal Institute for International Affairs), huko London, Uingereza mwezi Julai, 2016. Kulia kwake ni Dr. Alex Vines, Mkurugenzi wa Masuala ya Afrika kwenye Taasisi hiyo.
#MaalimSeifLegacy - Mwezi Disemba 2018, Maalim Seif Sharif Hamad aliandaa Mkutano wa Kutathmini Mwelekeo wa Demokrasia Tanzania ambapo aliwaalika viongozi mbali mbali wa vyama vikuu vya siasa na wanaharakati wa masuala ya demokrasia na utawala wa sheria. Mkutano huo ulifanyika Hoteli ya Verde, Zanzibar.
Pichani anaonekana akiwa pamoja na baadhi ya washiriki ambao ni Mohamed Ahmed Al Mugheiry (maarufu kama Eddy Riyami), Mansoor Yussuf Himid, Ismail Jussa na Zitto Kabwe.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad akinong'ona jambo na Mhe. Juma Duni Haji wakati wakiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Chadema uliompitisha Mhe. Edward Lowassa kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Juma Duni kuwa Mgombea Mwenza kupitia muungano wa vyama vya upinzani (UKAWA) mwaka 2015.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad aliziteka nyoyo za Wazanzibari ambao walimkubali kama Kiongozi wao na Alama ya Harakati zao za kudai Mamlaka Kamili ya nchi yao. Pichani ni bango la kampeni la Maalim Seif likiwa limewekwa ndani ya nyumba mojawapo ya Mji Mkongwe, Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad wakati huo akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar akitembelea mojawapo ya skuli wakati alipofanya ziara kukagua kazi za Wizara ya Elimu mwaka 2012.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad wakati huo akiwa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, akiwajulia hali wagonjwa wakati alipotembelea hospitali mbali mbali zilizo chini ya Wizara ya Afya mwaka 2011.
#MaalimSeifLegacy - Maalim Seif Sharif Hamad akimtambulisha Eddy Calipso kwa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Dk. Amani Karume baada ya kumalizika Hafla ya Maulid ya Mtume Muhammad (SAW) yaliyofanyika Ukumbi wa Salama katika Hoteli ya Bwawani, Zanzibar mwaka 2010.
As we step into 2026, we extend our sincere gratitude to our supporters, partners, volunteers and beneficiaries for standing with us throughout the past year. Your trust and commitment continue to inspire our work. Wishing you a year of peace, progress and shared impact. Happy New Year 2026.
Uchaguzi Mkuu nchini Tanzania utakuwa wa tofauti mwaka huu, hasa visiwani Zanzibar ambapo kwa mara ya kwanza katika historia yake uchaguzi wa vyama vingi utafanyika bila kuwepo kwa mwanasiasa nguli Maalim Seif Sharif Hamad.
Je, ni kwa kiasi gani kutokuwepo kwa mwanasiasa huyo kumeathiri siasa za Zanzibar?