Wanajeshi watano waliokuwa kwenye helikopta ya Jeshi la Anga iliopata ajali wakati wa mazoezi eneo la Eskisehir wamefariki mashahidi – Wizara ya Ulinzi ya Uturuki
Mkuu wa Ujasusi wa wapiganaji wa RSF, Al-Tayeb Jabara, amejiunga na upande wa jeshi la Sudan, vyombo vya habari vimeripoti siku ya Jumanne.
Katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na mwanaharakati wa Sudan, Jabara alitangaza uamuzi wake wa kuondoka RSF, akiomba radhi watu wa Sudan kwa kujiunga na kundi hilo la wapiganaji dhidi ya taifa.
Jabara alisema kuwa awali amewahi kufanya kazi katika ofisi ya kamanda wa RSF Mohamed Hamdan Dagalo, ambaye pia anajulikana kama Hemedti, katika Ikulu mjini Khartoum na baadaye Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini.
Senegal wamerudishiwa ubingwa wao wa AFCON 2025 baada ya Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) siku ya Jumanne kukubali rufaa yao ya kupinga kupokonywa taji hilo.
Senegal ilipinga uamuzi wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) wa kutangaza kuwa Morocco ndiyo mabingwa wa fainali hizo, licha ya Senegal kuwafunga wenyeji hao 1-0 katika mechi iliyochezwa mjini Rabat mwezi Januari.
Uingereza imetangaza vikwazo dhidi ya maafisa wa ngazi za juu wa kundi la wapiganaji la Houthi, ikiwa ni mwitikio kwa “uhasama mpya” ndani ya Yemen na dhidi ya Saudi Arabia.
Tume ya Uchaguzi nchini Kenya (IEBC) inasema kutangaza matokeo mubashara kutoka kwenye vituo vyote 50,000 itakuwa ni gharama kubwa kwa taifa hilo.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Erastus Ethekon anasema iwapo watatakiwa kufanya hivyo, basi watalazimika kuwa na kamera kila mahali na hilo litamaanisha kuajiri watu 50,000 kwa ajili ya kazi hiyo, na kwa sasa Tume haina uwezo huo.
Ethekon anasema wataendelea kurusha matangazo mubashara kutoka katika kituo cha kuhesabu kura kitaifa kwa Uchaguzi huo wa Agosti 10, 2027.
Zimbabwe imeanzisha mahakama zinazotembea ili kusogeza huduma ya mahakama karibu zaidi na wananchi.
Mahakama hiyo inapatikana ndani ya lori ambalo limebadilishwa kuwa mahakama inayofanya kazi kikamilifu.
Tume ya Huduma za Mahakama ya Zimbabwe (JSC) ilizindua mpango huo ili kusaidia kupunguza msongamano wa kesi, hasa katika baadhi ya maeneo yenye idadi kubwa ya watu jijini Harare.
Burkina Faso imeanzisha kituo maalum kitakachotoa mafunzo ya teknolojia. Chuo hicho Academy of Faso kilichopo eneo la Padre kimejengwa katika eneo la hekta 60 ni maalumu kwa kutoa mafunzo ya uhandishi katika madini, sayansi ya nyuklia na utengezaji wa ndege.
Uzinduzi huu unakuja wakati ambapo nchi hiyo iko mbioni kuleta mabadiliko makubwa katika sekta mbalimbali ikiwemo madini baada ya kuzindua kiwanda cha kusafisha dhahabu mwezi Septemba 2026.
Wanajeshi 23 wa Israel wamejiua mwaka huu, ikiwa ni idadi kubwa tangu mwaka 2010, na kuashiria ongezeko tangu Oktoba 7, 2023 pindi Israel ilipoanzisha mauaji ya halaiki huko Gaza, Palestina, imeripoti Haaretz
Dahabaya Oumar Souni, mke wa Rais wa Chad, Mahamat Idriss Deby Itno ni mwandishi wa habari na mtaalamu wa mawasiliano kutoka Chad, Alijipatia umaarufu kupitia uhusiano wake na ofisi ya rais nchini humo kuanzia wakati wa baba ya mumewe aliyekuwa rais wa nchi hiyo Idriss Deby.
Souni alichukua wadhifa kama Mke wa Rais wa Chad kuanzia Aprili 21, 2021, kufuatia kifo cha Rais Idriss Deby, na mume wake Mahamat Idriss Déby Itno, kuchukua madaraka.
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe amesisitiza kuwa, uamuzi wowote utakaotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) kuhusu matokeo ya mchezo wa fainali ya AFCON 2025 kati ya Morocco na Senegal, uheshimiwe na pande zote, ikiwemo CAF yenyewe.
Motsepe ametoa kauli hiyo, ikiwa imebaki saa chache kabla ya CAS kutoa uamuzi wake, ambao huenda ukahitimisha mvutano wa kisheria kati ya Senegal na Morocco uliodumu tangu fainali iliyochezwa Januari 18, 2026, jijini Rabat.
Mahakama Kuu ya Kenya imepinga tozo ya asilimia mbili kwenye mfumo wa usimamizi wa huduma za afya nchini humo (HIMS), ikidai kuwa inakiuka katiba kwa kutokuwa shirikishi kwa umma.
Akisoma hukumu yake kwa njia ya mtandao, Jaji Reuben Nyakundi alisema kuwa serikali ya nchi hiyo ilishindwa kuonesha ushirikishwaji wa wananchi kuhusu kiwango cha tozo hiyo na kikokotoo kilichotumika kuanzisha tozo hiyo.
Hata hivyo, jaji huyo, ametoa muda kwa serikali kutatua changamoto ya kisheria katika shauri hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Novemba 24, 2026, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Tanzania Bara, John Heche amesema kuwa chama hicho cha upinzani kitaingia kwenye maridhiano, iwapo tu kutakuwa na mpatanishi huru kwenye mchakato huo.
Kiongozi wa zamani wa upinzani nchini Burundi, Agathon Rwasa ameweka wazi nia yake ya kugombea kiti cha urais wa nchi hiyo, kama mgombea binafsi wakati wa uchaguzi wa rais utakaofanyika Mei 3, 2027.
Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden na mkewe, Jill Biden, walionekana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Philadelphia huko Pennsylvania siku ya Jumapili Novemba 22, 2026.
Biden alionekana akitmbea kwa taaabu, akipita katika jengo la uwanja wa ndege akiwa kwenye chombo cha usafiri cha umeme.
Rais huyo wa zamani, mwenye umri wa miaka 84, aligunduliwa kuwa na saratani ya tezi dume mwezi Mei 2025 na hajaonekana hadharani kwa muda mrefu.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi amesema siku ya Jumatatu kuwa rasilimali ya madini adimu yaliyopo nchini mwake sharti yanufaishe taifa hilo.
Akizungumza katika jukwaa la uchimbaji madini Makutano Mining Forum, amekosoa mfumo ambao nchi inasafirisha madini ghafi lakini faida inayopata ni ndogo baada ya madini hayo kuchakatwa na kuongezewa thamani.
Onesho kubwa zaidi la sanaa ya kisasa barani Afrika, kwa jina la Dakar Biennale, limewakutanisha wasanii na wabunifu 79 kutoka Afrika na diaspora wanaoonesha ubora na ubunifu wa kazi zao katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.
Tukio hilo linalofanyika chini ya kaulimbiu “Kupambana na Udhaifu: sanaa za ukarabati na mikakati ya kukabiliana na mshtuko” linachunguza jinsi sanaa inavyoweza kuchangia katika kuleta mshikamano wa kijamii na kupona wakati wa shida.
Onesho la Biennale, lilianza Novemba 19 na litaendelea hadi Disemba 19.
Tanzania imepanda kwa nafasi tatu hadi ya 112 duniani, kwa mujibu wa orodha ya viwango vya soka, iliyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), hivi karibuni.
Hali kadhalika, Tanzania ni ya tatu kwa ubora wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki, mbele ya Kenya, ambayo inashika nafasi ya 115 duniani, na ya nne Afrika Mashariki.
Kwa upande wake, Uganda, inashika nafasi ya pili katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku ikiwa ni ya 89 duniani.
DRC imeendeleza ubabe wa soka Afrika Mashariki, ambapo pia imeshika nafasi ya 39 duniani, wakati Somalia inashika nafasi ya 199 ulimwenguni, ikishika mkia katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Nahodha wa zamani wa meli ya kitalii ya Costa Concordia, Francesco Schettino, ameachiwa kutoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 16 jela.
Schettino amechiwa huru baada ya kukaa gerezani kwa miaka tisa, kufuatia ajali ya kuzama kwa meli hiyo iliyosababisha vifo vya watu 32 nchini Italia mwaka 2012.
Schettino alitolewa kutoka gereza la Rebibbia la jijini Roma, na kwa sasa atakuwa chini ya uangalizi maalumu katika eneo la Campania, Italia.
Januari 13, 2012, meli ya Costa Concordia ikiwa na takribani abiria 3,200 pamoja na zaidi ya wafanyakazi 1,000 iligonga mwamba wa baharini karibu na Kisiwa cha Giglio katika Bahari ya Mediterania na kuanza kupinduka.
Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu 32 huku Schettino, akipatikana na hatia ya kusababisha vifo hivyo na kuitekeleza meli hiyo hiyo ya kitalii.
Mamlaka katika jimbo la Niger nchini Nigeria imesema kuwa ripoti za uchunguzi zimethibitisha watu 38 waliuawa na kuzikwa kufuatia mashambulizi ya kulipiza kisasi mwishoni mwa juma.
Mauaji hayo yalifuatia shambulio la mapema Jumamosi katika kijiji cha karibu cha Lumman-Ba’are, ambapo serikali ya jimbo ilisema watu wenye silaha waliwaua watu watano, akiwemo mkuu wa kijiji, wakati wa swala za asubuhi.
Baadhi ya wakazi wamedai kuwa washambuliaji walitumia bunduki na mapanga na kuchoma moto majengo huku watu wakiwa ndani.
Wafuasi wa chama cha Indian Youth Congress (IYC), tawi la vijana la chama kikuu cha upinzani cha Congress, walifanya maandamano katika ofisi za Meta nchini India, na kuilamu kampuni hiyo kwa kufuta baadhi ya maudhui yaliyowekwa na kudhibiti akaunti za mitandao ya kijamii ya wanaharakati.
Maandamano yametokea katika ofisi kuu za Meta zilizopo Gurugram, karibu na New Delhi, Hyderabad na Mumbai. Polisi inawashikilia waandamanaji kadhaa.