Dkt. Samia Suluhu Hassan akiapishwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, George Mcheche Masaju kuwa Rais wa Tanzania katika sherehe zilizofanyika Uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma leo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa silaha za jadi Mkuki kutoka kwa Mzee Ndijina Ndilanza Ndilito, mwakilishi wa wazee wa Tanzania Bara pamoja na ngao kutoka kwa Bi. Ubwa Hamis Ally mwakilishi wa Wazee wa Zanzibar kama ishara ya kulinda na kuitetea Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kuapishwa katika uwanja wa Gwaride, Chamwino Ikulu mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan akihutubia Taifa mara baada ya kuapishwa katika sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Gwaride Ikulu Chamwino mkoani Dodoma tarehe 03 Novemba, 2025.
Mabadiliko Makubwa Kwenye Sheria 57 Zilizotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mwezi Februari 2024
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, katika kikao chake kilichofanyika mwezi Februari 2024, lilipitisha mabadiliko makubwa katika Sheria 57. Mabadiliko haya yanalenga kuboresha utekelezaji wa sheria hizo ili kuendana na mahitaji ya sasa ya kijamii, kiuchumi, na kisiasa.
#katibanasheria #MSLAC #SSH #kaziiendelee #SisiniTanzania #nchiyangukwanza #matokeochanya