@AnnaTibaijuka Kudiriki kumuhukumu Lissu kesi ya uchochezi kwa maelekezo ya Ikulu ya Samia ni kuwaonyesha wananchi wote kukubali kuwa hakuna mahakama huru na kuwa sote ni watumwa katika nchi yetu. Ni kufunga domo. Kwamba ukihoji, ukitoa maoni utakamatwa. Utapotezwa. Utauawa.
6.11.2026: Hukumu ya TUNDU LISSU NA KUMBUKUMBU YA KESI YA MWALIMU NYERERE YA MWAKA 1958. HISTORIA INATUFUNDISHA NINI?
Leo, tarehe 6 Novemba 2026, Tundu Lissu ameshinda kesi ya uhaini lakini mahakama ikasema amepatikana na hatia ya uchochezi (incitement) na kuhukumiwa kifungo cha miaka 4. Tunamshukuru Mungu kwa kesi ya uhaini kutupiliwa mbali na kumpongeza Lissu kwa umahiri na ujasiri wake hadi kujitetea. Lakini hukumu ya uchochezi inasikitisha, inafikirisha na inatukumbusha historia ya Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, ambaye naye mwaka 1958 alikutwa na hatia ya jinai ya kashfa (criminal libel) wakati wa harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Makosa haya mawili ni tofauti kisheria, lakini kesi hizi zinafanana katika jambo muhimu: zote zilihusu kiongozi mkuu wa upinzani aliyeshtakiwa na Serikali kutokana na kauli zake za kisiasa.
Turejee historia.
Tarehe 27 Mei 1958, Mwalimu Nyerere alichapisha makala katika gazeti la Sauti ya TANU, Toleo Na. 29, akiwakosoa Wakuu wawili wa Wilaya wa Serikali ya kikoloni kwa madai ya kutumia madaraka yao vibaya na kuihujumu TANU.
Akafunguliwa kesi ya jinai Na. 2207/1958 chini ya kifungu cha 187 cha Kanuni ya Adhabu (Penal Code). Serikali ya Uingereza ilitoa maelezo kuhusu mashtaka hayo katika Bunge lake (House of Commons) tarehe 26 Juni 1958.
Nyaraka za UN zinathibitisha kwamba Mwalimu alikutwa na hatia katika mashtaka mawili na kuhukumiwa kulipa faini ya shilingi 3,000 za Afrika Mashariki, sawa na pauni 150 za wakati huo, au kifungo cha miezi sita. Alilipa faini tarehe 12 Agosti 1958 na hakukata rufaa.
Kesi hiyo ilizua mjadala mkubwa. Wanaharakati wa kupigania uhuru huko London walihoji iwapo Mwalimu angepata haki katika mahakama za kikoloni na kudai kuwepo kwa waangalizi huru. Serikali ilikataa, ikisisitiza kuwa uamuzi wa kufungua mashtaka ulikuwa chini ya mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Miaka 68 baadaye, tunajikuta tena tukitafakari maswali kuhusu uhuru wa kisiasa, matumizi ya sheria za jinai na nafasi ya mahakama katika mfumo wa kidemokrasia.
Pamoja na hukumu ya mwaka 1958, Mwalimu Nyerere aliendelea na harakati zake hadi Tanganyika ilipopata uhuru mwaka 1961.
Funzo muhimu ni kwamba hukumu ya jinai dhidi ya kiongozi wa kisiasa si lazima iwe mwisho wa safari yake ya kisiasa. Historia inaonesha umuhimu wa kuendeleza majadiliano (dialogue) badala ya mapambano na vurugu (confrontation).
Kwa wanaothamini demokrasia, mfumo wa vyama vingi, haki za binadamu, uhuru wa kujieleza na utawala wa sheria, hukumu ya uchochezi dhidi ya kiongozi mkuu wa upinzani inaibua maswali mazito yanayohitaji mjadala mpana wa kitaifa.
Je, mipaka kati ya ukosoaji halali wa Serikali na uchochezi wa jinai ikoje?
Je, mwanasiasa awe mpinzani au wa chama tawala atakosoa je Serikali au kudai maboresho au mageuzi bila kuhofia kutafsiriwa kuwa mchochezi?
Je, wananchi watawezaje kudai haki zao kwa nguvu ya hoja bila kuonekana wanachochea uvunjifu wa amani?
Walimu na wanataaluma tutawezaje kufundisha, kuchambua sera, kutoa mapendekezo na kukosoa mifumo ya utawala bila kuhofu kuitwa wachochezi?
Viongozi wetu wa dini watawezaje kutekeleza wajibu wao wa kinabii wa kukemea maovu na kusimamia haki bila kuonekana wanachochea waumini wao?
Uhuru wa kujieleza una mipaka yake na hauhalalishi haki ya kukashfu, kuchochea vurugu au uhalifu. Lakini ni muhimu sana kuweka mipaka iliyo wazi kati ya uchochezi wa jinai na ukosoaji halali wa kisiasa.
Iwapo sheria za jinai zitatumika kudhibiti ukosoaji halali wa kisiasa au kitaalamu, tunaweza kujikuta tunadhoofisha demokrasia, haki za binadamu, kuongeza hofu na kuzidisha mkwamo wa kisiasa na kiuchumi badala ya kuutatua.
Hukumu ya leo inatupa sababu nyingine ya kujadili kwa kina uhuru wa kujieleza, uhuru wa mahakama, haki za raia na za vyama vya upinzani na mipaka ya matumizi ya sheria za jinai katika siasa.
Ninarejea msisitizo wangu wa muda mrefu kuhusu falsafa ya Rais Samia ya 4Rs. Tujenge utamaduni wa kusikilizana na kukosoana kwa hoja
TUJISAHIHISHE
Mwaka 1957 wakoloni wazungu walimfungulia Mwalimu Nyerere kesi ya uchochezi.
Kwenye hiyo kesi wakoloni wazungu walimkuta na hatia mwalimu Nyerere. Pamoja na kumkuta na hatia Mwalimu wakoloni hawakumfunga Nyerere gerezani bali walimlipisha faini na akaenda nyumbani.
Miaka zaidi ya 70 baadae, mahakama chini ya majaji kina Ndunguru na Jaji mkuu Masaju.
Yenyewe imejiundia kosa, imejitafutia ushahidi, imemfunga kiongozi wa upinzani nchini tena kwenye kosa lenye faini.
Ccm na serikali ya Samia Suluhu Hassan ni makatili kuliko wakoloni wazungu.
Historia itawaweka mnapostahili.
@AnnaTibaijuka Wow, Sikujua NCCR MAGEUZI ina makamu mwenyekiti mwanamke. Na kumbe aliondolewa ofisini kibabe pamoja na kurejeshwa na mahakama na amri ikadharauliwa na maisha yakaendelea. Hii nchi tunaipeleka wapi? Utawala wa sheria uko wapi??
Makamu Mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI. Pongezi kufikisha miaka 70 ya kuzaliwa. Mungu akubariki kwa mapambano yako mengi hasa juhudi za kupigania utawala bora ndani ya vyama vya siasa. Ubarikiwe.
Hakuna mtu anaeweza kukwamisha watu kuja kutoa maoni….
Watanzania wanajiuliza kuhusu kuaminika kwenu Nyie tume… Kama Watanzania wangekua na Imani na nyie hakuna mtu mwenye uwezo wa kuwazuia kuja kutoa maoni..
Watanzania wanajuliza je nyie mnaweza kuja na ripoti tofauti na ambacho aliewateua amekwisha sema?
1. Walioandamana walilipwa fedha
2. Wanatumiwa na walitumiwa na mabeberu
3.Sio Watanzania ni watu kutoka Mataifa ya nje.
4. Waliandamana kwa mkumbo tu hawajui walichokua wanadai na hata madai yao hayapo.
Je nyie mnaweza kutoa ripoti tofauti na mawazo ya hawa waliowapa kazi?
Chuki mnayojenga mlipuko wake utakua wa kishindo kikubwa mno..
Mlipomteka Mdude, Soka , Ben Saanane na wengine mliamini kila mtu atajificha ndani na kunyamaza…
Sasa wanaongea mpaka Wazee..
Kufikiria kwamba mtachukua watu mpaka wote wawapigie magoti ni kujidanganya mno..
Kama Hitler, na madikteta wengine hawakufanikiwa kwa mbinu hii, historia inatuambia kwamba hakuna anaeweza kushinda kwa kujaza watu hofu..
Muachieni huyu kijana Nicodemus Julius Loyore.
Ukimsikiliza Mwigulu na ccm wenzake wanazungumza… utafikiri Nchi hii ni mali yao binafsi na sisi wengine wote ni wapangaji!!
Unawezaje kuiba uchaguzi, ukajitangaza kwa nguvu, ukaua maelfu ya watu na wengine ukawafanya walemavu ili uwe kiongozi usie na ridhaa wala kura za umma.
Alafu unapata ujasiri wa kukemea wale wanaokwambia umeiba, wale wanaotaka uchaguzi uwe huru na haki, wale wanaotaka Mwananchi ndie awe na sauti ya kuweka kiongozi anaemtaka.
Tena unamwambia analeta vurugu na kuchafua Nchi…
Hivi alieiba uchaguzi na kuua watu na yule anaesema utaratibu ufuatwe nani analeta vurugu? Nani anatumika kuchafua Nchi?
Mwigulu Nchi hii sio mali yenu binafsi, wananchi wana haki na mamlaka yote na Nchi yao..
Acheni kutishia wananchi.