Mwenge wa Uhuru umepokelewa Wilaya ya Mvomero eneo la Sangasanga Mzumbe tarehe 13.04.2025 kutoka Manispaa ya Morogoro na kukimbizwa umbali wa kilomita 98 katika Tarafa ya Mlali Kata 4 na Vijiji 11 vya Halmashauri na umepita katika miradi 7 yenye thamani ya TShs. Bilioni 1.06 .
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mwl. Linno Mwageni ametoa agizo kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa shule mpya ya sekondari katika Kata ya Mkindo kuhakikisha kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati uliopangwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mvomero Mwl. Linno Mwageni akikabidhi pikipiki kwa waratibu wa chanjo pamoja na wasimamizi wa miradi ya usafi wa mazingira katika kata za Mlali, Mgeta, Dakawa na Mvomero HQ.
Zoezi hil limefanyika Januari 16,2025 katika Ofisi za H/W
SHIRIKA LA SAWA LAPONGEZWA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU
Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imepongeza juhudi za Shirika la SAWA WANAWAKE TANZANIA katika kuboresha miundombinu ya elimu Wilayani humo kwa kujenga madarasa, vyoo na miundombinu ya maji.
Shamrashamra za Wananchi wa Gairo mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuwasili katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuwahutubia tarehe 02 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizindua Daraja la Berega, Wilayani Kilosa katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi iliyoanza Mkoani Morogoro leo tarehe 02 Agosti, 2024.
Sehemu ya Wananchi wa Dumila Mkoani Morogoro wakiwa kwenye Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, tarehe 02 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi wa Dumila katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wafanyabiashara wa mbogamboga na matunda mara baada ya kusimama eneo la Dumila darajani katika muendelezo wa ziara yake ya Kikazi Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.
Wafanyabiashara wa mbogamboga na matunda wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mara baada ya kusimama katika eneo la Dumila darajani, Kilosa Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akifurahiajambo na Watoto wa Dumila mara baada ya kuwasalimiaWananchi wa eneo hilo Kilosa Mkoani Morogoro tarehe 02 Agosti, 2024.