IMETHIBITISHWA Na vyombo vya Habari vya Iran kuwa KHAMENEI kiongozi Mkuu wa Iran ameuawa. Hivyo ni Rasmi sasa utawala wa Kiimla wa Ayatollah Khamenei umeanguka.
DONALD TRUMP athibitisha kuuwawa kwa Kiongozi Mkuu wa IRAN Ayatollah Khamenei. Kwa upande mwingine Iran inaendelea kukanusha vikali wakidai kiongozi wao bado yupo hai. Tuendelee kusubiri taarifa zaidi.. #US - ISRAEL vs Iran
Kuna mengi yanazungumzwa kuhusu huyu kiongozi mkuu wa Iran 'Ayatollah Khamenei' Media House za Israel Zinareport uwezekano wa kufa huyu jamaa wakati wa Shambulizi la Israel dhidi ya Iran. Kipindi cha vita kunakuwa na propaganda nyingi ngoja tusubiri tuone.
MATOKEO YA HARAKA YA US - IRAN WAR
DUBAI imefunga anga lake kufuatia shambulizi la Iran jion ya leo ambapo baadhi ya raia wamejeruhiwa huko Dubai.
Hali hii imepelekea Shirika la ndege TANZANIA kusitisha safari zake Dubai.
Hii inatwa piga nikupige,
Usiku huu Irani karusha Makombora kuelekea Tel aviv - Israel kwa upande mwingine Marekani Kaishambulia Iran katika mji wake muhimu kihistoria Zanjan kaskazini magharibi mwa Iran.
#US VS IRAN
'Sardar Jabbari'
kamanda wa Jeshi la Iran anamwambia Donald Trump kuwa alichokiona ni Shehena ya Makombora ya Kizamani sana, hivyo asubiri muda si mrefu ataoneshwa mapya ambayo hajawahi kuyaona.
#US-ISRAEL strike on Iran
#Homozgan Iran
Shambulio la Marekan na Israel limelenga shule ya watoto wa Kike na kuuwa kati ya wanafunzi 40. Hii Vita inachukua sura mpya, Kiongozi mkuu wa Jeshi la Iran ametangaza kufanya mashambulizi ya awam ya pili usiku wa leo.
Sera ya huyu Jamaa "Make America Great Again"(MAGA)
ndo sababu kubwa ya strike dhidi ya Iran, tutegemee hali hatari zaidi maana Mpaka sasa Iran imejibu kwa kushambulia US Military base huko Saudi Arabia, Qatar, Bahrain, Israel na maeneo mengine.
Ni msimu wa Uboreshaji wa Daftari la mpiga kura. Ni haki na wajibu kupiga kura. Twende tukajiandikishe haijalishi uchaguzi utakuwaje ila muhimu uwe na sifa za Kupiga kura. Viongozi hawachaguliwi kwa maneno ya Vijiweni bali kwa kupiga kura. Nenda kapate kitambulisho cha Kura.
Bunge la Tz mbali na mapungufu mengi. Yapo mambo mawili wameamua kwa usahihi.
>Kupitia kamati ya kudumu ya Bunge ya bajeti, kuondoa ongezeko la ushuru ges ya magari sh 382/=
>kupitia Waziri wa Fedha, Kupunguza faini kwa wasiotoa risit kutoka 15m hadi 4m.πββοΈ
Nimesikiliza mrejesho wa Kikao cha PM na Wafanyabiashara: kilikuwa ni kikao muhimu sana, kikao kimekuja na maazimio 14; yapo maagizo ambayo serikali imetoa kwa TRA, TBS, Mawaziri wa Biashara na wataalam wa Forodha. Serikali imeonesha nia njema katika hili.π
#Luis Miquissone ni mchezaji mzuri.. ila hajapewa kipaumbele. Simba isiingie mkenge wa Kumuacha Kisa maneno ya waandishi wa habari wenye mlengo tofauti. Wamekuwa wakimtaja vibaya kuwa kashuka kiwango ili tumuache kisha wapinzani wanase sain yake. #apeweNafasi
#UK PM Rishi Sunak ametangaza kumsapoti Israel dhidi ya kundi la Hamas huko #GAZA. US ilishatoa kauli ya kupeleka msaada wa kijesh Israel. upande wa Palestine Syria anahisiwa kuisaidia #HAMAS, madai ambao yamekanushwa. Urusi inapinga hatua ya Marekan. #pray
Vita ya Mashariki ya kati ni vita nzito sana. Wanamgambo wa Hamas wameamsha upya joto lilopoa kwa muda kidogo. Sasa Israel wametangaza Operation kali kuwahi kutokea, Raia wasio na hatia wanakutwa na umaiti. #prayforIsrael#prayforPalestine