Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Kongamano la Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Urusi lililofanyika Jijini St. Petersburg nchini Urusi tarehe 05 Juni, 2026. Kongamano hilo limewakutanisha Wafanyabiashara, Wawekezaji pamoja na Taasisi za kukuza Uwekezaji kutoka Tanzania na Urusi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akitunukiwa Shahada ya Udaktari wa Heshima (Honoris Causa) na Chuo Kikuu cha Urafiki wa Watu wa Urusi- (RUDN University) kutoka kwa Mkuu wa Chuo hicho Profesa Oleg Yastrebov kwenye hafla iliyofanyika Chuoni hapo Moscow nchini Urusi, tarehe 04 Juni, 2026. Rais Mhe. Dkt. Samia ametunukiwa Shahada hiyo ya Udaktari wa Heshima kutokana na mchango wake katika Mageuzi ya sekta ya Elimu, juhudi zake za kuimarisha Diplomasia ya Tanzania, pamoja na mchango wake katika kuimarisha hadhi ya Tanzania Kimataifa ikiwemo kupitia sekta ya Utalii,
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa kuashiria uzinduzi wa Soko Kuu jipya la Kariakoo, Ilala Jijini Dar es Salaam tarehe 08 Februari, 2026.
_____
#KaziNaUtuTunasongaMbele#TabasamuLaUtu#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mazungumzo ya pamoja na Ujumbe wa Uganda uliongozwa na Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2026.
_____
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TabasamuLaUtu
#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2026.
_____
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TabasamuLaUtu
#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 07 Februari, 2026.
_____
#KaziNaUtuTunasongaMbele
#TabasamuLaUtu
#MaendeleoEndelevu
Fuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia akaunti zetu za Instagram: ikulu_mawasiliano, Facebook: Ikulu Tanzania Facebook fanpage: Ikulu Mawasiliano, Twitter: ikulu_Tanzania Youtube Channel: Ikulu Tanzania na Tovuti: https://t.co/wmldPXYfck
_________
#TanzaniaYetuSote
#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
“Nawatakia Watanzania wote heri ya kumbukizi ya Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Tuyakumbuke na kuyaenzi Mapinduzi haya si kwa kufanya kazi kwa bidii pekee, bali kwa kuoanisha kazi zetu na UTU. Hapo ndipo tutasonga mbele kwa mshikamano, tukijenga Tabasamu la Utu.”
—————
#KaziNaUtu
#TunasongaMbele
#TabasamuLaUtu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi, Ikulu Jijini Dar es Salaamtarehe 10 Januari, 2026. Pia katika mazungumzo hayo Mhe. Waziri Wang Yi aliwasilisha Salamu Maalum kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Xi Jinping.
———
#TanzaniaYetuSote
#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamojana Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Watu wa China, Mhe. Wang Yi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 10 Januari, 2026.
———
#TanzaniaYetuSote#NchiYetuKwanza#MaendeleoEndelevu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Jaz Elite Aurora, Bw. Hamed El Chiaty kuashiria uzinduzi wa Hoteli hiyo katika hafla iliyofanyika Michamvi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, tarehe 09 Januari, 2026.
_____
#TanzaniaYetuSote
#NchiYetuKwanza
#MaendeleoEndelevu