Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema Ujenzi wa Stand mpya ya Mabasi ya mikoani ya Mbezi Luis umefikia 90% na itaanza majaribio ya Kwanza November 25 na kuanza kutumika rasmi November 30.
Imeelezwa kuwa kuboreshwa kwa miundombinu imesaidia kwa kiasi kikubwa huduma ya damu salama kwenye Kanda ya Magharibi ambayo inahudumia mikoa ya Tabora,Katavi,Singida na Kigoma.
๏ฟผ
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Hamis Juma amewataka Majaji na Mahakimu nchini kuongeza matumizi ya njia ya usuluhishi katika kusikiliza na kumaliza mashauri hususan mashauri yanayohusu Mirathi
Watumishi 24 na wahandisi kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (MWTC), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Kampuni ya Mawasiliano Tanzania (TTCL Corp.) na Tume ya TEHAMA (ICTC) wametunukiwa vyeti vya kukamilisha mafunzo ya siku 9 ya teknolojia ya 5G.
Hospitali ya Taifa Muhimbili imethibitisha kwamba Jonathan Shana Warioba ambaye aliwahi kuwa Kamanda wa Polisi Arusha amefariki usiku wa kuamkia leo Sept. 16
TUME ya vyuo vikuu (TCU), nchini imewataka wale wote wanaotegeme kujiunga na elimu juu kufanya maamuzi na uchaguzi sahihi wakati wakiomba udahili kwenye vyuo vya elimu ya juu hapa nchini ili pindi wamalizapo masomo yao waweze kuhimili soko la ajira.
NAIBU waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa wananchi wa Tanzania hawana sababu ya kutokipigia Kura chama Cha mapinduzi CCM kutokana Kazi nzuri iliyofanywa na chama hicho kwa kipindi Cha miaka mitano.
MGOMBEA Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Dkt.John Magufuli amewahkikishia wananchi wa Wilaya ya Bahi kuwa wakimchgua katika Uchaguzi Mkuu mwaka unaotarajia kufanyika Oktoba 28 atahakikisha anaendelea kuleta maendeleo kwa kasi kubwa.
WITO umetolewa kwa wanasiasa wote nchini kufanya siasa za kistaraabu na kuepuka rushwa na matusi katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwenzi Octoba mwaka huu.
TANZIA
Aliyeigiza kama Mfalme wa nchi ya Wakanda katika filamu maarufu iitwayo "BLACK PANTHER" @chadwickboseman Amefariki Dunia baada ya kusumbuliwa na kansa ya utumbo tangu 2016
#ripchadwickboseman๐ค
Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Dk Wilson Charles amesema tume bado haijatoa taarifa yoyote ya kutangaza mgombea wa mbunge au Udiwani ambaye amepitishwa bila kupingwa.
Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC kimewataka wakazi waishio jirani na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Uwekezaji nchini kutunza maeneo hayo ili yaweze kuchochea uchumi wa Taifa kutokana na Uwekezaji unaotarajiwa au uliofanywa kuweza kuimarika
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), usiku huu imemteua Tundu Lissu kuwa mgombea Urais wa Tanzania kupitia CHADEMA na mgombea mwenza, Salum Mwalimu kwenye Uchaguzi Mkuu utakaofanyika October 28, 2020.