Baada kuridhishwa na maendeleo ya mradi huo Mhe. Waziri ameridhia ombi hilo na kuagiza wataalamu kutoka VETA kuanza kwa haraka mchakato wa mapitio ya mradi ili kuharakisha utekelezaji huo.
Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda mapema leo amefanya ziara ya kikazi Wilayani Mwanga ambapo ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule mpya ya Sekondari Kilaweni.
Katika ziara hiyo wananchi wa Mwanga wakiwakilishwa na mbunge wao Mhe. Joseph Anania Thadayo wamemwomba mhe waziri kwa mamlaka aliyonayo aifanye shule hiyo iwe moja ya shule ya amali.
Zoezi hilo la kuaga timu hiyo limefanyika mapema leo Juni 4, 2025, katika viwanja vya CD Msuya mara baada ya mchujo uliofanyika kwa makini kwenye shule mbalimbali wilayani hapa.
MICHEZO: DED MWANGA AWAAGA VIJANA 120 WANAOENDA KUSHIRIKI MASHINDANO YA UMISSETA NGAZI YA MKOA.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Bi. Zahara A. Msangi, ameiaga rasmi timu yake ya wanafunzi 120 watakaoiwakilisha wilaya ya Mwanga kwenye mashindano ya michezo
Timu ya Wataalamu wa Msaada wa kisheria ikiwa na Mheshimiwa Mwanahamisi Munkunda, Mkuu wa Wilaya ya Mwanga (katikati) mara baada ya kuhitimisha zoezi lililoanza tarehe 30 Januari hadi 7 Februari,2025
Kikundi cha Utamaduni cha Teule Cultural Group kutoka Wilayani Mwanga kilicho wakilisha Mkoa wa Kilimanjaro kwenye Tamasha la Kitaifa la Utamaduni Mkoani Ruvuma kimeibuka mshindi wa kwanza Kitaifa katika maandalizi ya vyakula vya asili kwa mwaka wa tatu mfululizo.