Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda, katika kikao na ujumbe wa mradi wa "Excellence Boost" unaofadhiliwa na EU kwa lengo la kuboresha Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi stadi nchini.
Kwenye Banda la NACTVET utapata taarifa na huduma mbalimbali ikiwemo;
1.Usaidizi wa Kufanya Udahili kwa Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa Masomo 2025/2026
2.Taratibu za Usajili wa Vyuo vya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi
3.Uhakiki wa Taarifa za Udahili
Wajumbe wa Baraza la Uongozi la NACTVET wamejengewa uwezo juu ya masuala mbalimbali ili kuimarisha uwezo wa Baraza hilo kusimamia Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET).
Semina hiyo imefunguliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi, Bi. Bernadetta Ndunguru. @ElimuTz
Halfa ya uzinduzi wa kampeni ya "Mwanachuo Smart" imefanyika katika ofisi za NACTVET Kanda ya Mashariki, ambapo Katibu Mtendaji wa NACTVET, Dkt. Mwajuma Lingwanda, ameizindua rasmi kampeni hiyo. Hafla hiyo imewashirikisha viongozi wa TAHLISO na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali.