@mangekimambi Hongera sana.
1. Swahili. Kwanini? Ujumbe kufika utafika tu lakini ili mijadala ilete impact lazima ianzie ndani. Ni kama video zako tu ujumbe kufika utafika tu ata kwa hao wasiojua kiswahili
2. Dada na Taifa inakupa room ata ya kumwachia successsor
Niffer na Dudubaya wanatumika bila kujua na wanawasaidia wauaji kuwatoa Watanzania kwenye reli.
Hizi kampeni za kipumbavu lazma Watanzania tuzikatae..
Kampeni zinahitajia Tanzania ni 3 tu.
1. Katiba mpya
2. Free Tundu Lissu
3. Uwajibikaji wa mauwaji ya October 29
Kampeni zingine zozote ni ushenzi na laana za kuhakikisha haki haipatikani.
Dunia inafahamu ukweli. Ndiyo maana Tundu Lissu anasema akipatikana na hatia, anyongwe hadi kufa. CCM wanasema adhabu siyo kunyongwa pekee
Tundu Lissu anaeleza Mahakama kwamba adhabu ya uhaini ni kuachiwa huru au kunyongwa hadi kufa. CCM wanasema Mahakama iamue kwa hisia tu
Anyways, tuachane na huo ujinga wa CCM
EPP Group (European People’s Party Group). Ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kati-kulia (centre-right) katika Bunge la Ulaya.
EPP Group (European People’s Party Group) ndilo kundi kubwa zaidi na lenye ushawishi mkubwa zaidi katika Bunge la Ulaya (European Parliament).
EPP GROUP (European People’s Party Group) wamempendekeza Tundu Lissu kugombea Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought)
Pia, ECR GROUP (European Conservatives and Reformists Group) wameungana na EPP GROUP kumpendekeza Tundu Lissu kuwa mgombea wao
ECR GROUP ni muungano wa kisiasa wa mwelekeo wa kulia/kihafidhina (right-wing/conservative) katika Bunge la Ulaya (European Parliament)
Kumpendekeza Tundu Lissu kunamaanisha wanamuona ni alama ya ujasiri na kielelezo cha watetezi wa demokrasia wanaopitia vizuizi
Kupendekezwa kwa Tundu Lissu ni tamko kwamba mapambano ya miaka mingi, yametambuliwa katika ngazi ya juu kabisa ya kitaasisi Barani Ulaya
Uteuzi huu TAL akiwa gerezani kwa mashtaka ya uhaini unaiweka diplomasia ya Tanzania na mazingira ya kisiasa ya ndani katika jicho la kimataifa;
Unaiwekea serikali na taasisi za kisheria ‘presha’ ya kuendelea kuheshimu misingi ya demokrasia, uwazi, na haki za kisiasa na michakato ya kiuchaguzi
Mchakato wa kumchagua mshindi wa Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) unafuata hatua zilizowekwa na Bunge la Ulaya
Kupendekezwa ni hatua ya kwanza katika mchakato mrefu wa utoaji wa tuzo hii. Siyo kwamba Tundu Lissu kupendekezwa ndiyo ameteuliwa mshindi
Ili mteule aingie katika kinyanganyiro, anapaswa kupendekezwa na: Kila kundi au kundi la wabunge linaweza kupendekeza jina moja pekee
Wagombea waliopendekezwa huwasilishwa katika mkutano wa pamoja wa kamati kadhaa za Bunge la Ulaya kwa ajili ya mchujo wa wagombea
Kamati ya Mambo ya Nje, Kamati ya Mandeleo, na Kamati Ndogo ya Haki za Binadamu. Hapa, maelezo ya kila mgombea husomwa mbele ya wabunge
Kamati mbili kuu za Bunge la Ulaya; Kamati ya Mambo ya Nje (AFET) na Kamati ya Mandeleo (DEVE), hufanya zoezi la kura ya pamoja kwa njia ya siri
Kutokana na kura hizo, wanachagua wagombea watatu wenye kura nyingi zaidi ili kuunda orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Uamuzi wa mwisho wa kumchagua na kumpata mshindi haufanywi na kamati, bali unafanywa na Mkutano wa Marais (Conference of Presidents)
Kundi hili hukutana faragha, kujadili finalists watatu, na kumtangaza mshindi mmoja rasmi kutoka katika orodha fupi ya mwisho (shortlist of three finalists)
Mshindi hualikwa katika ukumbi wa Bunge la
Ulaya mjini Strasbourg, France, wakati wa kikao cha pekee cha Bunge la Ulaya, mwezi Desemba
Huko, mshindi hutunukiwa cheti rasmi cha ushindi pamoja na zawadi ya kifedha ya £50,000. Hii kwa sasa ni sawa na takribani TZS 174,262,600
Tuzo ya Sakharov ni kitu gani?
Tuzo ya Sakharov (Sakharov Prize for Freedom of Thought) ndiyo tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya
Sakharov Prize for Freedom of Thought iIlianzishwa mwaka 1988 kwa heshima ya mwanasayansi na mpinzani wa Kisovieti Andrei Sakharov
Tuzo hizi wamewahi kushinda watu wazito sana Duniani wakiwepo; Nelson Mandela (1988), Kofi Annan (2003), na Malala Yousafzai (2013)
Sakharov Prize for Freedom of Thought hutolewa pia kwa watu au mashirika yanayojitolea kutetea uhuru wa mawazo na haki za binadamu Duniani
Wakati Serikali Katili ya CCM inataka kuaminisha Dunia Tundu Lissu ni mhaini, Dunia inakataa kwa vitendo uongo na ghiliba za serikali ya CCM
Dunia inampendekeza Tundu Lissu kuwa mshindi wa tuzo ya juu zaidi na heshima ya haki za binadamu inayotolewa na Bunge la Ulaya. Kwa heshimaaaa.
MMM, Martin Maranja Masese, Mtikila.
MUNGU NI MWEMA JANA HUKUMU IMETOKA NA TUMESHINDA.
Hii ni Baada ya SERIKALI HARAMU YA TANZANIA kutaka kibali cha MAHAKAMA nikakamatwe nchini "KENYA" na kurejeshwa Tanzania ili nipewe KESI YA UHAINI (NINYONGWE MPAKA KUFA).
Chawa waliambiwa WASAMBAZE Ujumbe huu wa kwamba "NAIROBI SIO MBALI" Ili niogope nikae kimya nisubiri KUKAMATWA NA KUNYONGWA ila moto unaendelea kuwaka bila Kuchoka.
Nawashukuru mawakili wangu kwa kupambana mahakamani kipindi chote hiki na huu ni ushindi wetu sote wapenda HAKI. @Advocate_Jebra@TitoMagoti
HUKUMU INA KURASA 12, NIMEWEKA HAPO MUHTASARI KWA LUGHA YA KINGREZA NA KISWAHILI. KAMA UTAHITAJI HUKUMU YOTE WASILIANA NA MAWAKILI WANGU.
WAKOLONI WEUSI MTANIONA SANA.
REPOST 500.
Huyu ni shemeji yake na makamu wa Rais haram, Deo Ndejebi… Yani huyu ni mdogo wa baba mmoja na mama mmoja wa Subira mke wa Deo. Yani huyu ni binti wa mwisho wa Adadi….
Mtoto mdogo huyu, hajui A wala B…
Nchi imetekwa na kundi dogo. It’s time to fight.
Yani wanahakikisha nchi nzima imeshikwa na familia zao au close friends tu, sisi wengine tunakamuliwa.
Alafu Watanzania wenyewe wako busy na upumbavu wa linda mgongo wako. Hivi huu ustupid tutaacha lini? Wanaweka wananchi busy na trend za kipuuzi huku wao kimya kimya wanainyonya nchi na familia zao. Imagine mambo kama haya yanaendelea Watanzania wanatolewa focus na upuuzi
This is why CCM wanang’ang’ania nchi ni ili mpaka wajukuu zao waje kututawala kama hivi….
Ila mijitu ya CCM sijui ni mi zero brain kiasi gani, mijitu imesota huko CCM miaka na miaka ila position za maana wapeana wenyewe CCM mtandao na familia zao, yenyewe imebaki kufanya uchawa kama mazuzu.
*MANENO YA MWISHO YA TUNDU LISU, leo:*
“Waheshimiwa Majaji miaka 60 iliyopita, kuna mhaini mwingine alifungwa kifungo cha maisha nchini Afrika Kusini, kabla hajahukumiwa alisema maneno yafuatayo ambayo naomba kuyafanya yawe maneno yangu leo, “During my lifetime I have dedicated myself to this struggle of the African people. I have fought against white domination, and I have fought against black domination. I have cherished the ideal of a democratic and free society in which all persons live together in harmony and with equal opportunities. It is an ideal which I hope to live for and to achieve. But if needs be, it is an ideal for which I am prepared to die”.
Nimepigania haki na demokrasia kwa sehemu kubwa, kuwa na nchi ya demokrasia, imekuwa ni ideal kwa nchi yangu, msimamo huo umenigharimu sana, umeniletea madhira mengi sana, msimamo huo kwa siku zilizobaki kwa maisha yangu ni msimamo ambao nitaendelea kuusimamia, na kama ikibidi kufa ni msimamo ambao nipo tayari kufa.
Namalziia kwa neno moja:
waheshimiwa majaji, kosa la uhaini halina kosa dogo, halina kosa ambalo ukishindwa kuthibitisha uhaini unahukumu kwa kosa dogo, it is either death sentence or acquittal, hakuna kakosa kadogo kwenye uhaini, waheshimiwa majaji, mzigo ambao mmekabidhiwa mabegani mwenu ni
kuamua kama kwa ushahdii huu kuna uhaini, kama mkiona kuna uhaini you should not hesitate to convict and punish me appropriately, do not hesitate, msiogope, kama mtaona kuna uhaini msiogope kunihukumu, kama mkiona hamna uhaini
msiogope kuniachia huru.
You have God before you, msije mkaletewa maneno kuna kosa dogo, hakuna kosa dogo kwenye uhaini, if the evidence doesn’t fit— acquit, huo ni mzigo ambao ni wa kwenu peke yenu waheshimiwa majaji. Nimemaliza”
Tundu Antiphas Lissu, September 28, 2026. Mahakama Kuu, Dar.