Sababu 3 Zinazoufanya Muungano wa Tanzania Kuwa wa Kipekee Afrika ๐น๐ฟ
1๏ธโฃ Umejengwa kwa hiari na umedumu kwa zaidi ya miaka 60 kwa amani
2๏ธโฃ Mfumo wa kipekee wa Serikali mbili ndani ya taifa moja
3๏ธโฃ Umejenga utambulisho imara wa โMtanzaniaโ
#miminamuungano#muunganotanzania#ssh
*Unanufaikaje na Muungano bila hata kujua?Unaposafiri bila vikwazo, unapofanya biashara popote nchini, unapotumia sarafu moja, unapojivunia amani na utulivu, hayo yote ni matunda ya Muungano. #sisinitanzania#nchiyangufahariyangu#nchiyangukwanza
Hotuba yangu leo Januari 15, 2026, katika Sherehe ya Mwaka Mpya wa Mabalozi (Diplomatic Sherry Party) kwa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania, Wawakilishi wa Heshima na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa, Ikulu, Chamwino, Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiagana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda, mara baada ya mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 06 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Viongozi wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 06 Januari, 2026.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu โ Kazi, Ajira na Mahusiano, Deus Sangu amewataka wamiliki wa viwanda nchini kuzingatia masuala ya usalama na afya mahali pa kazi ili kulinda ustawi wa wafanyakazi na kuongeza tija ya uzalishaji.
ย
Waziri Sangu ametoa wito huo (Januari 05, 2026) mkoani Mwanza, wakati wa ziara yake maalum ya kukagua utekelezaji wa masuala ya ย Usalama na Afya Mahali Pa Kazi katika Kiwanda cha Omega Fish Limited.
ย
Akiwa kiwandani hapo Waziri Sangu amepongeza menejimenti ya kiwanda hicho kwa kutoa ajira kwa wazawa na kuzingatia kwa vitendo sheria, kanuni na taratibu za usalama na afya mahali pa kazi.
ย
Sambamba na hayo, Sangu amevitaka viwanda vyote nchini kushirikiana kwa karibu na Wakala wa Usalama na Afya Mahala Pa Kazi (OSHA) ili kuhakikisha mazingira ya kazi yanakuwa salama, yenye tija na yanayochangia ukuaji wa uchumi wa taifa.
ย
Awali akizungumza Mkurugenzi Mkuu OSHA, Khadija Mwenda alisema OSHA itaendelea kusimamia wamiliki wa viwanda nchini kutekeleza sheria ya usalama mahala pa kazi katika ili kuwawezesha wafanyakazi na waajiri kutumia muda mwingi katika shughuli za uzalishaji wenye tija.
ย
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Omega Fish Market Hamad Alsalman ameishukuru Serikali na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa serikali katika kutekeleza majukumu ya kuhakikisha usalama mahala pa kazi ย unazingatiwa kisheria.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kawaida cha Baraza la Mawaziri kilichofanyika Ikulu Ndogo ya Tunguu, Zanzibar, tarehe 07 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na viongozi mbalimbali mara baada ya kuwasili katika Jengo la Taaluma na Utawala la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Jengo la Taaluma na Utawala na Bweni la Wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akivuta kitambaa pamoja na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kama ishara ya uzinduzi wa Jengo la Taaluma na Utawala na Bweni la Wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.
Taswira ya Jengo la Taaluma na Utawala na Bweni la Wanafunzi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Taasisi ya Sayansi za Bahari, Buyu Zanzibar mara baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Buyu Zanzibar tarehe 08 Januari, 2026.