Ujumbe wa Umoja wa Mataifa kwa Tanzania kuelekea D9
Kabla ya maandamano ya tarehe 9 Desemba, Ofisi ya #UmojawaMataifa ya Haki za Binadamu inawakumbusha viongozi kuhakikisha haki za kujieleza, kukusanyika kwa amani na kujiunga katika makundi.
Tunawakumbusha vikosi vya usalama kujiepusha na matumizi ya nguvu dhidi ya mikusanyiko isiyo ya vurugu na kuchukua hatua za kupunguza mvutano. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa, matumizi yoyote ya nguvu, ikiwemo silaha zisizo za moto, yanapaswa kuwa ya kiwango cha chini kabisa kinachohitajika.
Tunazitaka mamlaka kuhakikisha vikosi vya usalama vinapanga na kutekeleza operesheni kwa namna inayowezesha Watanzania kutumia haki hizi bila hofu.
#D9
#SamaiaMustGo
#SiriNiNamba
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Kumficha mtu kwa saa 48 bila kumfikisha Mahakamani au kumpa dhamana ni kuvunja sheria mnazotakiwa kuzifuata. Muacheni HURU ndugu @fbuyobe au mfikisheni Mahakamani kama kuna tuhuma zozote dhidi yake. Hii ni nchi yetu na wote tunayo HAKI ya kuishi kwa UHURU na AMANI. #FreeBuyobe
‼️Breaking news‼️
Inadaiwa na vyanzo viwili vinavyojitegemea kuwa Fadhili Saga (msaidizi wa Mombo) ameondolewa kwenye nafasi yake! Kumbukeni huyu nimempigia sana kelele kutokana na kuhusishwa na ushenzi mwingi sana na ukatili!
Hii haitoshi lakini maana alikuwa anafurahisha wakubwa zake so #SamiaMustGo #D9 #D9Tunatoka
UN inaungana na watanzania wote kuelekea maandamano ya AMANI DISEMBA 9 #D9
UN inazo taarifa za Polisi kuzuia maandmaano hayo-hivyo wanawakumbusha kazi yao kikatiba ya kulinda waandamanaji na sio vinginevyo.
Dunia ipo upande wa Watanzania kuelekea #D9 tutoke kwa wingi na mabango yetu yenye jumbe zetu za kutaka HAKI KWENYE TAIFA LETU.
Faida kubwa tuliyonayo kama wananchi kuelekea #D9 sisi ni wengi kuliko wao wakoloni weusi. Sauti ya wengi ni sauti ya MUNGU ushindi ni lazima.
#D9
#Disemba9Tunatoka
#SiriNiNamba
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Sisi kama kanisa ni wahanga, tulishapewa tahadhari tutapotezwa, hatupuuzi.
Ametekwa Padri Jordan Kibiki Mafinga.
Ametekwa Padri Padre Camillus.
Tarehe 26 Novemba 2025 juzi mwanafunzi wa usista ametekwa Mwanza.
Tusikilizwe ama tusisikilizwe tutaongea.
Fr. Charles Kitima
UBALOZI WA MAREKANI TANZANIA UMETOA TAHADHALI YA KIUSALAMA KWA RAIA WAKE. WAKIWEZA WAONDOKE AU WASIJE TANZANIA.
Ubalozi wa Marekani umeonya kuwa maandamano nchini Tanzania yanaweza kuanza kuanzia Desemba 5–9.
Na yanaweza kusababisha machafuko;
1.kufungwa kwa intaneti.
2. vizuizi barabarani.
3. usumbufu wa safari.
Polisi wanaweza kukagua simu kwa maudhui ya kisiasa.
Wanashauri watu wao kuepuka mikusanyiko, kufuata sheria, na kujiandaa na mahitaji ya dharura.
#D9 is REAL MOVEMENT.
#D9
#Disemba9Tunatoka
#SiriNiNamba
#TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Anaandika Mwanasheria mkuu wa CHADEMA DR. Rugemeleza Nshala.👇🏾
Samia na wenzake wote waliotwaa madaraka ya nchi kinyume cha demokrasia kushiriki katika mchakato wa kuliokoa na kulileta Taifa pamoja. Wote hawa wanatakiwa kujiuzulu mara Moja.
1. Samia atueleze Watanzania na Dunia Nzima ni nani aliyetoa amri ya kuuawa kwa Watanzania waliokuwa wakidai uchaguzi huru na haki?
2. Je ni Sheria ipi katika Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayompa Raisi madaraka ya kuzuia raia kuandamana na kusema "hakutakuwa na nywinywi Wala nywinywinywi"?
3. Je, kauli yake hiyo si ndiyo ilikuwa amri kwa Jeshi la Polisi la kuwafyatulia raia risasi za kuua kuzuia wasiandamane?
4. Je, anaifahamu na kuielewa ibara ya 14 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania inayosema kuwa Kila mtu anayo haki ya kuishi na kupata hifadhi ya maisha yake kutoka kwa jamii kwa mujibu wa sheria?
5. Kama anaifahamu je anakumbuka kuwa ni miongoni mwa ibara alizotuapia na kutueleza kuwa atazilinda na kuzitetea mnamo tarehe 19 Machi 2021? Na Kwa Nini hakufanya hivyo mnamo na baada ya tarehe 29 Oktoba 2025?
6. Kama Raisi, wakati uchaguzi unafanyika, nani alitoa amri ya kuzimwa intaneti kwa siku tano?
7. Ni nani aliyempa mamlaka IGP Wambura kuweka zuio "curfew" kwa wakazi wa Dar es Salaam na amri hiyo kutekelezwa katika sehemu mbali mbali nchini wakati hakuna Sheria inayomruhusu kufanya hivyo?
8. Kama si yeye, alichukua hatua gani za kinidhamu na kisheria dhidi ya IGP Wambura na wote hao waliojivika madaraka wasiyo kuwa nayo kisheria?
9. Ni nani aliyetoa amri ya miili ya waliouawa kuchukuliwa na kupotezwa bila kukabidhiwa kwa ndugu zao?
10. Ni nani aliyeamuru wapendwa wetu hao kutupwa na kurundikwa kwenye na nje ya mochuari kama mizoga?
11.. Ni nani aliyezuia Taifa kuwaomboleza waliouawa kinyama na Jeshi la Polisi na vikosi vingine vya Usalama?
12. Je Samia anafahamu msemo usemao za "buck stops at the president" ikimaanisha uwajibikaji katika serikali humwangukia raisi?
13. Sasa kama anafahamu msemo huo anasubiri nini yeye na genge lake kuondoka madarakani?
MWISHO
REPOST 200
TUTAKUWEPO🫵🏾😎
Jana nimejaribu kuwatembela kijana Mika Chavala na Niffer gerezani Segerea .
Kuwatia moyo na kuwambia hawako peke yao katika vita hii.
Pia kuwambia Watanzania wako pamoja nao na wanawaombea.
Lakini serikali dhalimu ya ccm wamekataa nisiwaone hawa vijana.
Nataka kutoa wito kwa Serikali hii dhalimu, kuwaachia watu wote waliobambikiziwa kesi za uongo za uhaini na ugaidi Nchi nzima.
Serikali inayobambikizia watu kesi haifai kuheshimiwa wala kubaki madarakani.
Watu huongozwa kwa ushawishi, sio kwa kuwatia hofu.
Hakuna kitisho kitakachoturudisha nyuma.
This was Mika Chavala (left) when he was finally arraigned in court and he is not among the hundreds freed! He is still detained along with Niffer
Mungu atasimama tu - vijana wanaonewa na kuteswa kwa sababu ya wazee wenye tamaa na roho nyeusi 🚮
Stay strong Gen Z 💪🏽🇹🇿 It shall be well
#FreeAllPoliticalPrisoners
#SamiaMustGo
#D9
"Nilipigwa sana bila kuulizwa chochote, niliyokutana nayo mahabusu ni ya ajabu sana watu wengi walifia ndani, walipigwa risasi za kiuno, nyonga. Nashukuru sana watanzania kwa kupiga kelele"-; Mtuhumiwa wa Uhaini aliyeachiwa huru
Meet brilliant young man Mika Chivala
He has been detained on treason charges by the illegitimare govt of @SuluhuSamia
He led a prayer for the protestors and later joined them 😓
This exceptional young leader is punished for speaming his mind like thousands of others!
Nchi ya kiwaki sana 🚮 huyu Mika ndo kiongozi anayetakiwa eti leo mmemfunga na kumpa kesi - chuki na husda tu maana kimama mtoto wake wa kiume tumeona posts zake anawaza mambo ya ajabu tu na bangi - leo anapewa pesa na kundi la mauaji ananyanyasa vijana bright kama Mika
Eniwei #SamiaMustGo and we will free all political prisoners on #D9
Serikali zenye watu wenye ubongo unaofanya kazi zinatakiwa kutumia akili ya (@MikaChavala) katika uzalishaji siyo kumpa mashtaka ya uongo ya uhaini ambayo haiwezekani kuyathibitisha. Wanaostahili kuwepo gerezani ni mafisadi wanaotajwa na CAG. Muacheni CHAVALA. #FreeMikeChavala
It will be well Mika 💪🏽🇹🇿
Wewe ni mshindi tayari
Mungu akufunike kwa mbawa zake
Nimepitia video zako - simama imara usiyumbishwe - you are destined for greatness! Usiogope hawa mafedhuli na usi-compromise! Mungu amekupangia mengi mema!
🙏🏽 Amen!
‼️ROUTE ZA MAANDAMANO - MAPENDEKEZO‼️
Jamani mapendekezo ni kuwa watu wakutane katika ofisi ya mkuu wa Wilaya katika wilaya zao
Kwa Dar es Salaam na Dodoma nadhani imeeleeweka
Hapa ni mapendekezo kwa mikoa ya Shinyanga, Mara na Simiyu
#D9 iko vizuri
#SamiaMustGo
Leo ni 29.11.25 zimetimia siku 32 tangu mauaji ya kutisha ya raia yafanyike kuanzia siku na baada ya uchaguzi. Hakuna hata kiumbe mmoja amewajibika/amewajibishwa kwa udhalimu huo. Wameendelea kukana maovu yao yote. Wamegoma kutaja idadi ya watu waliouwawa. Hawana dhamira njema. Hatuwezi kusahau ukatili wa kutisha na uhalifu dhidi ya binadamu. Hata kama watawala na wapambe wao watafanya press milioni kumi. Hatuwezi kusahau. Tunahitaji ukweli na uwajibikaji. Hatuhitaji ujanja-ujanja wa kufunika kombe, ili mwanaharamu apite. Waliohusika na kutoa amri ya kuua, walioua, walioficha na kupoteza ushahidi, hawa wote wachukuliwe hatua kali za kisheria.