๐ค๐ Kila show huwa na maoni tofauti kutoka kwa mashabiki. Mwisho wa siku, kilicho muhimu ni wasanii kuendelea kufanya kazi na kuwaacha watu waamue wenyewe. ๐ฅ
@chino_kidd7 ananyoosha maelezo juu ya kupokea baadhi ya comments kwamba amemfunika @officialalikiba kwenye show ya Simba Day uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
#PlanetBongo
๐๐ญ Kumbe uigizaji wake ulikuwa umefika level nyingine! Ila tukio moja haliwezi kuwa kipimo cha kila mtu. Cha muhimu ni kujifunza kutokurukia hitimisho kwa hisia pekee. ๐ ๐๐พ
๐๐ Kama taarifa hizi ni kweli, basi ni somo kwamba uaminifu na uwazi kwenye masuala ya mali ni muhimu sana. Inasikitisha kuona mtu akipitia hali kama hii. Mwenyezi Mungu ampe nguvu apite kipindi hiki. ๐๐พ
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa ufafanuzi kuhusu matukio ya ghasia yaliyotokea nchini mnamo Oktoba 29,2025 akidai kuwa yalikuwa na ajenda maalum ya siri na hayakufanyika kwa utashi wa hiari wa Watanzania wengi.
Katika mahojiano maalum na DW, Katambi amebainisha kuwa ushahidi upo wazi kuwa machafuko hayo yalipangwa na kuratibiwa kwa malengo ya kisiasa. Waziri Katambi amewataka Watanzania na jumuiya ya kimataifa kujiuliza maswali ya msingi kuhusu uhalali wa kile kilichoitwa maandamano siku hiyo. Amehoji ni nchi gani duniani inayoruhusu maandamano siku ya uchaguzi mkuu, na ni sheria gani inayoruhusu maandamano yasiyokuwa na taarifa, viongozi wanaojulikana, wala ruti maalumu.
โNchi gani duniani imewahi kuruhusu maandamano kama yangekuwa ya halali, halafu waandamanaji wakaenda kwenye duka la simu la mtu wakachoma moto... wakaenda kwenye sheli wakachoma sheli moto... wakaenda kuchoma vituo vya polisi?โ amehoji Katambi akionesha kusikitishwa na uharibifu wa miundombinu muhimu ya taifa
Katambi ametoa hoja ya kitakwimu akijiuliza kwanini ghasia hizo zilitokea katika mikoa minne au mitano tu, wakati taifa lina watu zaidi milioni 61. Amebainisha kuwa ikiwa hasira ingekuwa ya wananchi wote, ghasia hizo zingejitokeza pia vijijini ambako asilimia 70 ya Watanzania wanaishi, lakini hali huko ilikuwa ya utulivu
Aidha, amewashutumu aliowaita viongozi wa maandamano hayo kwa kushindwa kujitokeza tarehe 30 au 31 Oktoba kuomba radhi kwa mali zilizopotea, badala yake wakaendelea na uchochezi.
โWakati haya yanatokea na kama kweliโฆsi ilikuwa siku tarehe 29 Oktoba, tarehe 30 kwanini hawakujitokeza viongozi wa kusema kwamba sasa sisi tulikuwa tuna maandamano halali lakini imetokea bahati mbaya labda kuna wahuni waliingilia, tunaomba radhi kwa mali zilizopotea kwa wale waliofanyiwa uhalifu, kwanini, tarehe 30. Kwanini hawakujitokeza hao viongozi? Tarehe 31 sijui tarehe moja, kwanini badala ya kusikia watu wakitoa kauli za pole kwa mamlaka mbalimbali na walioathirika badala yake tulisikia uchochezi wa aina nyingine, na baadhi ya watu kujilaumu kwamba tumefeli tungefanya hiviโฆtarehe moja, kwanini hatukuona hata baadhi ya viongozi wa dini...
NB: Soma zaidi https://t.co/4yxMQu4P8L
https://t.co/iAgEeNnqrn
VIDEO:
Kada wa Chama cha ACT Wazalendo, Luhaga Mpina, leo Jumapili Agosti 09, 2026, amepinga kauli ya serikali kuwa imeshafikia makubaliano na vyama vyote vya siasa isipokuwa kimoja.
Mpina amerejea kauli ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyoitoa tarehe 30 Julai 2026, alipokutana na viongozi wa vyama vya siasa Ikulu, ambapo alidai kuwa vyama vyote viko vizuri isipokuwa chama kimoja ambacho kimeelezwa na wadau siasa kuwa CHADEMA.
Mpina amebainisha kuwa msimamo wa ACT Wazalendo kuhusu maridhiano bado upo vile vile kama ulivyotangazwa kwenye matamko ya kamati kuu ya chama hicho. Mpina amesema kuwa hakuna maridhiano yoyote yanayoweza kufanyika bila kuzingatia misingi mitatu mikuu: Ukweli, Haki, na Uwajibikaji kufuatia matukio ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Amesema kuwa CHADEMA pia ilishatoa taarifa tarehe 3 Agosti 2026 kuwa haijawahi kukutana kwa siri na CCM au serikali kwa mazungumzo yoyote.
โSasa haya maneno ambayo anayazungumza mtawala kwamba ameshaelewana na vyama vya siasa isipokuwa chama kimoja ina maana gani? Ina maana gani?โ amehoji Mpina.
๐ค Binafsi bado nina mashaka. Maneno yanaweza kubadilika, lakini matendo ndiyo yanayoonyesha ukweli. Tutaendelea kutazama na kuhukumu kwa yale tunayoyaona, si yale tunayoambiwa. ๐น๐ฟ๐
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema, HecheJohn, akizungumza katika Mkutano Mkuu Maalum Mkoa wa Mara leo.
Katika muendelezo wa kuchangisha fedha, Tonetone, CHADEMA Family wamechangia Sh. 400,000 na mkutanoni imepatikana Sh. 100,000, jumla Sh. 500,000 kwa ajili ya kuwezesha Baraza Kuu la Umma. Mhe. Heche pia amekabidhiwa zawadi ya samaki.
Siasa zina changamoto zake, lakini ukweli na uwajibikaji ndio muhimu zaidi. Tusubiri taratibu za kisheria zifanye kazi na kila upande utoe hoja zake. ๐น๐ฟ
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi Rhoda Kunchela amesema Chama hicho kitachukua hatua za kuwapeleka mahakamani wanachama wa CHAUMMA waliotoa tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa chama hicho John Heche kuhusu matumizi mabaya ya fedha.
Rhoda amesema wanachama hao ni Elizabeth Sigera, alijitambulisha kama katibu wa baraza la vijana CHADEMA Mkoa wa Katavi na Antony Mwamba, kalala alijitambulisha kama Mwenyekiti wa baraza la wazee Jimbo la Katavi.
Ktibu Mwenezi wa Vijana wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) Taifa, Elizabeth Kasera, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Maalum ya Taifa kupitia Jukwaa la Vijana la chama hicho, ametoa ufafanuzi kuhusu sakata hilo kuwa tuhuma hizo sio misimamo wa CHAUMMA na hatua zozote zitakazochukuliwa dhidi yao Chama hakitahusika.
Kwa mujibu wa Kasera, Sigera alinukuliwa akitoa tuhuma dhidi ya Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, huku akijitambulisha kama mwanachama wa CHADEMA, jambo ambalo Kasera amesema si la kweli kwa kuwa Sigera alikuwa mwanachama wa CHAUMMA.
Kasera amesema kitendo hicho ni kinyume na maadili ya chama na hakikubaliki na kutokana na hatua hiyo, CHAUMMA imeamua kumvua Elizabeth Sigera uanachama pamoja na nyadhifa zote alizokuwa akizishikilia ndani ya chama.
"Kitendo alichokifanya Elizabeth Sigera ni kiovu na kisichovumilika. Chama kimeamua kumfuta uanachama na kumvua rasmi vyeo vyote alivyokuwa navyo ndani ya CHAUMMA," amesema Kasera.
Kasera amesisitiza kuwa CHAUMMA, kama chama cha upinzani, kinatambua CHADEMA kuwa ni miongoni mwa vyama vikuu vya upinzani nchini. Hivyo, amesema si sahihi kwa wanachama wa CHAUMMA kushambulia vyama vingine vya upinzani badala ya kushirikiana katika malengo yao ya kisiasa.
"Sisi vyama vya upinzani adui yetu mkubwa ni CCM. Hivyo si vyema sisi kwa sisi kushambuliana," amesema.
Aidha, Kasera amesema chama kinaamini kila mtu anapaswa kuwajibika kwa matendo yake binafsi, na kwamba makosa yanayodaiwa kufanywa na Sigera hayapaswi kubebwa na taasisi ya CHAUMMA.
Masoko ya uhakika ndiyo nguvu ya mkulima. ๐พ๐น๐ฟ Tunatumaini jitihada hizi zitawasaidia wazalishaji kuuza mazao yao kwa thamani nzuri na kunufaika zaidi. ๐
#HABARI Rais Samia Suluhu Hassan amesema Serikali itaendelea kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi kwa ajili ya mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi, akisisitiza kuwa Tanzania imefungua milango zaidi kwa biashara na uwekezaji.
Rais Samia amesema hayo leo, Agosti 8, 2026, wakati akizungumza katika maadhimisho ya Siku ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa yaliyofanyika katika Viwanja vya John Malecela, Nzuguni, Dodoma.
Amesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha wazalishaji kupata masoko ya uhakika huku ikiendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi.
โTumeifungua nchi kibiashara na uwekezaji na tunaendelea kuvutia wawekezaji wa ndani na nje, sambamba na mwelekeo wa Dira yetu ya Taifa unaoipa sekta binafsi asilimia 70 ya utekelezaji wake,โ amesema Rais Samia.
#EastAfricaRadio #TogetherTunawakilisha
๐ Mjadala umevuka mipaka ya Tanzania. Unadhani ushiriki wa majaji wa kimataifa kwenye tume kama hii unaongeza uaminifu au unaibua maswali zaidi? ๐ค๐
John Bocco ni sehemu ya historia ya Simba. Itakuwa burudani ya kipekee kuwaona mastaa waliowahi kuipa heshima klabu wakirejea uwanjani tena. ๐ดโฝ #SimbaDay2026
๐๐๐๐๐๐๐ ๐ ๐๐๐๐๐๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐๐ ๐๐๐ ๐๐๐๐.
Legend John Bocco atakuwa mmoja wa wageni maalumu katika Simba Day 2026, lakini pia atashiriki mchezo wa kirafiki kama mmoja wa wachezaji wa timu ya menejimenti ya Simba. Vuta picha hapa Okwi, pale Kagere na Bocco. Kesho hiyooo. #SimbaWeek2026 #SimbaDay2026 #NguvuMoja
VIDEO:
Naibu Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Bukombe, Dkt. Doto Biteko, amewataka Watanzania kuendelea kuuenzi na kuudumisha utamaduni wa amani, upendo na mshikamano, akisisitiza kuwa misingi hiyo ndiyo nguzo kuu ya maendeleo endelevu ya Taifa.
Akizungumza wakati wa ibada na mazishi ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Ilolangulu, Kabula Ndabacha, yaliyofanyika wilayani Mbogwe, Dkt. Biteko alisema nyakati za mafanikio na changamoto zinahitaji wananchi kuendelea kuthaminiana, kusaidiana na kuishi kwa upendo bila kujali tofauti zao.
โAmani ni urithi wetu mkubwa na ndiyo msingi wa maendeleo tunayoyashuhudia leo. Tuilinde kwa kuendelea kuishi kwa upendo, umoja na kuheshimiana, kwani maendeleo ya Taifa letu yanategemea mshikamano wa wananchi wake,โ alisema Dkt. Biteko.
Aidha, alitoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, marafiki na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akieleza kuwa kifo cha Mhe. Kabula Ndabacha ni pigo kwa familia, wananchi wa Kata ya Ilolangulu na Chama Cha Mapinduzi kutokana na mchango wake katika kuwatumikia wananchi.
Dkt. Biteko aliwahimiza wananchi kuendeleza mema yaliyoachwa na marehemu kwa kushiriki katika shughuli za maendeleo, kuimarisha mshikamano wa jamii na kuendelea kuilinda amani ambayo imeendelea kuwa tunu na fahari ya Tanzania.
Mwisho
Ufugaji wa samaki kwa mfumo wa aquaculture umeibuka kama fursa muhimu ya ajira na kipato kwa Vijana na Wananchi wengi, ukitumia teknolojia za kisasa zinazorahisisha uzalishaji na kuongeza tija, mfumo huo sasa unazidi kuvutia Watu wengi katika Maonesho ya Kimataifa ya Kilimo ya Nanenane yanayoendelea Jijini Dodoma, ambapo sekta ya uvuvi kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaonesha namna teknolojia hii inavyoweza kubadili maisha.
Akizungumza katika maonesho hayo, mtaalam wa mradi wa aquaculture Kusekwa Masondole amesema mfumo huo si tu unarahisisha ufugaji wa samaki bali pia unatoa ajira za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja kwa Vijana wanaojihusisha na usimamizi wa mabwawa, uuzaji wa chakula cha samaki na huduma za ufungaji wa mifumo ya kisasa.
Masondole ameongeza kuwa aquaculture imefungua milango ya biashara mpya, ambapo Watu sasa wanaweza kujiajiri kupitia ujenzi wa mabwawa, usambazaji wa vifaa na hata kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Wafugaji wapya, jambo linalochochea ukuaji wa sekta hiyo na kupunguza utegemezi wa ajira za ofisini.
Aidha amehimiza Wananchi kutumia fursa ya Maonesho ya Nanenane kujifunza kwa vitendo teknolojia hizi za kisasa za ufugaji wa samaki ili waweze kujiajiri na kuanzisha miradi yao midogo na ya kati inayoweza kuleta kipato endelevu katika maisha yao ya kila siku. #MillardAyoUPDATES
Hakika Yanga imepoteza mmoja wa mashabiki wake waaminifu. Jina la Mzee Motisha litaendelea kukumbukwa kwa mapenzi yake makubwa kwa klabu. Mwenyezi Mungu amrehemu. ๐๐๏ธ
Familia ya Yanga imepata pigo kubwa kufuatia kifo cha Mwanachama wake maarufu, Mzee Said โMotishaโ, aliyefariki dunia jioni ya leo.
Mzee Said Motisha alikuwa mmoja wa Mashabiki na wanachama wa muda mrefu wa Yanga SC, akijulikana kwa mapenzi yake ya dhati kwa klabu hiyo. Alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakihudhuria mechi nyingi za Yanga nyumbani na ugenini, akitoa hamasa kwa wachezaji na mashabiki wenzake bila kuchoka.
Kwa miaka mingi, jina la โMotishaโ lilikuwa sehemu ya utambulisho wa Yanga, huku uwepo wake ukiwa chanzo cha ari na mshikamano kwa Wananchi. Wengi walimfahamu kama shabiki wa kweli, aliyeishi na kuipenda Yanga katika nyakati za ushindi na changamoto.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na familia, maziko ya marehemu yatafanyika kesho, Ijumaa, baada ya Swala ya Alasiri.
Ibada ya mazishi itafanyika katika Msikiti wa Mwinyimkuu, kabla ya mwili wake kuzikwa katika Makaburi ya Mwinyimkuu.
Hakika mchango wake kwa familia ya Yanga utakumbukwa kwa muda mrefu. Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake, amrehemu kwa rehema zake pana, amjaalie Pepo ya Firdaus, na awape familia, ndugu, jamaa na Wanayanga wote subira na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu.
Inna Lillahi wa Inna Ilayhi Rajiโun.
#KitengeSports