@stillfaucie@kenyasgossips They are never difficult that's what we learned from primary level. That's what we're exposed to at first sight. We never thought out of that till we reached secondary level.
If you're told to learn mathematics in Chinese you will feel the same & it's contrary to chinese people
@tanpol Askari kwa ujumla hamna akili hata robo. Mnapokosea kuweni tayari kuomba msamaha. Sisi raia ndio maboss zenu
Lakini kwakuwa mmekosa utu kila kitu mwachukua sheria mkononi.
Sasa naskia mnatafuta aliyerekodi mumpoteze kama mlivyozoea huyo ni ndugu yangu lolote litalomkuta mtalpa
Watanzania tusimwangushe huyu babaโฆโฆโฆ..
Angalau akitoka ndani akute tumepiga hatua kubwa kwenye maendeleo.
KUCHANGIA TUMA PESA:
M-Pesa
Namba: 0744446969
Jina: CHADEMA HQ
NMB Bank
Namba ya Akaunti: 22606600140
Jina la Akaunti: Chama cha Demokrasia na Maendeleo
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 8
Anaendelea Mhe. Lissu.
Wakili Kisabo: Ni sahihi nilikuletea lakini admission officer aliichukua akaisoma na kuwapa wengine na baada ya hapo wakasema hatuwezi kuruhusu umpatie Tundu Lissu hii nyaraka.
Jaji: Unasema mwenyekiti wa kikao unamaanisha nini?
Wakili Kisabo: Ni mtu aliyekuwa anasimamia yale mazungumzo yetu.
Mhe. Lissu: Sasa katika ofisi hiyo ya naibu Mkuu wa gereza kuna uwezekano wa kuzungumza bila kusikilizwa upo kweli?
Wakili Kisabo: Huo uwezekano haupo kabisa.
Mhe. Lissu: Kesi yangu ya uhaini imeendeshwa kwenye chumba hiki hiki cha mahakama?
Wakili Kisabo: Ni kweli
Mhe. Lissu: Na kila ninapoletwa na kwamba hata mara moja mmewahi kuruhusiwa kuja kuniona huko lockup?
Wakili Kisabo: huwa tunazuiwa kabisa.
Mhe. Lissu: Je hapa mahakamani mmewahi kuruhusiwa kunipa nyaraka yoyote?
Wakili Kisabo: Huwa wanazichukua hawa maaskari magereza hata kama ni mbele ya Jaji.
Mhe. Lissu: Ilikuwaje ulipotaka kunipa uamuzi wa Jaji Mkwizu kuhusu malalamiko yangu ya kutopewa haki zangu?
Wakili Kisabo: Walipokonya hawakukupatia.
Mhe. Lissu: Vipi unasemaje kuhusu utendaji kazi wa Mkuu Wa Gereza?
Wakili Kisabo: Hafuati sheria kabisa. Anajiamulia tu.
Mhe. Lissu: Jaji Mkwizu alitoa amri kuwa utaratibu wa sheria ufuatwe lakini amri hiyo imepuuzwa?
Wakili Kisabo: Ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Na nyie mawakili mlilalamika sana toka Kisutu pia?
Wakili Kisabo: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Ni kweli kikosi kazi cha umoja wa mataifa kimesema mawasiliano kati yangu na mawakili wangu iheshimiwe?
Wakili Kisabo: imesema hivyo lakini halijawahi kuzingatiwa na hawa mapolisi.
Mhe. Lissu: Je mmekosea kuja kulalamikia mambo haya.
Wakili Kisabo: Mahakama hii ya Kikatiba ndio eneo sahihi kabisa.
Wakili Lissu: Ni kweli Mahakama hii ina ushahidi mwingi kuhusu jambo hili ukiachana na ushahidi wangu na ushahidi wenu?
Wakili Kisabo: Ni sahihi kabisa. Maana mambo mengine yametokea mbele ya mahakama hii Kuu na pia nyaraka za mwenendo wa mashauri yaliyopo hapa.
Mhe. Lissu: Ni kweli wajibu maombi haya akiwemo mkuu wa gereza katika majibu yake na kiapo chake ametusaidia kutuwekea nyaraka nyingi sana zinazotusaidia kwenye kesi yetu.
Wakili Kisabo: Kwakweli ametusaidia sana kutuletea mavitabu ya kuonesha walivyokuwa wanatuandika majina na kusema sababu za tusimamiwe na kusikilizwa.
Mhe. Lissu: Nimemaliza.
Anasimama Wakili wa Serikali Kalokola anasema tunaomba break ya lisaa.
Kesi imeahirishwa baada ya lisaa limoja.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Leo July 21, 2026
Jana tuliishia part 6 so leo tunaendelea na-;
Part 7
Leo Mhe. Lissu aanaendelea kuhoji Mawakili wake ambapo anamuhoji Wakili Paul Kisabo.
Mhe. Lissu : Nitakuuliza maswali kuanzia Tar. 16/06 hadi November 15.
Tar. 16/06 pale Kisutu Nililalamika kuhusu mawasiliano yangu na mawakili wangu?
Wakili Kisabo: Ni kweli na ukasema umetuondoa kazini.
Mhe. Lissu: Baada ya hapo utaratibu wa mawasiliano ulibadilika?
Wakili Kisabo: Ni kweli
Mhe. Lissu: Utaratibu ulibadilika na tukawa tunazungumza kwenye admission office.
Wakili Kisabo: Ndio na walikuwa wanatusikiliza
Mhe. Lissu: Kwenye kiti cha wakili anachokaa pale admission kuna askari anapiga type anaandika. Na wengine wengi wanaandika humo ndani na Insp. Mwingine wa sheria na mwingine wa usalama.
Wakili Kisabo: ni kweli kabisa.
Mhe. Lissu: Na kule kwenye kile chumba cha awali tunachoongea na simu ni kweli wanakusimamia na kukusikia unachoongea kwenye hiyo simu?
Wakili Kisabo: Ni kweli.
Mhe.Lissu: Kuna CCTV camera hapo kwenye kale ka Chumba?
Wakili Kisabo: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Na turudi kwenye admission office napo CCTV zipo?
Wakili Kisabo: Ni kweli zipo.
Mhe. Lissu: Je unapozungumza na mteja wako kuna usiri wowote?
Wakili Kisabo: hakuna usiri maana wanakusikiliza na kutusimamia kwa kila kitu.
Mhe. Lissu: Soma kanuni ya 33(1)(a) ya Kanuni za Magereza. Je kwa kanuni hiyo utaratibu unaotumika kunisimamia mimi kama huo utaratibu ni wafungwa wa kifo au wafungwa wengine kawaida?
Wakili Kisabo: Huo ni utaratibu wa wafungwa waliohukumiwa kifo sio mtu kama wewe.
Mhe. Lissu: Soma sheria ya magereza na kanuni zake. Je mahabusu kama mimi anaruhusiwa kusimamiwa hivyo kama ninavyosimamiwa mimi?
Wakili Kisabo: Hakuna mahali kokote inaruhusiwa kwenye sheria.
Mhe. Lissu: Baada ya 15/11/2025 utaratibu ukabadilika kutoka admission office kwenye kwa naibu mkuu wa gereza ofisi ambayo yupo pia mtu wa usalama wa gereza?
Wakili Kisabo: Haswaaa ilikuwa hivyo.
Mhe. Lissu: Ofisi ya mkuu wa jela tumekutana mara ngapi ukazungumza na mimi?
Wakili Kisabo: Zaidi ya mara tatu.
Mhe. Lissu: Tulipofanya kwa mkuu wa gereza tulikuwa peke yetu?
Wakili Kisabo: Alikuwepo Mkuu wa Gereza, Walinzi wako na maaskari wengine wanajaaa mle.
Mhe: Lissu: Ni kweli hujawahi kupima ukubwa wa ofisi ya Mkuu wa Gereza?
Wakili Kisabo: sijawahi kupima.
Mhe. Lissu: Je sasa kuna uwezekano wa kusikia au kutosikia tunachoongea?
Wakili Kisabo: Lazima watusikie. Wametusikia mara zote.
Mhe. Lissu: Kwanini unasema wanatusikia.
Wakili Kisabo: Kwanza wako karibu na sisi chumba ni kidogo. Kuna muda tukicheka wanacheka na kuna muda tukisikitika na wao wanasikitika. Maana yake wanatufuatilia.
Kicheko kwa mbali kinatokea. ๐๐๐
Mhe. Lissu: Sasa kule kwa naibu mkuu wa gereza kukoje?
Wakili Kisabo: Na kwenyewe walikuwa wanajazana na kusikiliza kila kitu. Kulikuwa hakuna faragha kabisa.
Mhe.Lissu: Tuzungumze mabadilishano ya nyaraka, Ni kweli mmeniletea nyaraka mbalimbali kuhusu kesi inayonikabili Mahakama kuu.
Wakili Kisabo: Ni kweli lakini kabla hatujakupa wanazichukua na kuzisoma.
Mhe. Lissu: Na hadi unapoondoka huwa bado wako nazo wao?
Wakili Kisabo: Ni sahihi
Mhe. Lissu: Ni kweli mara nyingi nimewalalamikia kuwa sipati hizo nyaraka mara nyingine?
Wakili Kisabo: Mara nyingi sana umelalamika hata ile hotuba ya Jaji Chande kuhusu ripoti ya uchunguzi wa matukio ya oktoba 29 hujapata hadi leo.
Mhe. Lissu: Unafahamu kama mawakili wa serikali walisema Mahakamani wanataka kuongeza ushahidi kuniunganisha na matukio ya oktoba 29
Wakili Kisabo: Ni kweli na nyaraka ile nilikuletea ujiandae na utetezi.
Mhe. Lissu: Ni kweli mwezi uliopita uliniletea nyaraka kutoka umoja wa mataifa ikisema niachiwe kwa kesi hii.
Part 8 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba Repost yako.
#UPDATES_KESI_YA_MAWAKILI_WA_MHE_LISSU_DHIDI_YA_MKUU_WA_MAGEREZA
Part 4
Anaendelea Mhe. Lissu
Mhe. Lissu: Twende Annexure SUPP 6 angalia Tarehe 12/12/2025 mtu wa pili ameandikwa Paul Emanuel Kilasa Kisabo na yeye alikuja kuniona na akaruhusiwa?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Kwa Mawakili wangu aliyekatazwa kuja kuniona ni wewe peke yako?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Sasa tuje kwenye sababu za kukukatalia wewe kuja kuniona. Soma Annexure SUPP 3 entry ya Tar. 28/10/2025 je siku hiyo ulikwenda Gereza la Ukonga na Wakili mwenzako Gaston Garubindi?
Wakili Maduhu: Ni kweli
Mhe. Lissu: Nenda kwenye SUPP 1 ile orodha na wambie majaji kama Gaston Garubindi yupo kwenye hiyo orodha?
Wakili Maduhu: Jina lake ni namba 3.
Mhe. Lissu: sasa angalia hiyo nyaraka sawasawa imeandika mambo mengi kule mwisho kuna maoni ya OC ni officer in charge yaani BWANA JELA.
Ameandika maoni yake kuwa aruhusiwe kumuona ambae yupo kwenye orodha ya mawakili. Na huyo mwingine asiruhusiwe kwasababu hayupo kwenye hiyo orodha.
Wakili Maduhu: Niliambiwa toka hapa haupo kwenye orodha.
Mhe. Lissu: Je kuna Wakili mwingine ameandikiwa maoni ya namna hiyo kwenye orodha ya mawakili wangu kuwa asinione hayupo kwenye majina niliyompa Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Hakuna wakili mwingine.
Mhe. Lissu: Je kuna utaratibu wa kisheria kuhusu mambo haya?
Wakili Maduhu: nimekutana nao ukonga. Haujawahi kuwepo.
Mhe. Lissu: Kwani wewe una makosa gani ya Bwana Jela wa Ukonga?
Wakili Maduhu: Sifahamiani nae sijui nilichomkosea.
Mhe. Lissu: Wakati umeruhusiwa kuja kuniona Juma Mwaibako ndio alikuwa anakaimu ukuu wa gereza?
Wakili Maduhu: Ndio
Mhe. Lissu: Huyu aliyekuzuia ni Andrew Shabani ndio aliyekuzuia?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Wewe una tatizo la ngozi? Albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi.
Mhe. Lissu: Kwenye hili Taifa kuna ubaguzi wa watu wenye albinism?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Sasa Wakili aliyezuiwa ni wewe mwenye albinism?
Wakili Maduhu: Ni mimi peke yangu ndio nimekataliwa by implication.
Mhe. Lissu: ulipenda uwe albino?
Wakili Maduhu: Sikupenda. Ila ndio nimebaguliwa hivyo.
Mhe. Lissu: Nilisema naomba samahani.
Shahidi ametoa machozi na kuumia sana juu ya vitendo hivi. Watu wameumia sana hapa Mahakamani wanaofuatilia kesi hii. Matendo haya ni ya kinyama sana.๐ฅน
Mhe. Lissu: Niliandika orodha ya pili na kuwaongeza wewe na Kisabo kwenye hiyo orodha ya pili. Niliwaongeza wewe na Kisabo na hatimaye Kisabo akaanza kuruhusiwa na wewe ukaendelea kuzuiwa kuingia.
Wakili Maduhu: Ni kweli.
Mhe. Lissu: Nikaandika orodha nyingine na kuwaongeza Wakili Deogratias Mahinyila, Dickson Matata na mawakili wengine kwenye hiyo orodha ya pili.
Wakili Maduhu: Ni sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Anayetunza hizo nyaraka ni Mjibu maombi wa tatu ambae ni Bwana Jela?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama mawakili ambao hawapo kwenye hiyo orodha na wameruhusiwa kuja kuniona.
Neema Saruni
Denis Luwis
Nyaronyo Kichere
Unafahamu kama wameruhusiwa kuja kuniona na hawapo kwenye orodha ya mawakili waliokuja kunitembelea.
Wakili Maduhu: Nafahamu ndio.
Mhe. Lissu: Waeleze Majaji kama ni kweli au si kweli kwamba mara ya kwanza mlipokuja kuniona hatukuonana ana kwa ana bali mlipelekwa kwenye chumba chenye ukuta wa kioo?
Wakili Maduhu: Ni sahihi.
Mhe. Lissu: Kwahiyo msingeweza kunipa mkono mkasema Mwenyekiti Pole?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Mhe. Lissu: Na namna pekee ya mawasiliano kwa siku hiyo ilikuwa ni simu upande wenu na upande wangu?
Wakili Maduhu: Sahihi kabisa.
Part 5 itaendelea kwenye post inayofuata.
Naomba repost yako.
@lyim99872@Mvuvi_Nyasa Ujue nimeangalia mara nyingi sana kutaka kugundua shida ya dogo ni nini kumbe anamaanisha rasta.
Sasa rasta zinashida gani wakuu?
Hiyo ndo utambulisho wetu sisi black men
@HecheJohn Heche anapiga kazi ya kitume sana Mungu akubariki kaka.
Back to Back mikutano sio poa. Energy uliyonayo sio ya kawaida.
Nimefuatilia mikutano yako nimegundua unatoa speech kulingana na hali ya eneo husika.
Hii consistency ni top notch. Mungu akuweke sana wewe ni TUNU ya TAIFA
@Wakutumwa_@INFLUENCERjr Acha waoane wao kwa wao mbali na hapo utaimba Yesu nibebe.
Kwenye haya maisha kwa mara ya kwanza nimeshuhudia mzazi wa kike akiwa na chuki dhidi ya mwanae wa kumzaa namimi ndo baba.
Mwanangu yupo shule ya boarding Mwanga, yeye anaishi Mwanga na hajawahi enda hata kumwona.
@mangekimambi Kwa haraka unaweza sema uko sahihi ila kwa jicho la pili CDM wako sahihi why?
CDM ni taasisi na wamefunguliwa kufanya siasa hivi karibuni tu. Kamati kuu ikakaa kikao ikaandaa dira (hapo ni kabla ya 7/7)
Kwasasa wanafata dira waliyoiandaa na maandamano yamo ila sio 7/7