Kiwango kimoja cha kumtegemea Mungu ni kumuomba Yeye pekee mahitaji yako yote. Lakini kiwango cha juu zaidi ni kuamini kuwa baada ya kumuomba, Atajibu kwa namna bora zaidi, kwa wakati bora zaidi, kulingana na hekima Yake — si mipango yako.
Ukifanikiwa kumdanganya mtu, usidhani kuwa yeye ni mjinga. Tafakari tu ni kwa kiwango gani alikuamini, na wewe ukaivunja imani hiyo. Maumivu ya usaliti huwa makubwa kuliko udanganyifu wenyewe.
Chuki, husuda, wivu na kinyongo haviwaumizi wengine—vinamuumiza zaidi mwenye kuvibeba. Usijidanganye kwamba ni sumu kwa wengine; ni kama kunywa sumu ukitegemea mwingine afe. Ukweli ni rahisi: wewe ndiye unaathirika kwanza, kabla ya yeyote.
Miongoni mwa mafundisho ya Uislamu ni kudumisha uhusiano mzuri na ndugu zako. Kukata mawasiliano na familia si jambo jema—maisha yanaweza kufupishwa. Unganisha undugu, uongeze kheri na umri wenye baraka. 🤲
Katika dini zetu tumefundishwa kuwa Mungu hutujaribu kupitia mali, afya, familia na watoto. Hivyo tuwe na imani thabiti kwa Mwenyezi Mungu, tuvumilie na tusimame imara katika kila hali. 🤲
Usiwafanyie watu mabaya tu, bali pia usiwatamanie mabaya mioyoni mwako. Maana dunia ina mzunguko—unayotenda au kutamani kwa wengine, nayo hukurudia. Chagua wema kila wakati. 🙏
Binti katoka kuniomba kitita taslimu cha ELFU 15 mpaka nimeogopa hapa.
Naomba namba za Kamanda Muliro nikamshtaki nina hofu au anataka kupindua nchi? Pesa yote hiyo? Au anafadhili Magaidi, elfu 15 ni Utajiri wangu huo au anahisi Mimi ni Mhujumu Uchumi?😀
Ifike wakati wawe na huruma kwenye suala la pesa.