Chief Communication manager - TAMWA Zanzibar .
Freelance Journalist and Gender activist, Facilitator in Gender and Safely for female journalists and Mentor.
Wiki mpya, fursa mpya ya kuendelea kujenga jamii yenye usawa, haki na maendeleo jumuishi. 💙
TAMWA-ZNZ inaendelea kuhimiza ushirikiano wa jamii katika kupinga ukatili wa kijinsia, kuimarisha uongozi wa wanawake na kulinda haki za watoto na makundi mbalimbali.
Mabadiliko yanaanza na sisi. Tunawatakia wiki njema na yenye mafanikio! ✨
-------------------
A new week, a new opportunity to continue building an equitable, just, and inclusive society. 💙
TAMWA-ZNZ continues to encourage collective action to prevent gender-based violence, strengthen women’s leadership, and protect the rights of children and diverse groups in our communities.
Change starts with us. Wishing you a wonderful and a successful week ahead! ✨
#mwanamkenatabianchi
#Mwanamkenikiongozi
#stopgbv
Sisi TAMWA-ZNZ tunaanza na Mkurugenzi wetu Ms. Nairat Ali, yeye anatuhamasisha kwa uongozi na mchango wake katika kuendeleza utetezi wa haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.
Sasa ni zamu yako! Mtag kiongozi mwanamke anaekuhamasisha na umwambie kwa nini unathamini uongozi na mchango wake.
------------
At TAMWA-ZNZ, we are starting with our Director Ms. Nairat Ali, in recognition of her leadership and contribution to advancing the rights of women, children, and persons with disabilities.
Now it’s your turn! Tag a woman leader and tell her why you value her leadership and contribution.
Investing in young women’s leadership starts with building the right knowledge and skills.
TAMWA Zanzibar in collaboration with Zanzibar University (ZU), convened a stakeholder meeting to review the draft Women’s Leadership Curriculum, bringing together leaders from ZU Students' Government, lecturers, journalists, CSOs and other key stakeholders to provide valuable input before its implementation at the university.
The curriculum aims to equip young women with the knowledge, skills and confidence to actively participate in leadership and decision-making.
W-LEAD is implemented with support from UN Women and funding from the European Union under the WYDE Women’s Leadership Initiative.
#WLEAD
WYDEWomenLeadership
#Mwanamkenikiongozi
@unwomen
@euintanzania
@eucommissionofficial
@zanab1993_znz
TAMWA-ZNZ, kupitia utekelezaji wa Programu ya CADiR, inaendelea na mafunzo ya siku nne ya utengenezaji wa unga mchanganyiko wa lishe kwa wanachama wa vikundi vitano vya Kijaluba iSAVE kutoka Wilaya ya Kusini, Unguja.
Mafunzo hayo yanawashirikisha washiriki 120, wakiwemo wanawake na watu wenye ulemavu, kwa lengo la kuwajengea ujuzi wa vitendo utakaowawezesha kujiajiri, kuongeza kipato na kuimarisha shughuli zao za uzalishaji kwa maendeleo jumuishi na endelevu.
**********************************************Through the implementation of the CADiR Programme, TAMWA-ZNZ is conducting a four-day training on the production of nutritious composite flour for members of five Kijaluba iSAVE groups from South Unguja District.
The training brings together 120 participants, including women and persons with disabilities, to equip them with practical skills that promote self-employment, increase household income, and strengthen income-generating activities for inclusive and sustainable development.
Teknolojia na dunia ya leo zimebadilisha namna ya kufanya kazi.
Uongozi wa kisasa unahitaji maarifa, taarifa, ubunifu na uwezo wa kushirikisha watu. #MwanamkeNiKiongozi@TAMWA_Zanzibar
Kamati ya Wataalamu wa Masuala ya Habari Zanzibar (ZAMECO) imekutana kutafakari mafanikio ya nusu mwaka wa 2026 na kuweka mikakati ya kuendelea kuimarisha sekta ya habari hapa Zanzibar.
Kikao hicho pia kilishuhudia uchaguzi wa viongozi wapya wa kamati watakaoongoza juhudi za kukuza taaluma ya habari, uhuru wa vyombo vya habari na uwajibikaji katika sekta hiyo.
Hongera kwa viongozi waliochaguliwa na kila la heri katika majukumu yao mapya.
Pongezi kwa wahitimu 20 kutoka vikundi 7 vya Kijaluba iSAVE vya Unguja kwa kuhitimu mafunzo ya utengenezaji wa batiki na ushonaji, hii ni hatua muhimu kuelekea uwezeshaji wa kiuchumi na fursa mpya za maisha kwa watu wenye ulemavu.
Tunawatakia kila la heri katika safari yao mpya ya mafanikio. ✨
Jamii ya Shehia ya Kangani, Wilaya ya Mkoani Pemba, imepata fursa ya kujadili haki za watu wenye ulemavu, kwa kuangazia umuhimu wa elimu mjumuisho na ushiriki wao katika shughuli za kiuchumi.
Majadiliano hayo ni sehemu ya juhudi za kuendelea kujenga jamii inayotambua, kuheshimu na kuimarisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
#CADiR
@shijuwaza_znz @zanab1993_znz @nad_zanzibar @chavitahq @shivyawata @zafayco_
Wikiendi njema kutoka TAMWA ZNZ.
Tunapoingia katika mapumziko ya wikiendi, tuendelee kutafakari namna kila mmoja wetu anavyoweza kuchangia kujenga jamii salama, jumuishi na yenye usawa kwa wote.
Changamoto kubwa kwa watu wenye ulemavu si ulemavu wenyewe bali ni vikwazo vinavyowekwa na mazingira na mitazamo ya kijamii.
Tujitahidi kufungua milango ya ushiriki, ubunifu na mchango wa kila mmoja katika maendeleo.
Je wewe unachukua hatua hatua gani kuifanya jamii yetu iwe jumuishi zaidi?
@shijuwaza_znz @zanab1993_znz @zafayco_ @chavitahq @ShivyawataTz
Leo tunaadhimisha Siku ya Mtoto wa Afrika, siku inayotukumbusha wajibu wetu wa kuhakikisha kila mtoto anapata haki zake za msingi, ulinzi, elimu bora na fursa za kufikia ndoto zake.
Tuweke watoto mbele kwa kusikiliza sauti zao, kuwalinda dhidi ya aina zote za udhalilishaji na kuunda mazingira salama yatakayowawezesha kukua na kustawi.
#SikuYaMtotoWaAfrika #DayOfTheAfricanChild #TAMWAZNZ
Juni 16 ni Siku ya Mtoto wa Afrika.
Katika kuadhimisha siku hii muhimu, huu hapa ni ujumbe kutoka kwa Afisa Mkuu wa Programu wa TAMWA-ZNZ, Zaina Abdalla Mzee, akitoa rai kuhusu umuhimu wa kulinda, kuendeleza na kuhakikisha watoto wanapata haki zao za msingi kwa maendeleo yao na ya jamii kwa ujumla.
#DayOfTheAfricanChild
#stopgbv
Katika juhudi za kuimarisha upatikanaji wa takwimu sahihi na za wakati kuhusu masuala ya uongozi, TAMWA-ZNZ kwa kushirikiana na wadau wanaotekeleza Programu ya Kuimarisha Ushiriki wa Wanawake katika Uongozi (SWIL), imekutana na Maafisa Takwimu kutoka wilaya saba za Unguja katika ofisi za TAMWA-ZNZ, Tunguu.
Mkutano huo ulitoa fursa ya kujadili namna bora ya kuboresha ukusanyaji, uhifadhi na upatikanaji wa takwimu katika ngazi ya wilaya ili kuwezesha upangaji wa mipango na maamuzi yanayotegemea ushahidi.
Jumla ya Maafisa Takwimu 14 kutoka wilaya saba za Unguja walishiriki katika mkutano huo, ulioweka msingi wa kuimarisha mifumo ya takwimu na upatikanaji wa taarifa za uongozi kwa ufanisi zaidi.
#mwanamkenikiongozi
Leo tarehe 21 Mei 2026, TAMWA-ZNZ imekutana na viongozi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (ZU) kwa ajili ya kujadili fursa za ushirikiano katika kuimarisha ushiriki wa vijana wa kike katika nafasi mbalimbali za uongozi.
Mkutano huo ni sehemu ya jitihada za kuendelea kujenga uelewa na ushirikiano wa pamoja katika kuwawezesha vijana wa kike kushiriki kikamilifu katika maendeleo na nafasi za uongozi.
Sauti za mabadiliko zinaanza hapa ✨
Waandishi wa habari 40 kutoka Unguja na Pemba wameshiriki mafunzo maalum ya uandishi wa habari za uchambuzi kuhusu udhalilishaji na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na wasichana.
Mafunzo hayo yametolewa ikiwa ni utekelezaji wa programu ya TUNAWEZA PAMOJA yenye lengo la kutokomeza udhalilishaji hapa visiwani Zanzibar inayotekelezwa na TAMWA ZNZ na UN WOMEN kwa ufadhili wa Norway.