Haya safari njema huko Washington DC - ila hakuna namna ni lazima mpigwe tu
Madai yako palepale
#FreeTunduLissu#SamiaMustGo#KatibaMpya#Haki na Uwajibikaji kwa mauaji halaiki ya Oktoba
Labda kama umeenda kueleza mpango kazi wa kufanikisha haya madai yetu 🙃 si mbaya!
Otherwise utapigwa spana size kubwa!
WAPENDWA Jueni CCM kwenye kubaki madarakani yao moja - hakuna mwenye afadhali! Huyu Nchimbi haendi na Kombo kutupigania Washington DC - anaenda kuipigania liserikali lao haramu! 🚮
#TutaelewanaTu
Kama wewe ni Mtanzania diaspora na unaumia na mauaji ya October 29 ila mpaka leo haujatuma chochote kwa Chadema jijue wewe ni sehemu ya tatizo.
Chadema wanahitaji pesa ili kutusaidia Watanzania kupata haki. Hawalipwi ruzuku, wanatutegemea sisi wananchi.
Leo nimewatumia $1,000. Wewe diaspora mwenzangu ukiwatumia hata $10 inatosha.
Ila nyie bana mna mambo ya kiwaki !
Kumbe mlipanga kumfutia Lissu uhaini alafu nje kumkamata kwa kosa lingine na kumweka house arrest! 😁
Kila uovu mnaopanga Mungu 🙏🏽anatufunulia!
Nasema #TutaelewanaTu
Kuelekea Mkutano wa Hadhara wa kesho, tarehe 13 Juni 2026, utakaofanyika Iringa Mjini katika Uwanja wa Mwembetogwa, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, Mhe. @HecheJohn, atakuwa Mgeni Rasmi, leo tarehe 12 Juni 2026 amewasili mkoani Iringa na kuanza ziara yake ya kazi.
Mara baada ya kuwasili, Mhe. Heche alishiriki zoezi la kupandisha bendera za Chama katika Kata ya Kihesa, ikiwa ni sehemu ya kuendelea kuimarisha uhai na shughuli za chama ngazi za msingi.
Aidha, katika Kata ya Kihesa, amezindua Jiwe la Msingi la Tawi la Semutema A na amechangia kiasi cha shilingi 1,000,000 kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa Ofisi ya Kata ya Kihesa, akionesha dhamira ya kuimarisha miundombinu ya chama.
Wanachama, wapenzi, wafuasi na wananchi wote mnakaribishwa kujitokeza kwa wingi katika Mkutano wa Hadhara utakaofanyika kesho, tarehe 13 Juni 2026, katika Uwanja wa Mwembetogwa, Iringa Mjini.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinapenda kuuarifu Umma kuwa Alhamisi, tarehe 11 Juni 2026, Mahakama ya Rufani ya Tanzania jijini Dar es Salaam itasikiliza Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati ya Jamhuri na Mwenyekiti Tundu Antiphas Lissu.
DAR: Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA) kimetoa taarifa kuwa shauri la Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu, ambalo lilipangwa kuendelea Juni 11, 2026, limeahirishwa, litasikilizwa Julai 3, 2026, kisha Julai 6, 2026 itakuwa kwaajili ya kutolewa Hukumu na Orders.
Kwa mujibu wa taarifa ya Mahakama ya Rufani, shauri hilo limepangwa kuendelea kwa ajili ya kutoa hukumu, maamuzi na amri.
Ikumbukwe Lissu alifunguliwa mashtaka ya uhaini Aprili 2025, akidaiwa kutoa kauli zilizolenga kuhamasisha Wananchi kuzuia au kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa 2025, tangu wakati huo, amekuwa mahabusu huku kesi hiyo ikiendelea kusikilizwa katika Mahakama Kuu ya Tanzania mbele ya jopo la majaji watatu.
Soma https://t.co/f9G3KI0OdJ
#JamiiForums #Governance #JFSheria
"Nitoe wito kwa Jaji Mkuu na Jaji Kiongozi kama watendaji na viongozi wanaosimamia muhimili wa mahakama katika majukumu, siyo tu ya usimamizi wa haki na majukumu ya kiutawala kuweza kuingilia kati jambo hili, ili mahakama kwa ujumla wake isipate aibu ya kuonyesha kwamba imeshiriki njama za kudhibiti watu kuwepo kwenye mahakama ya umma ambayo ni mahakama ya wazi." Mhe. @jjmnyika
Kwanini kesi ya Mwenyekiti wetu isogezwe mbele kwa mda mrefu kiasi hiki mara tu baada ya chama kueleza mpango mbovu wa polisi hapo kesho.
Chama kimeeleza nia ovu ya polisi dhidi ya chama chetu alafu kesi inasogezwa mbele!!!
Mahakama ya Tanzania inaondoa imani ya wananchi na kuchochea chuki kwa matendo kama haya.
Kesi ya Mwenyekiti Tundu Lissu Sasa itakuwa tarehe 3 Julai 2026 na si kesho tarehe 11 Juni 2026.
Tundu Lissu's revision case at the Court of Appeal of Tanzania has been rescheduled to the 3rd of July 2026 instead of June 11 2026.
Halafu Msajili wa Vyama vya Siasa Francis Mutungi na Naibu wake Sisty Nyahoza hawaoni kuwa hizi ni kauli za kibaguzi na za kikaburu zinaonyesha kuwa CCM ni chama cha Kibaguzi kinachotakiwa kufutwa mara Moja. Kazi yao isiyokwisha ni kuisakama na kuisulubu Chadema. AIBU MBONA AIBU!
Kesho walipanga kujaza Mapolisi waje kufanya fujo na kupiga watu Mahakamani kwenye kesi ya Mhe. Lissu ila walipoona Katibu Mkuu Mhe. @jjmnyika kasema kuhusu mipango yao michafu dhidi yetu kwa aibu kubwa wameona waweke mpira kwapani na kusogeza kesi mbele.
Ni wazi kuna Collabo kali katika ya Mahakama, Jeshi la Polisi na Serikali haram ndo maana leo wamepiga simu moja tu na Mahakama ikakubali kusogeza kesi mbele.
Yani Tanzania hatuna Mahakama, hatuna Bunge wala Serikali ila kuna genge la vibaka ambao wanaendesha nchi yetu wanavotaka kinachoniuma ni kwamba hawa wauaji hatukuwachagua bali walijiweka madarakani baada ya kuuwa kwa risasi Watanganyika wenzetu zaidi ya elfu kumi.
Kata ya Idukilo wilaya ya Kishapu, Mkoa wa Shinyanga. Iko jirani na Maganzo Magharibi ya Mwigumbi.
Wananchi wamemkataa Diwani fake wa ccm aliejiweka madarakani 2025…
Tangu wakati huo wananchi hawamtaki.
RPC Shinyanga amepeleka Oparesheni hapo, mamia ya watu wamepigwa na kuumizwa wengine zaidi ya 150 wana kesi mahakani Kishapu..
Uonevu huu haukubaliki.
Nimeelekeza Mawakili wa chama waingilie kati na chama ngazi ya kanda wafanye mkutano Idukilo kuzungumza na wananchi.
RPC Shinyanga sio wajibu wako kisheria kulazimishia wananchi Kiongozi wasiemtaka ambae hawajamchagua.