Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anauita "wakati wa kihistoria" kwa Kanisa Katoliki, na anapanua "ujumbe wa udugu". "Naomba papa huyu mpya awe wa amani na matumaini," anasema.
#UPDATES: Moshi mweupe umeonekana ukifuka kutoka kwenye bomba la moshi katika Kanisa la Sistine Chapel, ni wazi mchakato wa upigaji kura umekamilika na makadinali wamemchagua mrithi wa Papa Francis. #PopeFrancis#PopeElection
Uongozi wa Klabu ya Yanga umesema msimamo wa Klabu hiyo juu ya mchezo namba 184 wa Ligi Kuu msimu huu uko palepale kuwa hawatashiriki kwenye mchezo huo kwa namna yoyote ile.
#sports#npointtzupdates#npointtzsports
Beki wa kulia wa Uingereza, Trent Alexander-Arnold, amethibitisha kuwa ataondoka na kuikacha mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, Liverpool, mwishoni mwa msimu.
#Liverpool#sports#michezo
Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamua kuwekeza kwenye sekta ya madini ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kupata kipato na kujikwamua kiuchumi.#majaliwa#TanzaniaYaSamia#npointtz#npointtzupdates
Maafisa wa polisi eneo la Kuria Magharibi, Kaunti ya Migori, wamewakamata watu watatu wanaoshukiwa kumrushia kiatu Rais William Ruto alipokuwa akiwahutubia wakazi wa eneo la Kehancha siku ya Jumapili.
UJENZI NI BAJETI YA KAZI NA UTU
Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, amewasilisha bungeni bajeti ya wizara yake ambayo imeahidi ujenzi zaidi wa barabara na madaraja nchini – huku akisisitiza uchapakazi zaidi na utu kwenye utekelezaji wa miradi.
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Heche amewataka Wanachama wa Chama hicho na Wananchi kwa ujumla kufika kwa wingi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu siku ambayo Mwenyekiti wa Chama hicho Tundu Lissu atafikishwa Mahakamani April 24.
Chama cha ACT Wazalendo leo Unguja, Zanzibar kupitia Kiongozi wake Doroth Semu, kimetangaza rasmi kushiriki katika ngazi zote za uchaguzi mkuu wa Tanzania unaotarajiwa kufanyika October mwaka 2025.
OFISI ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) imewasilisha bungeni makadirio ya mapato kwa mwaka 2025/26 yenye takribani Shilingi trilioni 11. 783 kwa ajili ya wizara na taasisi zilizo chini yake.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (#CHADEMA), #TunduLissu amefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa shitaka la Uhaini.
Lissu amefikishwa Mahakamani na kusomewa shitaka hilo huku kesi ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025.#FreeTunduLissu
Katibu Mkuu Wizara ya michezo Gerson Msigwa ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, amethibitisha Uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es salaam kufungwa kwa muda kuanzia jana April 9 2025 ili kupisha marekebisho katika eneo la kuchezea. #sports#MICHEZO#TANZANIA
Hadi kufikia Februari, 2025, abiria 1,809,983 wamesafirishwa [treni ya SGR] na jumla ya shilingi bilioni 54.9 zimekusanywa. Uwepo wa huduma hiyo ya treni, umepunguza muda wa safari kati ya Dar es Salaam na Dodoma kutoka wastani wa saa 10 kwa basi hadi kati ya saa tatu na nne.
Klabu ya Yanga leo Februari 11, 2025 imetimiza miaka 90 tangu kuanzishwa kwake rasmi mwaka 1935, na ndiyo klabu yenye mafanikio zaidi kwenye soka la Tanzania ikiwa imeshinda ubingwa wa Ligi Kuu mara 30.
#UPDATES: Kilevi kipya cha kienyeji kimekutwa kikitumiwa na watoto wadogo wanaokadiriwa kuwa na miaka kumi kushuka chini.
Kilevi hicho kilichogunduliwa kuwa ni Mafuta ya Ndege kimeonekana kikitumika na watoto hao katika baadhi ya miji nchini Kenya.
#npointzaidiyahabari
Msigwa ameiba siri zangu na kuzipeleka CCM maneno ya @TunduALissu wakati akifanya mahojiano katika studio za @npointtz twende youtube kwa account hiyo tutazame mahojiano haya yaliyo fanywa na mwandishi wetu @shirati_george .@Twaha_Mwaipaya
Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ameshiriki zoezi la kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa katika kitongoji cha Sokoine Kijiji cha Chamwino Mkoani Dodoma, leo tarehe 27 Novemba, 2024. #npointtz#npointtzupdates#election#uchaguzi
Sengasu amesema kwa sasa imefika wakati wanawake wajitambue lakini pia wanaume waone thamani ya mwanamke na kumjali kwa kile hata kidogo alichofanya Mwanamke. #npointzaidiyahabari@polisi.tanzania @sengasuzainab_ @gwajimad
#UPDATES: Baada ya kusambaa kwa Tukio la Binti mwenye umri wa miaka 16 kufanyiwa unyanyasaji huko wilayani Longido na mwanaume aliyemupa akimtuhumu kuwa Binti huyo kwanini anachelewa kupata Ujauzito, Jeshi la polisi kuptia maafisa wake mbali mbali akiwemo
A/Insp Zainabu Sengasu ambae ni mkaguzi msaidizi wa Kata ya Namanga Wilaya ya Longido Mkoa wa Arusha ametoa Ujumbe Mzito kwa Wanawake na wakazi wa Longido. Katika kuelekea siku 16 za kupinga ukatili,